Kumekucha: CCM kuwafungia Maisha wagombea watakaokutwa na hatia ya rushwa kwenye uchaguzi mkuu

Rushwa ndani CCM katika chaguzi ni sawa kabisa na maji na samaki, kutolewa kwa kauli hakuonyeshi uhalisia wowote, bali porojo kama tulizozoea kuzisikia kutoka kwa makada mbalimbali ktk nyakati kama hizi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Eti mtu anasimama na kusema,

Mikutano ya kisiasa haijakatazwa,

Wabunge na Madiwani wanafanya mikutano kwenye maeneo waliyoshinda.

Ni Sheria gani imetumika? Kimya.

Vyama ni vya Kitaifa si vya Majimbo wala Kata.

Anasimama na kusema Tume ya Uchaguzi ni huru hata Katiba na Sheria zinatamka hivyo.

Atuambie haya maneno yalitamkwa na nani?

"Nikuteue Mimi, mshahara nikulipe Mimi, gari la kutembelea nikupe Mimi, halafu wewe umtangaze mpinzani ameshinda hiiiiiiiiiiiiii!!!!!!!!

Hapo Tume iko huru kiutendaji au iko huru kwenye Katiba na Sheria tu?
 
CCM imetoa onyo kwa wagombea wake wote wa uchaguzi mkuu kwamba yoyote atakayepatikana akitoa rushwa atafungiwa maisha yake yote kushiriki uchaguzi kupitia chama hicho.

Hii ni hatua muhimu sana katika kudhibiti wale wote wenye nia ya kununua nafasi za uongozi.

Source Mtanzania Jumapili
Hii iwe kwa uchaguzi mkuu, watunge sheria. Zito ni fisadi. Hafai.
 
Hakuna kitu siku hizi kinanikosesha amani katika siasa za nchi hii kama hizi kauli nyepesi kuhusu kudhibiti rushwa. Rushwa ni kansa na inasikitisha kuwa mapambano dhidi ya tatizo hili yamegeuzwa kuwa siasa. Ingawa rushwa imekuwepo siku zote katika miaka ya karibuni hali imebadilika kutokana na kutamalaki kwa rushwa ya kisiasa. Awamu ya tano ilipoanza na kuahidi kuwa vita dhidi ya rushwa itaimarishwa nilitarajia kuwa ile taarifa ya Mzee Warioba kuhusu kero ya rushwa itakuwa ndiyo rejea. Kinyume chake sijawahi hata kumsikia kiongozi yeyote akiizungumzia hiyo taarifa. Badala yake tumeona vita dhidi ya rushwa ikiendeshwa kisiasa na kwa kuchagua. Tumeona pia wadau muhimu sana kwa vita hii wakiwekewa vikwazo na kushindwa kusaidia kufanikisha mapambano dhidi ya rushwa. Matokeo yake vita dhidi ya rushwa imebaki kuwa jukumu la mdau mmoja tu: serikali. Tumeona serikali nayo ikishughulikia tatizo hili kisiasa zaidi kuliko kitaalam. Matokeo yake rushwa katika siasa imeshika kasi ikiwa ni pamoja na rushwa ya kupeana vyeo katika siasa, uongozi na utumishi wa umma. Imefikia mahali wabunge walituhumiwa kupewa rushwa na serikali na tuhuma hizo zilipowekwa hadharani bungeni kiti kilizuia mtuhumiwa (serikali) kutoa maelezo na ikiwezekana kujisafisha. Kibaya zaidi na kilichonikatisha tamaa ni pale nilipotazama "body language" na kusikia kauli ya rais kuhusu tuhuma za wabunge kuhongwa! Kwa hali sijui watu wanapata wapi ujasiri wa kuwaambia wananchi lolote kuhusu vita dhidi rushwa? Tukubali tu kwamba vita ya dhati dhidi ya rushwa tumeiahirisha hadi wakati mwingine. Kinachofanyika sasa ni maigizo tu yakiwa na lengo pia la kuweka mazingira ya kuwashughulikia wanasiasa wasiotakiwa.
 
CCM imetoa onyo kwa wagombea wake wote wa uchaguzi mkuu kwamba yoyote atakayepatikana akitoa rushwa atafungiwa maisha yake yote kushiriki uchaguzi kupitia chama hicho.

Hii ni hatua muhimu sana katika kudhibiti wale wote wenye nia ya kununua nafasi za uongozi.

Source Mtanzania Jumapili
Mzee Mgaya! je wale wagombea wanaopitishwa na ccm alafu kwa kuhofia ushindani mkali wanahonga wapinzani ili wapite bila kupingwa hii inawahusu? Kama wakati ule ilivyokuwa kwenye jimbo LA chato

Au onyo ni marufuku rushwa ndani ya ccm kwa maccm tu. Ikitokea liccm limehonga wapinzani na kukipa chama ushindi haramu, hiyo ni ruksa

Kwa jinsi sisi maccm tulivyo wanafiki tunachukia rushwa inapotolewa na mccm kwa mccm lakini ikitolewa na mccm kwa mpinzani sawa tu
 
CCM imetoa onyo kwa wagombea wake wote wa uchaguzi mkuu kwamba yoyote atakayepatikana akitoa rushwa atafungiwa maisha yake yote kushiriki uchaguzi kupitia chama hicho.

Hii ni hatua muhimu sana katika kudhibiti wale wote wenye nia ya kununua nafasi za uongozi.

Source Mtanzania Jumapili
Is it? Basi nihabari njema kama itafanyiwa kazi.
 
CCM imetoa onyo kwa wagombea wake wote wa uchaguzi mkuu kwamba yoyote atakayepatikana akitoa rushwa atafungiwa maisha yake yote kushiriki uchaguzi kupitia chama hicho.

Hii ni hatua muhimu sana katika kudhibiti wale wote wenye nia ya kununua nafasi za uongozi.

Source Mtanzania Jumapili
Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu
 
CCM imetoa onyo kwa wagombea wake wote wa uchaguzi mkuu kwamba yoyote atakayepatikana akitoa rushwa atafungiwa maisha yake yote kushiriki uchaguzi kupitia chama hicho.

Hii ni hatua muhimu sana katika kudhibiti wale wote wenye nia ya kununua nafasi za uongozi.

Source Mtanzania Jumapili
Haitatokea milele na milele
 
Back
Top Bottom