View attachment 16689View attachment 16690
Hii picha uliyoonyesha siyo ya leo, hiyo ilikuwa kipindi cha kampeni.
View attachment 16689View attachment 16690
Hii picha uliyoonyesha siyo ya leo, hiyo ilikuwa kipindi cha kampeni.
sidhani km ni picha ya leo hii. inataka uvumilivu wa ziada kusalimiana kwa bashasha namna hii.
Wow... Ha ha ha
Yaani huyu kilaza sitaki hata kumuona!
Jamani iweni na adabu!!!, maswali ya nini !!!asante mkuu!
Mheshimiwa Mbunge... Kupitia viti maalum CCM.Jamani huyu vick kamata ndiye nani? what is specialties in her?
[/ATTACH]View attachment 16690
Hii picha uliyoonyesha siyo ya leo, hiyo ilikuwa kipindi cha kampeni.
Naona yuko na Mbunge mpya wa Umoja wa Vijana wa CCM, mkoa wa Arusha, Catherine Magige. Ama siyo yeye?
Kama ndiye magazeti ya Shigongo yalimripoti hivi:
Kwa mujibu wa vyanzo makini vya Risasi, baada ya Catherine ‘Catty' kutwaa nafasi hiyo, anaingia bungeni kwa nia moja tu, kuhakikisha sera za CCM zinafanya kazi kwenye uwakilishi wake, UV-CCM.
"Yale ambayo uliwahi kusikia marehemu Amina Chifupa akiyafanyia kazi, atayachukua yote na kwenda nayo mpaka mafanikio yake," kilisema chanzo chetu.
Mheshimiwa huyo mtarajiwa ambaye jina lake la utotoni ni Pamela inaelezwa kwamba, kifo cha Amina ndicho kilichomsukuma kuchukua maamuzi magumu ya kujitosa kwenye ubunge ili kuyaendeleza mazuri yote ya marehemu.
"Unajua marehemu (Amina) alikuwa mwanaharakati wa kufanya mapambano ya kutetea jamii, hasa vijana, kifo chake kikakatisha mafanikio yake, sasa ilikuwa lazima azaliwe Amina mwingine ili kuyaendeleza, ni Catty," kilisema chanzo kingine cha Risasi.
Ikazidi kuwekwa kweupe kwamba, Catherine ambaye aliandika barua ya kuacha kazi rasmi katika Benki ya Barclays jijini Dar, Desemba 2009 (Risasi lina nakala yake) ili kujipanga na Ubunge na mapambano ya kutetea jamii husika huku ikielezwa kwamba siyo mtu wa kurudi nyuma katika harakati zake.
Chanzo hicho kiliendelea kuweka wazi kwamba, wako waliokuwa na dalili ya kumvunja moyo, "lakini pia wapo waliokuwa wakimtia moyo," kilisema chanzo hicho.
Kwa mujibu wa ‘dokumenti' zinazoshikiliwa na Risasi bila ridhaa yake, Catty alimaliza masomo ya Uandishi wa Habari mwaka 2004 katika Chuo cha Dar es Salaam (DSJ).
Hata hivyo, Risasi Jumatano lina ‘kopi' za vyeti vyake vyote ambavyo havina chembe hata moja ya ‘kufojiwa', kuanzia vile vya shule ambapo kuhusu elimu ya Sekondari, ilibainika kwamba, mwaka 1999 alimaliza Sekondari ya Mtakatifu Joseph (Saint Joseph), Ngarenaro, Arusha.
Mwaka 2004 alisoma Chuo cha Institute for Information Technology (IT), Dar kabla ya mwaka 2006 kusomea masomo ya Biashara (CBE), pia jijini Dar. Kote huko alitunukiwa vyeti vya kufuzu (Risasi lina nakala zote).
Mheshimiwa Catty ana mtoto mmoja wa kike aliyemzaa mwaka 2002, ambapo kwa mujibu wa chanzo chetu, kama kuna watu wanadhani ‘amefoji' vyeti, ni vyema wakaenda kwenye taasisi hizo ili kupata ukweli, lakini kwake, "anaendelea kupambana kwa nafasi yake hiyo," kilisema chanzo hicho.
Mheshimiwa Catty alizaliwa mwaka 1981 kama marehemu Amina huku wote wakipata mtoto mwaka 2002. Wana ‘nafsi' moja ya kutumikia vijana huku wote kauli mbiu yao ikiwa moja, ‘mapambano mbele daima'.
Marehemu Amina alikuwa mbunge wa Viti Maalum kupitia Umoja wa Vijana wa CCM kati ya mwaka 2005-2007 alipofariki dunia. Alizikwa mkoani Njombe (wakati huo wilaya) kwenye Kijiji cha Lupembe ambapo ameacha mtoto mmoja.