Kumbukumbu Ajali MV Bukoba Serikali imejifunza Umuhimu wa Ubora Vyombo vya Kusafiria? Inawajibika vya kutosha kupunguza ajali nchini?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
MV Bukoba.jpg


Leo tarehe 21/05/2023 ni kumbukumbu ya ajali mbaya ya meli Buboka, ajali iliyosababisha pigo kubwa kubwa kwa watanzania waliopoteza na wapendwa wao kwenye ajali hiyo iliyotokea 21/05/1996. Tukio hili lilisababisha vifo vya watu zaidi ya 800 limeendelea kuwa kumbukumbu mbaya na yenye maumivu makali kwa wote waliopoteza wapendwa wao lakini funzo kubwa kwa serikali na watu wote kwa ujumla umuhimu wa ubora kwenye vyombo vya kusafiria.

Mwaka 2023 bado kuna uzembe mwingi linapokuja ubora na usalama wa vyombo wa kusafiria na uwajibikaji pindi zinapotokea ajali. Kuna uzembe mwingi kwenye ukaguzi kwa wanaotakiwa kuhakikisha sheria inafatwa kuhakikisha usalama kwa watu wanaotumia vyombo hivi.

Lakini pia Rushwa na Upigaji ni maadui wakubwa wanaorudisha nyuma juhudi za kupunguza na kutokomeza ajali nchini. Inasikitisha kuona hata ilipotokea ajali ya ndege Bukoba juzi tu hapa bado tuna hali mbaya kwenye uokozi pindi inapotokea ajali, na wananchi ndio wamekuwa msaada mkubwa kusaidia kwenye uokozi na vyombo vyao duni ambavyo si salama kwa shughuli hiyo.

Pia soma 👉 Zijue ajali kubwa zilizowahi kutokea Tanzania

Kwa maoni yako, serikali inawajibika vya kutosha kuhakikisha ajali zinapungua na kuisha kabisa nchini?
 
Tumuombe MUNGU ailinde Bukoba.
1. Ajali ya meli kuzama
2. Tetemeko la ardhi.
3. Ajali ya kuanguka ndege.
Maombi ni muhimu. Mwenyezi MUNGU tunakuomba uepushe ajali
mbaya mkoani Kagera. Amina
 
Back
Top Bottom