Kumbe sababu ya kifo cha Mkapa ni Cardiac Arrest. Asante sana mwanafamilia William Erio kumaliza sintofahamu hii

Urio ni mchaga na mkapa ni mmakonde ile haikuwa kauli thabiti ya familia bali walikurupuka ingawa sasa wanajuta
Kwani kuwa mwanafamilia ni lazima uwe kabila moja na muhusika? Waswahili tunasema mjomba ni mama lakini wewe na mjomba wako mnaweza kuwa makabila tofauti. Mama yako mzazi mnaweza kuwa makabila tofauti.

Naomba pia nikukumbushe kuwa mama Anna Mkapa ni mchagga
 
Wanabodi,
Kumbe sababu ya kifo cha Mpendwa wetu, Benjamin William Mkapa ni Cardiac Arrest!.

Asante sana Mwanafamilia wa familia ya Mkapa, William Erio, kuusema ukweli huu na kumaliza rasmi ile sintofahamu ya chanzo cha kifo, ambayo imezua mijadala kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo JF.

Kama Tangazo la kifo lingezingatia sheria tangu pale mwanzo, wala kusingetokea sintofahamu yoyote!.

Hivyo japo haijasemwa ni JF, lakini amini usiamini, mabandiko kama haya

Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Japo yanalaumiwa kwa kuonekana watu wana mind vitu vidogo vidogo ambayo sio vya msingi, lakini yanasaidia.

Chanzo cha kifo cha ghafla cha any state leader ambaye hajawahi kutamkwa kusumbuliwa na maradhi yoyote, automatically kita send a shock wave kwenda viral.

Baada ya kauli hii, sasa minongo yote kuhusu chanzo cha kifo imemalizwa rasmi.
Naombeni sana, wanabodi, tuwe na heshima kwa viongozi wetu na tuwe na heshima kwa marehemu, mkiisha ambiwa ukweli wa familia, then tuupokee ukweli huu, tuuamini, na kumheshimu Marehemu kwa kuto toa comments zozote negative based on hisia!.

RIP, Mhe. Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa.

Paskali
basi sawa... but yule nanii wa hapo Bujumbura walisema eti ni "heart attack". na mama wa kwanza alikuwa Nairobi kwa matibabu dhidi ya mdudu "equalizer".

yaani!
 
Wanadai alilazwa sababu ya Malaria so cardiac arrest imempitia usiku...!! Mtu alazwi sababu ya cardiac arrest ile inakupigaa na kukukaushaa chap hakuna cha CPR wala dawaa...
 
Attachments

  • Screenshot_20200727-231726.png
    Screenshot_20200727-231726.png
    110.1 KB · Views: 1
Tangu lini cardiac arrest ukawa ugonjwa, magonjwa yote yanayosababisha kifo lazima yatapelekea moyo kusimama na hiyo ndo inaitwa cardiac arrest, sasa nyie waandishi makanjanja wa kibongo mnajitia ujuaji kwenye mambo ambayo hamna uelewa hata chembe kujitafutia cheap popularity, kwa nini msiulize wataalamu kwanza, bullshit..
Basi hujui maana ya cardiac arrest; na usiombe ikukute, kwa sababu ndiyo chanzo kikuu cha vifo tunavyoita vya ghafla.
 
"Kichuguu, post: 36153031, member: 348"]
Umeandika maneni mengi lakini hayana mantiki kabisa; kwa mfano unaponiluliza kuhusu ushiano wa cardiac arrest na malaria inaonyesha ama hujui maana ya cardiac arrest au hutaki kuamini yaliyosemwa na nduugu tu.
Ni kweli kabisa mkuu, mimi sijui cardiac arrest kama ugonjwa. Ninafahamu kwa utaalam maana ya cardiac arrest , ina presentation gani, sababu za kutokea na kwanini. Hapo sibebi maelezo ya kienyeji, reja reja au kwa kuchuuza! nope.
Wanaoamini ugonjwa wa cardiac arrest waendelee kuamini sina tatizo
Cardiac arrest haina uhusiano na kitu kingine chochote bali mwili wenyewe. Na wala hakuna aliyesema kuwa cardiac arrest hiyo imesababishwa na Malaria; taarifa zilizoko ni kuwa alilazwa hospitali kwa sababu ya Malaria, na amepatwa na cardiac arrest akiwa hospitali; ingeweza kumkuta akiwa nyumbani au mahala pengine popote pale. Cardiac arrest huwa haina symptoms zozote; ni kitu cha ghafla tu. Ili upate resuscitation inabidi CPR ifanyike mara moja, ukishachelewa muda wa kama nusu saa basi, mgonjwa haponi tena. Halafu pia CPR huwa haina gurantee hasa watu wa zaidi ya miaka 65; ni kama 10-15% tu wanaopona. Mkapa alikuwa na miaka 81 na tena overwheight. Wewe huna record za afya yake na wala hujui alikuwa anatibiwa wapi maiak 15 iliyopita tangu atoke madarakani.
Mkuu naomba usiendelee kujibu mambo ya kitaalamu kwa utalaam binafsi.
Maelezo haya yana matundu mengi sana kwa wanaojua haya mambo. Nitakupa tu dondoo za matundu
1. Cardiac arrest inaweza kuwa na uhusiano na mwili au kitu kingine kutokan nje. Hili elewa tu bila ubishi
2. Kuhusu symptoms inategemea unaongelea sababu zipi zilizosababisha kutokea
3.Hakuna muda wa resusciation kama nusu saa unayosema, inategemea pia nini sababu mkuu!
4. CPR haina gurantee kwa 65, (10-15) una literature za kutosha kuhusu hili?
5. Mkapa alikuwa na 81, wewe uliwezaje kujua kama ni overweight? kwa kipimo gani mkuu! usiseme alionekana
6. Kama maelezo yako ni ''sahihi'' Mkapa alikuwa Hospitali, hivyo CPR isingesubiri nusu saa usemayo! contradiction
Mimi siyo mtu wa conspiracies na wala "sikukomalia malaria.
Sina theory ya aina yoyote ile, nilikuwa kimya. Nimechangia kutokana na wimbi la upotoshaji unaondelea kutokana na maelezo nusu nusu
Hakuna ugonjwa unaoitwa cardiac arrest. Sheria inayotawala vifo vya viongozi haikutumika vema!
Pamoja na yote hayo tunamuombea kwa mwenyezi mungu ampokee mzee wetu Mkapa ! Amen

Kwangu sina zaidi.
 
Basi hujui maana ya cardiac arrest; na usiombe ikukute, kwa sababu ndiyo chanzo kikuu cha vifo tunavyoita vya ghafla.
Mkuu mbona Nyumisi kaeleza vizuri! Tunakubaliana na ughafla wa cardiac arrest na tunakubali ni chanzo cha matatizo ya vifo vya ghafla.
Mkuu hakuna ugonjwa wa cardiac arrest! mbona hili lipo wazi?
Kuna matatizo yanayoweza kupelekea cardiac arrest.

Msome Nyumisi vizuri na maelezo ya watu wengine! tatizo liko wapi mkuu!
 
Mkuu mbona Nyumisi
Mkuu hakuna ugonjwa wa cardiac arrest!
Hii kwa lugha ya kistaarabu wengine husema hii ni rush to judgement lakini maana yake hasa ni poor reasoning, yaani mtu anayechukua maneno na kuyaungaunga ili atoe story anayotaka ikiwa hiana uhusinoa na story halisi.

Ni wapi mimi Kichuguu nimesema kuwa Mkapa alikuwa "anaumwa ugonjwa cardiac arrest"? Au ni wapi ndugu wa marehemu au wafanya kazi wake wa Mkapa Foundation waliposema kuwa alikuwa anaumwa ugonjwa wa cardiac arrest?

Wametupa taarifa kuwa Mkapa alikuwa hajisikii vizuri, akaenda hospitali, akakutwa na Malaria, hivyo akaanza matibabu ya malaria. Halafu alipokuwa akiendelea vizuri na matibabu akitegemea kuondoka hospitali kuendelea na mikutano yake ya kawaida akapatwa na cardiac arrest baada ya kusitikiliza taarifa ya habari ya saa mbili usiku. Wewe unataka kubadilisha kusema kuwa cardiac arrest ni ugonjwa wakati ile ni matokeao ya health conditions siyo disease?

Sikiliza huyu ni mtoto wa Mkapa; je nyie wote mnaopinga tarifa zake mnajua ukweli zaidi yake?

Kuna video clips kadhaa nimeziangalia hapo youtube kukiwa na mfanyakazi wa Mkapa Foundation aliyekuwa anaandaa mkutano wa marais wastaafu wa nchi za maeneo yetu na askofu aliyekuwa na appointmemt na Mkapa wote wanasema lile lile halafu eti wanakuja hapa wana JF waajuaji zaidi wa kufikirika tu, hii ni aibu sana kwa JF.
 
Tangu lini cardiac arrest ukawa ugonjwa, magonjwa yote yanayosababisha kifo lazima yatapelekea moyo kusimama na hiyo ndo inaitwa cardiac arrest, sasa nyie waandishi makanjanja wa kibongo mnajitia ujuaji kwenye mambo ambayo hamna uelewa hata chembe kujitafutia cheap popularity, kwa nini msiulize wataalamu kwanza, bullshit..
Basi hujui maana ya cardiac arrest; na usiombe ikukute, kwa sababu ndiyo chanzo kikuu cha vifo tunavyoita vya ghafla.
Mkuu Kichuguu usiwe na jazba, hoja inajibiwa kwa hoja.

Hapo juu maelezo yako hayana shaka 'cardiac arrest' ni maradhi.
Sisi tunakwambia hapana si maradhi ni matokeo ya tatizo au matatizo mengine

Clip na maneno mengine hayaondoi ukweli kuwa ' cardiac arrest' si ugonjwa ni matokeo ya matatizo

Mkuu kichuguu mimi sitegemei hadithi, nayafahamu haya mambo na nikikwambia nayafahamu ninayafahamu hasa.

Ili kuongelea moyo unapaswa ujue mambo mengi, nikikutajia utachanganyikiwa.
Unajua anatomy na physiology ya moyo, cardiac arrhythmia, unajua myocardial infarction, unajua angina, unajua CHF, unajua ion exchange katika heart muscle, unajua coronary artery na uniqueness yake, unaijua aorta wewe. Unajua heart valves

Ushawahi kusikia kitu kinaitwa biochemistry au pathophyisology.Sasa haya ni tone tu ndani ya ndoo ya elimu ya moyo. Kuna mahali umeongelea symptoms, sijui kama unajua tofauti ya symptom na sign

Ninahakika hujui kwasababu hata homa utaita ugonjwa wa homa!
Kwa taarifa hakuna ugonjwa wa homa Homa ni dalili ya ugonjwa (symptom).
Haitokei homa bila sababu. Ndiyo maana tunakushangaa na ''cardiac arrest'' .

Mkuu haya yanahitaji ukae darsa , hayahitaji kusikia na clip za mitandaoni.

Kama unasema kuna ugonjwa unaitwa cardiac arrest, basi kuna siku utatuambia kuna ugonjwa unaitwa edema, mwingine gallop rythm! mwingine mitral valve regurgitation, emboli au embolism n.k. hapo watu ni kicheko pwaaaaa!

Mkuu , wewe ongeleaa malaria na mbu mmoja kama ile post uwape watu siku.

Huku kwenye moyo kaa mbali,ninakusitiri mkuu jisetiri mwenyewe.
 
Ukiona wanakazia sana na kutoa mimacho ujue waongo. Alietakiwa kutaja sababu ya kifo kisheria ni Rais alishindwa .Hajasema hapo bado hatujui sababu. Mimi nasema Mzee alishindwa kuendelea kuishi ndio sababu.
 
Hii kwa lugha ya kistaarabu wengine husema hii ni rush to judgement lakini maana yake hasa ni poor reasoning, yaani mtu anayechukua maneno na kuyaungaunga ili atoe story anayotaka ikiwa hiana uhusinoa na story halisi.

Ni wapi mimi Kichuguu nimesema kuwa Mkapa alikuwa "anaumwa ugonjwa cardiac arrest"? Au ni wapi ndugu wa marehemu au wafanya kazi wake wa Mkapa Foundation waliposema kuwa alikuwa anaumwa ugonjwa wa cardiac arrest?

Wametupa taarifa kuwa Mkapa alikuwa hajisikii vizuri, akaenda hospitali, akakutwa na Malaria, hivyo akaanza matibabu ya malaria. Halafu alipokuwa akiendelea vizuri na matibabu akitegemea kuondoka hospitali kuendelea na mikutano yake ya kawaida akapatwa na cardiac arrest baada ya kusitikiliza taarifa ya habari ya saa mbili usiku. Wewe unataka kubadilisha kusema kuwa cardiac arrest ni ugonjwa wakati ile ni matokeao ya health conditions siyo disease?

Sikiliza huyu ni mtoto wa Mkapa; je nyie wote mnaopinga tarifa zake mnajua ukweli zaidi yake?

Kuna video clips kadhaa nimeziangalia hapo youtube kukiwa na mfanyakazi wa Mkapa Foundation aliyekuwa anaandaa mkutano wa marais wastaafu wa nchi za maeneo yetu na askofu aliyekuwa na appointmemt na Mkapa wote wanasema lile lile halafu eti wanakuja hapa wana JF waajuaji zaidi wa kufikirika tu, hii ni aibu sana kwa JF.
Mkuu wangu JF ya sasa si ile tuijuayo ,hii sasa ni sijui ikoje
 
Mkuu Kichuguu usiwe na jazba, hoja inajibiwa kwa hoja.

Hapo juu maelezo yako hayana shaka 'cardiac arrest' ni maradhi.
Sisi tunakwambia hapana si maradhi ni matokeo ya tatizo au matatizo mengine

Clip na maneno mengine hayaondoi ukweli kuwa ' cardiac arrest' si ugonjwa ni matokeo ya matatizo

Mkuu kichuguu mimi sitegemei hadithi, nayafahamu haya mambo na nikikwambia nayafahamu ninayafahamu hasa.

Ili kuongelea moyo unapaswa ujue mambo mengi, nikikutajia utachanganyikiwa.
Unajua anatomy na physiology ya moyo, cardiac arrhythmia, unajua myocardial infarction, unajua angina, unajua CHF, unajua ion exchange katika heart muscle, unajua coronary artery na uniqueness yake, unaijua aorta wewe. Unajua heart valves

Ushawahi kusikia kitu kinaitwa biochemistry au pathophyisology.Sasa haya ni tone tu ndani ya ndoo ya elimu ya moyo. Kuna mahali umeongelea symptoms, sijui kama unajua tofauti ya symptom na sign

Ninahakika hujui kwasababu hata homa utaita ugonjwa wa homa!
Kwa taarifa hakuna ugonjwa wa homa Homa ni dalili ya ugonjwa (symptom).
Haitokei homa bila sababu. Ndiyo maana tunakushangaa na ''cardiac arrest'' .

Mkuu haya yanahitaji ukae darsa , hayahitaji kusikia na clip za mitandaoni.

Kama unasema kuna ugonjwa unaitwa cardiac arrest, basi kuna siku utatuambia kuna ugonjwa unaitwa edema, mwingine gallop rythm! mwingine mitral valve regurgitation, emboli au embolism n.k. hapo watu ni kicheko pwaaaaa!

Mkuu , wewe ongeleaa malaria na mbu mmoja kama ile post uwape watu siku.

Huku kwenye moyo kaa mbali,ninakusitiri mkuu jisetiri mwenyewe.

Yaani unarukaruka sehemu zote bila hata kuwa makini unarukia wapi bali uandike tu; hakuna aliyesema kuwa mkapa alikuwa anaumwa cardiac arrest. Elewa hilo kwanza kwa sababu unaonekana kuwa mwepesi wa kurukia mambo. cardiac arrest siyo disease bali ni condition.

Mkapa alikuwa anaumwa malaria na ndiyo iliyompeleka hospitali- kulingana na habari za kuaminika kutoka kwa mtoto wake- sasa kama wewe unadhani mtoto wake ni mwongo bali wewe ndiye unayejua zaidi hilo ni juu yako bali mimi nitaendelea kuamini familia husika. Cardiac arrrest ni shamabulio la moyo linaloweza kumkuta mtu yeyote mahala popote na katika mazingira yoyote. Michael Jackson alipata cardiac arrest baada ya kutumia madawa ya usingizi, Mother Theresa alipata Cardiac Arrest akiwa amelala, Amy Winheouse alipata Cardiac Arrest akiwa amelala, Jomo Kenyatta alipata Cardiac arrest a akiwa amelala. Imemkuta mzee Mkapa akiwa hospitali anatibiwa maralia. Hivyo ndivyo tunavyojua sasa usituletee consip[iracy theories ambapo wewe hukuwa karibu na mzee mkapa wakati anaugua.

Na kama unadhani unajua mambo ya cardiac arrest basi ni wazi huyajui vizuri kwani maandiko yako hapa hayaonyeshi kutoka kwa mtu anayejua cardiology na human anatomy sawasawa. Ingawa mimi siyo daktari wa binadamu, at least nina uelewa wa kutosha kuhusu mwili wa binadamu kuliko wewe unayejaribu kuunganisha malaria na cardiac arrest.
 
Ni hivi kaa kimya hujui lolote la anatomy ya binadamu wala physiology.
Huwezi kuzungumza nami kuhusu medicine hata dakika moja.

Tume debunk hoja ya cardiac arrest kama maradhi uliyotaka kulisha watu.
Huko kwenye malaria utajua, the bottom line ni kuwa cardiac arrest si maradhi.

Sina sababu na sitaki hata kujua nini kilitokea, lakini sitakaa kimya ukipotosha umma !

Mwalimu wewe endelea kufundisha huku kwa binadamu tuachie tunaojua

Hakuna ugonjwa wa cardiac arrest duniani huo ni wako na inatosha kufunga mjadala .

Sijui jiografia kama wewe, lakini moyo! -tafadhali mwalimu.
 
Kushindwa kuunganisha information ni failure kubwa sana kwa mtu yeyote anayedhani ni mjuaji. Unapoanza kusema ninapotosha umma ni reflection ya kushindwa kuunganisha information iliyoflow kwenye mada hii. Mimi nitaendelea kuamini habarfi zinazotoka kwenye reliable sources, siyo za kijiweni. Sikusema kuwa Mkapa kafa kwa Cardiac arrest au kwa malaria bali ni ripoti zilizoletwa na mtoto wake. Kama wewe ni daktari wake au ni mtoto wake mwingine anayejua zaidi basi ongeeni hilo kiukoo ndipo mtuletee taarifa kamili.

Sifa moja kubwa ya intellectualism ni kuwa makini na unayosema.Siwezi kukujudge kwa ulioandika hapa, Bali nakushauri uwe makini na unayoandika na uachane kabisa na conspiracy theories
 
Still connecting the relation of Malaria with Cardiac arrest sipati jibu? but kuna uhusiano mkubwa kati ya upumuaji na shambulio la moyo.

Jiongezeni wakubwa, Israel mtoa roho bado anawinda roho za watu wenye shingo ngumu.
Nikushauri ukapitie pathophysiology of Malaria vizuri and its association with malaria...coz the association is there,

Malaria is usually associated with hemolysis of red blood cells...and one of the intracellular component is potassium...if there is massive hemolysis, we expect large amount of potassium to be released ..and since the therapeutic/ normal level of potassium in the body hav a very narrow range...a small defect in potassium levels in the body...either increase( hyperkalemia) or decrease( hypokalemia) can result into cardiac arrest if not controlled
-Malaria related acidosis can cause it as well

Rejea causes of cardiac arrest 5H and 4Ts
Hypoxia , Tension pneumothrax,
Hypovolemia , Temponade( cardiac)
Hypothemia , Thrombosis(Pulm),
Hydrogen ion(acidosis) , Toxins
Hyperkalemia/ hypokalemia

I am not saying those causes related to malaria might hav caused the sudden cardiac arrest to our beloved I just tried to show you the association......
Pulmonary Embolism🤔🤔🤔??
 
Kushindwa kuunganisha information ni failure kubwa sana kwa mtu yeyote anayedhani ni mjuaji. Unapoanza kusema ninapotosha umma ni reflection ya kushindwa kuunganisha information iliyoflow kwenye mada hii. Mimi nitaendelea kuamini habarfi zinazotoka kwenye reliable sources, siyo za kijiweni. Sikusema kuwa Mkapa kafa kwa Cardiac arrest au kwa malaria bali ni ripoti zilizoletwa na mtoto wake. Kama wewe ni daktari wake au ni mtoto wake mwingine anayejua zaidi basi ongeeni hilo kiukoo ndipo mtuletee taarifa kamili.

Sifa moja kubwa ya intellectualism ni kuwa makini na unayosema.Siwezi kukujudge kwa ulioandika hapa, Bali nakushauri uwe makini na unayoandika na uachane kabisa na conspiracy theories
Mimi sina conspiracy yoyote ile. Ninajaribu sana kuangalia nani anatengeneza conspiracy

1. Taarifa ya mtoto au ukoo wake itapokelewa kama ilivyo. Pascal Mayalla kaweka sheria inayoongoza kutangaza kifo cha kiongozi na taratibu za mazishi. Serikali haikutumia sheria yake yenyewe na hilo limetoa mwanya wa conspiracy ambazo mimi siziamini lakini kwa wanaosema kuna mantiki. Sheria haikufuata hadi mwanae aseme tena akiunganisha na habari kwamba 'kumekuwa na habari za mitandaoni''.

Haikupaswa kabisa kuwe na shaka ikiwa serikali ingefuata sheria zake. Swali kwanini serikali imesita kutoa taarifa

2. Taarifa ya William bado haielezi Rais wetu alipatwa wapi na mauti. Serikali haikueleza, na hakuna katika wale walioongea naye anayesema. Watu wamebaki kujiuliza hospitali ipi? Hapa wenye theory ndipo wanapopata miguu

3. Taarifa ya kwamba amefariki kwa ugonjwa wa cardiac arrest ina utata na usumbufu mkubwa hasa kwa wanaojua,

Haya yote ukiyaangalia kwa jicho pevu na upana wa akili utaona kuna kitu ima hakikuwa sawa wakati wa kutangaza, au kipo sawa bali kuna jingine. Na kwa bahati mbaya hakuna anayejitokeza alau kufukia mashimo

Narudia sina theory au conspiracy yoyote, lakini nitasema wazi kwamba kuna something wrong, iwe katika communication au vyovyote, kuna kitu hakipo sawa .

Rais Kikwete alijua ni public figure na kwamba Taifa lina interest kwake. Alijitokeza na kusema anaumwa Tezi dume.
Si kwamba aliondoa uvumi bali pia alisaidia sana kuondoa stigma ya tatizo la prostate.
Kusema tezi dume siku hizi ni kawaida tu, lakini, ilichukua courage ya mtu mmoja na hilo lilikuwa sahihi
 
Shambulio la moyo mara nyingi mtu huwa yupo kwenye coma na anakuwa chini ya uangalizi wa madaktari muda wa kuzungumza zaidi ya saa zima anatoa wapi...

Naona awamu hii shambulio la moyo ndio kimbilio..
Asee kama udaktari sio taaluma yako ni bora ukagather information ya kutosha kabla hujatoa hoja.Kwa kukusaidia tu nenda kagoogle sudden causes of cardiac arrest uone kama if it is necessarily for someone to be in coma ndio appate arrest.Tuachieni taaluma yetu.
 
Back
Top Bottom