Kumbe ndio maana hamuolewi!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe ndio maana hamuolewi!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Nov 9, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Siku hizi wanaume hupata mapenzi kirahisi sana kutoka kwa wanawake kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Hata ukiongea na mzee mwenzangu Bishanga atakubaliana na mimi.

  Zamani enzi zetu makahaba walikuwa ni wachache sana na ilikuwa ni aibu sana kwa mwanaume kwenda kwa kahaba. Ni wale tu waliokata tamaa ndio ambao walikuwa wanakwenda kwa makahaba.

  Enzi zetu sisi, mipaka na kanuni za jamii katika kushiriki mapenzi kabla ya ndoa zilikuwa ngumu sana. Mwanaume analazimika kuoa haraka kwa sababu kupata ridhiko nje ya ndoa ilikuwa ni shughuli pevu, na ndio maana wastani wa umri wa kuoa wakati huo ilikuwa ni kati ya miaka 23 mpaka 25, tofauti na siku hizi umri wa kijana kuoa umefikia miaka 30 mpaka 35. Mpaka hapo unaweza kuona ni kwa namna gani wanaume wanachelewa kuoa.

  Leo hii inaonekana kama vile kila msichana ni kahaba. Hata wale watoto wanaoitwa, ‘watoto wa geti kali,’ wanapatia mimba humo humo ndani ya mageti, sema tu kwamba, wengi huzichoropoa kiurahisi. Kufanya mapenzi ya utotoni hivi sasa ni kama sifa. Wataalamu wanasema kwamba, watoto wa kike wanaotoka kwenye familia zenye vurugu na tafrani hushiriki mapema tendo la ndoa.

  Hebu tujiulize, je ni familia ngapi zina amani? Kwa hiyo watoto wa kike wengi huanza mapenzi utotoni na hivyo, vijana hupata ‘asusa’ kwa kadiri wapendavyo, ni rahisi sana. Na ndio maana wanachelewa kuoa kwa sababu kile ambacho (kujamiiana) wanaamini ndio sababu ya wao kuoa wanakipata kwa urahisi.
   
 2. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,057
  Likes Received: 3,085
  Trophy Points: 280
  Watafiti wanadai wanawake ni mara3 ya wanaume kwa sasa duniani sasa labda waweza kuwa wanahofia wingi wao wenyewe dhidi ya kumiliki mwanaume...wanacheza,sandakalawe,amina..atakayewahi atapata,naasume tu.
   
 3. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  mhhhhhhhhh! kwa kuwa ni wewe umeongea utaona wenyewe wako kimyaaaaaaaaa, ngoja aongee bujibuji uone mashambulizi yao, utadhani wameambiwa kwamba umewachungulia wakati wa kuoga, loh!
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo unataka kuniambia kwamba enzi zetu uwiano ulikuwa wanaume ni mara 3 ya wanawake ndio sababu walikuwa ni adimu?
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  @Ndyoko...... unakosea bana, kwani mimi ni nani mpaka nisikosolewe?
   
 6. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kweli maadili yameporomoka ila mawazo yako sio kweli 100%. Hapo unaposema "ni kama kila msichana ni kahaba" unamaanisha nini?
  Mbona hata zamani watu walikua wanajua kuna kuolewa na bikra kama vile kuna kuolewa bila bikra? sasa hao wenye kuolewa bila bikra walikua wanabikiriwa vipi?
  Huoni kama huo utaratibu wa kuoa ili upate sex ni very diminishing kwa mwanamke? yaani unamtumia kama kifaa cha kupata regular sex kiurahisi kuliko kumtreat kama binadam mwenzio ambae anamahitaji mengi zaidi ya sex? no wonder wanaume wengine wanasema mke wake akikataa 'kutoa' anahakikisha 'anajichukulia bila kupewa,' hata kwa kumkata makofi!
  Anyway...
  Mchango wangu ni kwamba kama sababu za kuoa zamani zilikua kupata free and regular sex, sababu za kuoa leo ni tofauti kabisa na zinategemea Mvulana PAMOJA na msichana wanao husiana katika mapenzi. Sio sex tu (coz as you point out ni rahisi kupata sex hata bila ndoa).
   
 7. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #7
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Half truth!!!
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  RussianRoulette... neno, 'ni kama' means, 'is like' au niseme, 'inavyoonekana siku hizi kila msichana ni kma kahaba' kwa nini? ni kwa sababu swala la wao kugawa mapenzi limekuwa ni huria mno, tofauti na zamani.
  Kuhusu dhana ya kuoa, zamani pamoja na sababu nyingine za kuongeza uzao katika familia, lakini kujamiiana nako ilikwa ni sababu ya vijan kuoa mapema, zamani ukifikia umri wa ubarubaru (balehe) ambapo damu inachemka haikuwa ni jambo rahisi kumpata mwanamke, ilikuwa ni ngumu kweli, na ndio maana hata umri wa kuoa ulikuwa ni mdogo........ na ndio mana kwa waislamu wanaamini kwamba mtu mwanaume akishabalehe au mtu mwanamke akishavunja ungo ruksa kuoa au kuolewa, umri hautajwi.......... kwa sababu wanajua sarakasi za vijana wakishapevuka.
   
 9. AMINATA 9

  AMINATA 9 JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 2,132
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  watafiti wengine wanakula tu hela ya serikali loh! asa ndio umatafiti nn hapo mweh!
   
 10. Nemo

  Nemo JF-Expert Member

  #10
  Nov 10, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 662
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 80
  Mtambuzi
  We nawe sijui what u have against us! Mara tunacheatiwa kwa kuwa hatuwahudumii, mara hatuoelewi kwa kuwa kahaba.............kha!!

  Anyways here is my take:
  Unlike old days where women lived to be married, now days things are different. We go to school, and dare to dream and/or comprehend life other than being some silly man's missus!
   
 11. S

  Song'ito JF-Expert Member

  #11
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  naunga mkono hoja ndugu mtambuzi,

  lingine kama ziada huu ustaarabu wa kimagharibi umetuharibu sana tena sana...ni ustaarabu unaowafundisha watoto mambo ambayo ilikuwa haiwezekani kujifunza enziza mwalimu....ndugu mtambuzi kwa ajili ya utandawazi siku hizi utamkuta binti anapika na kupakua nyumbani kwa mwanaume, akikaa huko hata miezi huku akiwa hajaolewa..huku kwa wazazi akidanganya yuko kikazi au kimasomo mahali fulani...sasa kama kijana anapata huduma zote hizo ya nini kuharakia kuoa? si ni sawa na mtu aliye na mke tu? hii ni moja ya sababu kwa nini vijana hawaoi....

  wasichana wa siku hizi wanaona kuwatendea hivo wanaume ni kuwaonyesha mapenzi motomoto lakini wakati huo hawajui kuwa wanaondoa mshahawa wa vijana hawa kuwaoa mapema maana huduma inapatikana bila kuoa na tena inaweza kuwa nzuri kuliko ile anayopewa mtu aliyeoa.

  Kingine mtambuzi haya mambo yakuigwa nlotaja hapo juu yamepelekea vijana kuwa na mapenzi ya ki.com mi nayaita.... siku hizi udanganyifu ni mwingi mnooo na jamii kama inaanza kuzoea... siku hizi utakuta mtu kafumaniwa asubuhi jioni watu wanamsifu kuwa ye kiboko, au mathalani unakuta mvulana au msichana na wapenzi zaidi ya mmoja kwa pamoja..wakati enzi za mwalimu hata kusimama kavulana kamoja tu kwa mabinti ilikuwa kwa kuibia..kutokana na hilo vijan wengi wanahofia kuoa maana unaweza kuoa jambazi la mapenzi au kuolewa na jangili la mapenzi ukaishia kupata dissapointments tu....mifano mizuri mtambuzi chunguza mwenendo wa ndoa za vijana mtaani kwako tu hapo utaona mambo yalivo shaghala baghala...

  nawasilisha
   
 12. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #12
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Mtambuzi give us a Break walau a month.... We deserve it and bring something on the men! Maana kwa kweli umeegemea upande mmoja...
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  pole shem wangu ashad.... Naona kimeumana
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Nov 10, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  It's unconscionable to say the least..
   
 15. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #15
  Nov 10, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,420
  Likes Received: 3,768
  Trophy Points: 280
  Zamani ilikuwa hivi... Baba wa mvulana anamwona msichana, anampa taarifa mvulana na vile vile anatafuta mshenga wa kwenda kwa msichana... IKAFUATA... Mvulana anamwona msichana anampenda na kabla hajamweleza anakwenda kwa baba yake, baba anamtafuta mshenga na taratibu zingine zinafuata... IKAFUATA... Mvulana anamtongoza msichana, wanakubaliana halafu kila mmoja anaenda kusema kwao. Wazazi wa msichana watapewa taarifa na msichana tarehe ya mshenga kuja rasmi... IKAFUATA.... Wanatögozana, wanapeana mimba halafu wanafunga ndoa. Na ndiyo mbna siku ndoa za wenye mimba ni nyingi.... MALIZIA Kinachoendelea
   
 16. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #16
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ahsante Da AshaDii kwa angalizo, ushauri wako nimeupokea tena kwa mikono miwili..........................
   
 17. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #17
  Nov 10, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Shikamoo baba,nakusalimu katika jina la bwana yesu kristo!
   
 18. O

  Old Moshi Senior Member

  #18
  Nov 10, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mi nadhani sababu kubwa ya kuchelewa kuoa au kuolewa ni; matatizo mengi yanayoongelewa ktk ndoa. Wanandoa wengi pamoja na wazazi wamekua wakiwaambia vijana na watoto wao kuwa ndoa ni ngumu na ina shida na matatizo mengi. Hii imepelekea vijana wengi kuchelewa kuoa au kuolewa wakidai hawataki kuingia ktk shida mapema. Huo ndo mtazamo wangu.
   
 19. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #19
  Nov 10, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  hujambo Asha?
  Wala usikonde,naandaa uzi ...title...'Mianaume ndivyo tulivyo'...stay tuned!
   
 20. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #20
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kuna msemo wao wanapenda kuutumia siku hizi: "Virginity is not a matter of dignity but lack of opportunity"
   
Loading...