Kumbe Mzee Makumbi amefariki dunia! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe Mzee Makumbi amefariki dunia!

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Kwetunikwetu, Mar 7, 2009.

 1. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Leo jioni nilipitia pale tawi la Yanga buguruni adjacent na shule ya msingi Buguruni kumsalimi mzee mmoja anaitwa Makumbi. Nikawakuta jamaa wawili wamekaa kwenye benchi wanapiga story. Nikawasalimu, then nikawauliza;

  "Jamani samahani nilikuwa namuulizia mzee Makumbi sijui naweza kumpata wapi"
  Wale jamaa wakabaki wameduwaa, nikaona labda hawajanielewa, nikabadilisha swali;

  "Jamani Mzee Makumbi mmemuona jioni hii, nilikuwa nataka kumsalimu"

  Duh, jamaa mojawapo akaniuliza;
  "Kwani mara ya mwisho umemuona Makumbi lini"

  Nikamjibu "Ni muda mrefu sana inawezekana mwaka mmoja na zaidi umepita"

  Basi jamaa akajibu "Basi kipindi hicho hicho ndio huyu mzee amefariki, ilikuwa mwaka jana mwezi wa pili"

  Kwa kweli nilihisi baridi ghafla! Mungu amlaze mahali pema peponi, amini!
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Makumbi Juma yule homa ya Jiji?
   
 3. 3

  3 kids Member

  #3
  Mar 7, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tupe jibu basi Makumbi gani ni huyo???????
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Mar 7, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Mambo haya hutokea. Yalikuta mara mbili:

  (a) Nilikuwa na rafiki yangu wa karibu sana, ambaye kama mimi alikuwa pia mvivu sana wa kuandika barua. Kuna wakati nilikuwa nje ya nchi kwa mwaka mmja, niliporudi Dar, nikasema ngoja nikamwoen mshikaji wangu tuingine kwenye moja moto moja baridi. Nilipofika nyumbani kwake na kuulizia nikakutana na swali kama uliloulizwa.

  (b) Nilikuwa na mpenzi wangu poa sana mwishoni mwa miaka ya themanini. Nikatokea kuwa nje ya nchi kwa miezi sita tu, ila wakati nikiwa kule nilikuwa namtumia kadi ambazo zilikuwa hazijibiwi. Niliporudi Dar, nikakimbia haraka sana kwenda kumwona mwandani wangu huyo, nikakutana na swali kama hilo hilo uliloulizwa.


  Hiyo ni sehemu ya maisha.
   
 5. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Sio yule mchezaji, bali ni shabiki mmoja mashuhuri sana wa Yanga pale buguruni. Alikuwa mcheshi sana na mtu wa sound kweli kweli. Alikuwa al-watan fulani, mambo ya mjini-mjini alikuwa makini kuukuunganishia mishemishe
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,878
  Likes Received: 83,353
  Trophy Points: 280
  Kichuguu, hiyo pia mimi imeshawahi kunitokea. Kuna jamaa zangu niliokuwa nafanya kazi nao ambao tuliishi vizuri. Basi niliporudi bongo miaka ya karibuni nikaamua kuwachukulia vijizawadi vidogo vidogo. Nikapita pale ofisi kuwajulia hali. Nilikuwa nafahamiana na watu wengi sana pale ofisini lakini hawa tulikuwa tuko kaibu mno. Basi katika kusalimia mwishi nikaingia ofisi ya mmoja wa waliokuwa karibu na hao jamaa zangu. Nikauliza dada fulani na fulani wanakaa ofisi zipi? Akanijibu hao wameshafariki kwani hukusikia? Nikapata mshtuko ambao sikutegemea maana nilikuwa sijasikia vifo vyao. Miaka hiyo mawasiliano na Bongo yalikuwa ni shida kubwa sana siyo kama ilivyo sasa baada ya utandawazi na simu za mkono kurahisisha sana mawasiliano. Nikaambiwa watu wengi wamefariki nikaanza kutajiwa majina basi nikabaki nimepigwa na mshangao na kuwa na mshtuko wa hali ya juu. Madada wawili walikuwa wamefariki na njemba 6 kati ya wanane niliokuwa nimewachukulia vijizawadi nao walikuwa wamefariki. Kilichonisikisha zaidi wengi wao walikuwa bado wana maisha marefu mbele yao. Basi nikaishia kugawa zawadi zangu kwa watu ambao hawakuwemo kwenye list yangu.
   
 7. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2009
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180

  Unayemsema hapo ni KIZOTA!
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu usije kuwa unachanganya na Said Mwamba Kizota!
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,878
  Likes Received: 83,353
  Trophy Points: 280
  Aliyegongwa na gari na kufariki ni Said Kizota naye alikuwa ni mchezaji wa Yanga.
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Siku hizi nikirudi kijijini nasita kuulizia watu niliokuwa nawafahamu zamani. Nisipomwona mtu au kupata salamu zake huwa nakaa kimya.
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Jasusi inaelekea huulizii kabisa mademu zako wa kale...hutaki pressure! looooooh
   
 12. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  duh! naona nimeua mtu.
  naomba tena radhi kwa niliowakwaza.
   
 13. Chibidu

  Chibidu JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 387
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Du! Mzee isijekuwa unataka kumtoa kafara!!Ingekuwa busara zaidi ukaminya tu imya kinywa kama huna uhakika.maana kama bado yupo unaweza zua kilio kwa jamaa zake wa mbali ambao hawajamuona siku nyingi
   
 14. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,525
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
   
 15. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mwenzenu ilinitokea mwaka jana (2008). Nilikuwa nimepanga kwenda kumuona baba mdogo ambaye tulikuwa hatujaonana miaka mingi. Ila kwa kuwa nilikuwa na muda kidogo na sehemu hiyo wanayoishi pia usafiri wa shida hasa masika basi niliomba tukutane naye mji mkubwa wa karibu. Binamu yangu alinijibu .."haiwezekani, baba mdogo amefariki tangu mwaka 2006".

  Nilimpigia simu mtoto wake na ndugu wote kuwauliza imekuwaje ni mimi tu sijapata taarifa za msiba wa baba? Kila aliyepata simu alipata kigugumizi na kusema "wala sijui imetokea vipi..."
   
 16. Gottee

  Gottee Senior Member

  #16
  Mar 9, 2009
  Joined: Sep 7, 2008
  Messages: 174
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Makumbi Juma au Mzee Bonga yuko Sengerema Mwanza akifundisha mpira kule!!
   
 17. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #17
  Mar 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mkuu Sikonge, uwezekano mkubwa mpaka usisikie kifo cha Baba yako mdogo ulikuwa nje ya nchi. Manake kweli miaka karibia miwili usiwe na mawasiliano na Baba yako mdogo. Pole lakini mkuu. Hii habari ya Mzee Makumbi nilipoiona mwanzo nikajua ni Makumbi Juma.
   
 18. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #18
  Mar 9, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...kwa hali hii ya "huna habari alishafariki mwaka uleee...!" kuna haja hapa Jamvini ifanyike Roll-Call,

  isijekuwa wenzetu tayari wamesha Rest in Peace! ilhali sie twadhani wameuchuna tu!
   
 19. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #19
  Mar 9, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  naona umelishikia bango hili kosa pamoja na kumba radhi kwangu.
  ngoja basi nifute kabisa maneno yangu isje ikawa issue bure.
   
 20. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #20
  Mar 10, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ushukuru ulikuwa nje huenda hayo mavuno yangekupitia. Pole sana kwa kuwapoteza swahiba zako. Endelea kula maisha.
   
Loading...