Kumbe Mechi ya Yanga SC na Namungo FC imelazimishwa ili Kocha Nabi atumikie Red Card yake na Mechi ya Derby awepo Benchini?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
TFF tambueni kuwa wakati nyie mkijifanya kuwa mna Akili tambueni kuwa kuna Watanzania wenye Akili kuwazidi halafu ni Wajanja kuliko nyie.

Kwahiyo Matajiri wa Yanga SC wamewashawishi kwa kila namna huku wakiwapa chochote kitu ili muwapangie Mechi kabla ya kukutana na Simba SC ili Kocha wao Mkuu Nabi atumikie Red Card yake na katika Mechi ya Kariakoo Derby awepo Benchini?

Kwa ninavyowajua Yanga SC kama Kocha wao Nabi asingekuwa na hii Red Card hii Ratiba ya kucheza na Namungo FC wangeikataa na msingewafanya lolote ila na Wao wameifurahia kwakuwa wanajua itamsaidia Kocha wao Mkuu Nabi kuitumikia halafu katika Kariakoo Derby atakuwepo Kuwaongoza Wachezaji wake.

Kweli kwa Msimu huu Yanga SC imejipanga Kimkakati kote kote tu Hongereni na sasa haina mjadala Yanga SC iwe isiwe ndiyo Bingwa wa NBC Premier League.
 
Mkuu nimeandika nikiwa nimefumba macho .
Huyu jamaa sipati picha angekuwa na jinsia ya kike ni namna gani angekuwa mgombanishaji wa ndoa za watu.

Yaani anajifanya kujua ya ndani kumbe ni sifuri kichwani. Sheria ipo wazi kuwa ukipewa red card utatumikia adhabu mechi tatu.

Sasa huyu sheria ya mechi moja kaitolea wapi? Yaani hata sheria za mpira hazijui halafu anajifanya mjuaji
 
Back
Top Bottom