Kumbe mabinti ndivyo mlivyo?

Kumbe mabinti ndivyo mlivyo?

Za mida wajumbe?. Kuna friend of mine hapa ananipa mchapo akitaka kujua afanye nini.
Ana binti aliyenaye katika mahusiano kwa miaka kadhaa sasa. Kijana anasoma ila ana gratuate this year. Binti kamkaba jamaa wafunge ndoa jamaa naye kaona ni sawa kwani kaona binti amepass viwango kuwa naye kimaisha ila jamaa anakwama sehemu moja ana ajira somewhere ya mkataba na analipwa 80% ya mshahara kwa mwezi kwa sababu kiwango chake cha elimu hakijafikia lengo la mshahara kamili. Kwa hili binti akamtia moyo kuwa asijali kabisaaa kwani kwao mahari anataja binti na akamhakikishia kuwa haitazidi laki tano ama sita jamaa kwa kuona hivyo na kwa kuzingatia umri wa ampendaye unamtupa mkono akajitosa binti akawakusanya ndugu zake wengi kuwapa taarifa kuwa amepata mchumba in short jamaa anamuuliza binti ampe siri ndg wanataka kiasi gani ili awaelezee washenga watakapo kwenda wajue kiasi binti anamwambia jamaa ajiandaye kwa milioni moja na nusu khe jamaa kasara mbaya ukitegemea ni miezi kama mitano tu imebaki kwao kufunga ndoa. Binti ni form four failure ila anakibarua mkoa mwingine mbali jamaa mawasiliano ni Simu tu. Jamaa akaa kimnya akajikunja kwani wazazi wa binti waligomea hapo hawataki chini ya hapo.
Jamaa amekubali. Sasa wameenda kwenye swara la Pete ya engagement binti anataka ya dhahabu si chini ya gramu mbili jamaa anamsihi amsaidie japo kidogo binti anagoma kwa kusema nini maana ya kuwa engaged?. Anamwambia wanunue Pete ya silver anamwambia ataiweka kwenye kidole cha nani?. Sasa hivi wamebakiza siku chache jamaa akatoe hiyo mahari anamwambia binti amsaidie pesa kidogo za kununulia vitu vya kuwapa wazazi wake kama blanket na kanga binti anawaka ile mbaya kuwa hata kuwa na amani kabisa akiwa ndani ya ndoa akifanya hivyo. Jamaa hana hamu naye ananiomba ushauri hapa kwani kaamkia kwangu asubuhi hii akitaka kuniuzia boda boda yake ama niichikue bond. Ushauri tafadhari Wajumbe. Mnisamehe kwa uandishi sio mzuri.

Huyo jamaa, hata kama atamchukua huyo binti waishi kwa pamoja, hiyo ndoa itakuwa ndoano na mwisho wa siku haitadumu.
 
  • Thanks
Reactions: J C
TOka NduKi KimbiaAaaaaaaaaaaaaa....Atakufa Maskini unaowa ama Unanunuaaa
 
  • Thanks
Reactions: J C
Ndio, huyo demu anafanya kazi IMTU au?

Nadhani itakuwa hivyo mjumbe. Anataka sifa wakati akijua mwenzie anachukua risk ya kuoa bila ya kuwa na kazi ya uhakika . Hilo halioni kwa sasa anachoona ni ndoa tu. Mxiiii.
 
Huyo mwanamke ni wa kumpa chaguo, kama akitaka kuolewa aongee vizuri na ndugu zake na wapunguze hayo mahitaji. Halafu mshkaji kama anaweza kumpumzisha ampumzishe tu maana huyo dada ana tamaa na hana nia ya dhati ya kuolewa na jamaa, rather than kujionesha kwa ndugu zake
 
  • Thanks
Reactions: J C
Nikuulize wewe JC,huyo msichana angekuwa wako ungemuowa??

Aaa wapi nisingefanya hivyo ila mapito ya mtu huwezi yasemea kwani kila mtu anayo yanayomtosha mwenyewe.
 
Asipeleke mahari wala nn atulie tu kwan wanamuonea na ndoa hazko hivo lazma kuwe na maelewano.Atulie kwa muda usiopungua miezi miwl watajfunza tu na km akiona hawajifunzi aahrishe kabisa

Shukrani mjumbe
 
Asubuhi ya leo imeharibika,apige chini ajipange !harusi atataka ikafungiwe kwe ndege! Aaachane nae akimbie kabisa!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
  • Thanks
Reactions: J C
Kwani binti si ndo anataka ndoa, amwambie ameshindwa na ndoa bas amwone binti atakavokubali kuvaa hata pete ya majani na kujilipia mahari...
 
Sifa kuu moja wapo ya mwanaume ni kujiamni na kusimamia maamuzi yake.Kufanyiwa maamuzi na kuwa mtekelezaji,sio ukamilifu wa mwanaume.Akiisha oa mke na mke akimnyima unyumba kwa kisingizio cha kutoruhusiwa na mama yake.Atakimbia tena kuomba ushauri Hapa sio!!?
 
  • Thanks
Reactions: J C
Huyo msichana kaonesha tabia yake mapema sana na huyo kaka amshukuru Mungu kwa hilo.
Aachane naye haraka sana atakuja kumsumbua sana. Msichana ni aina ile ya wanawake wakiona
jirani kanunua vitz anakushinikiza ununue hummer au unyimwe unyumba.

Achana na hii kisirani!

Halafu hii thread mahali pake hasa ni MMU Invisible! Hebu fanya mpango wa hii kitu.
 
Last edited by a moderator:
mwambie aachane nae tu ful stop. Huyo hawez kuwa hata mke na wakioana hawawez kukaa hata mwaka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom