Kumbe kubandika stika ya BIMA kwenye kioo cha gari ni lazima, hata kama umekata BIMA yako mtandaoni

Mkuu, kivipi. Siku hizi ukienda kukata Bima haupewi kile cha kubandika ila unapewa tu katarasi kubwa ya A4 inayoonesha umelipia Bima. Sasa utabandikaje?
sheria ya usalama barabarani inataka ubandike tena kioo cha mbele kushoto ha haaaa tusome sheria japo tunapokuwa tumeama vizuri la sivyo tutapigwa sanaaa
 
Manjagu wao hukomaa na Stika, mimi kuna kipindi nimeshawahi kuweka Stika feki wakati sina hata Bima Manjagu wakaingia kingi miezi sita mpaka nilipopata mlungula ndio nikanunua Bima Orijino.
Hahahahah uliwachezea shere *****
 
Umepigwa mkuu... Mimi sio kipindi hiki tu hata kabla utaratibu haujabadilika sijawahi kubandika hiyo stickee kwenye kioo... Akitaka huwa namtolea huwa natembea nayo ndani ya gari
busara ndo inatumika ila sheria haijasemea mtu atembee na karatasi la bima ndani ya gari ila libandikwe kioo cha mbele tena kushoto, japo busara huwa inashinda sheria
 
Tatizo ni kubandika stika ya BIMA kwenye kioo, NI sheria kabisa na yeye alinionyesha inakutaka kubandika stika.
yani ni ka ile sheria isemayo ukikaa na mwanamke zaidi ya miaka miwili hiyo ni ndoa inayotambulika kisheria ha haaa, yani issue hapo kwa bwana mkubwa ni kubandika tuu sasa sheria ya mbunge wake haijafanyiwa marekebisho alafu unategemea nini ukikutana na askari? yani busara tuu ndo inaokoa
 
Wana JF

Leo nlisimamishwa na traffic, akakagua kioo na kukuta sina stika ya BIMA, alivyoniuliza nikamwambia BIMA nshakataa mtandaoni, na kwenye system ya TIRA MIMS inaonyesha gari tayari nina BIMA.

Ila kilichonishangaza zaidi ni kuwa huyu jamaa aliniandikia faini, kosa langu ni KUTOKUBANDIKA STIKA YA BIMA kwa kioo cha gari. Kwa kweli hili limenishangza sana kwamba sasa tuna uwezo wa kukata bima kwa simu, na kupata bima yako instantly .! Ila sheria za traffic bado zinatubana kwamba ni lazima ubandike stika ya bima kwenye kioo. !

Sijajua ni nani mwenye jukumu la kubadilisha hii sheria ila ni moja ya sheria ya kijinga sana kuendelea kuwepo, maana kunakua hakuna maana ya vifaa vya traffic kuunganishwa moja kwa moja na mfumo wa TIRA kama bado sheria inataka nibandike stika

Waziri husika tunaomba uliangalie hili.
hakuna hyo sheria kwamba ni lazima ubandike bro! ametumia maamuzi yake ya kila siku ..:eek:
 
Walikuwa hawaulizi Cover note wakinipiga mkono nilikuwa siwavuki ili akija anakagua Kioo anaiona Stika halafu ananiuliza kama nina maji ya kunywa nampa Buku natia gia 😁😁
Maaskar weng njaa njaa hawaijui cover note kuwa ndio bima yenyewe
 
Sasa makampuni yamebadili utaratibu kwann yeye alazimishe kutumia kanuni za zamani za kubandika stika na stika hazipo....

Ungemuuliza wakuu wako wa kazi hawajakwambia kuhusu utaratibu mpya au umeamua kuwa tapeli kwa kutumia vazi la uaskari....??!
sheria huwa ni nzuri sana ukiielewa ila sheria usipoifahamu utakuwa kitoweo kwa wasimamizi wa sheria japo sheria zinamlinda zaidi mkosaji
 
Wana JF

Leo nlisimamishwa na traffic, akakagua kioo na kukuta sina stika ya BIMA, alivyoniuliza nikamwambia BIMA nshakataa mtandaoni, na kwenye system ya TIRA MIMS inaonyesha gari tayari nina BIMA.

Ila kilichonishangaza zaidi ni kuwa huyu jamaa aliniandikia faini, kosa langu ni KUTOKUBANDIKA STIKA YA BIMA kwa kioo cha gari. Kwa kweli hili limenishangza sana kwamba sasa tuna uwezo wa kukata bima kwa simu, na kupata bima yako instantly .! Ila sheria za traffic bado zinatubana kwamba ni lazima ubandike stika ya bima kwenye kioo. !

Sijajua ni nani mwenye jukumu la kubadilisha hii sheria ila ni moja ya sheria ya kijinga sana kuendelea kuwepo, maana kunakua hakuna maana ya vifaa vya traffic kuunganishwa moja kwa moja na mfumo wa TIRA kama bado sheria inataka nibandike stika

Waziri husika tunaomba uliangalie hili.
mkuu huyo alikuwa anatengeneza mazingira ya kukupiga kwa kuamini kuwa hujui kinachoendelea. sasa hivi hata mawakala walishaambiwa warejeshe vitabu vya stika walivyokuwa wanatumia kukata stika kwa sababu havitumiki tena
kama alikupiga faini usikubali
 
Maaskar weng njaa njaa hawaijui cover note kuwa ndio bima yenyewe
Nilikuwa najua kabisa kuwa ninavunja Sheria, ila nilikuwa nauguza Mzazi na hali ilikuwa mbaya sana ila nilipozishika tu nikanunua Bima orijino nilimuomba sana Mungu nisipate ajali haswa kipindi hicho cha Bima feki.
 
Sheria haibadiliki automatic mkuu. Sheria inafanyiwa mabadiliko
So hapa walitumia sheria halali kabisa kunipiga fine.
mkuu umenena vyema inawezekana kuna baadhi ya marekebisho ya kanuni ila sheria bado imesimama ka miaka yote, kwahiyo ameadhibiwa kulingana na sheria iliyopo, japo busara ingetumika aneweza kuwa salama
 
Nilikuwa najua kabisa kuwa ninavunja Sheria, ila nilikuwa nauguza Mzazi na hali ilikuwa mbaya sana ila nilipozishika tu nikanunua Bima orijino nilimuomba sana Mungu nisipate ajali haswa kipindi hicho cha Bima feki.
Yah Mungu alisaidia maana msala wake ungekuwa sio wa kitoto
 
Nilikuwa najua kabisa kuwa ninavunja Sheria, ila nilikuwa nauguza Mzazi na hali ilikuwa mbaya sana ila nilipozishika tu nikanunua Bima orijino nilimuomba sana Mungu nisipate ajali haswa kipindi hicho cha Bima feki.
alafu mama anasema watu wapewe elimu ilihali watu tunajua sheria
 
Sheria haibadiliki automatic mkuu. Sheria inafanyiwa mabadiliko
So hapa walitumia sheria halali kabisa kunipiga fine.
Ina maana wewe hukuona tangazo la TIRA kuhusu kusitishwa utoaji wa stika za bima? Au unataka kutetea Uzenge wa uyo askari?
 
Mkuu upo sahihi,lakini tatizo ni kuwa wengine hawana muda huo,wanaletewa leseni nyumbani. Suluhisho rahisi ni kutoa elimu hii ya usalama barabarani nnje ya mfumo rasmi wa vyuo vya udereva.
mkuu kama itahitajika watu wapewe elimu basi, kilamtu apewe leseni yake alafu hao wasimamizi wa sheria ndo waanze kutoa elimu, .mtizamo wangu ni kila mtu kwa wakati wake hata ka kapewa leseni akiwa amelala basi aone umuhimu kujifunza alama na baadhi ya sheria za barabarani la sivyo ndo tutakuwa wafuu ama walemavu kisa watu wachache ambao ni wavivu kuhangaisha bongo zao kufahamu sheria na taratibu za barabarani
 
Ina maana wewe hukuona tangazo la TIRA kuhusu kusitishwa utoaji wa stika za bima? Au unataka kutetea Uzenge wa uyo askari?
mkuu maswala ya kisheria na kimfumo yanatakiwa kuandaliwa vyema maana kama unasema wamesema wamesitisha ni vizuri, ila je sheria imefanyiwa marekebisho? je vyombo vingine vya usimamizi wa sheria vimejiandaa kivifaa kwajili ya kuangalia kama mtu anabima ama laaa? yani vyombo vyote lazima vishirikiane na lazima kuwe na mapendekezo ya ubadilishwaji wa sheria. aliyehukumu anauhalali kulingana na sheria alotumia sema inauma maana mtu anabima tayari
 
Back
Top Bottom