Makanyaga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2007
- 10,327
- 6,850
Ni kwamba nimesoma LAW OF INSURANCE, na wale waliosoma sheria kama kuna sehemu sitaenda sawa, watanirekebisha katika hili.
Mimi siyo mwanachama wa mfuko huu, na kilichonisababisha nisijiunge ni namna makato ya mfuko huu jinsi yanavyofanyika.
Kwanza kabla sijaenda mbali sana, kawaida makato ya Bima huwa yana-base kwenye risk au kitu ambacho tahadhari yake inakufanya ukikatie Bima. Kwa mfano Bima tuseme ya maisha ya mtu ambaye huwa anavuta sigara, malipo yake kwa mwaka (premiums), ni kubwa kuliko mtu ambaye havuti sigara kwa sababu anayevuta sigara risk yake ya kupoteza maisha ni kubwa kuliko ya yule ambaye havuti sigara.
Kwa hiyo hawa watu wawili wakienda kwenye kampuni moja siku moja na kukata Bima za maisha za muda unaofanana tuseme wa miaka mitano (5), anayevuta sigara premuium yake itakuwa kubwa kuliko ya yule ambaye havuti sigara.
Kutokana na hali hiyo basi, PREMIUM au malipo anayotakiwa mwanachama kulipia kwa mwaka, huwa yako based on the RISK INSURED na si vinginevyo!
Kwa ufupi sana mapaka hapa sasa, naomba sasa nieleze mimi kwa nini nilishindwa kujiunga na BIMA YA AFYA YA NHIF, labda mpaka pale itakapokuwa ni mandotory:
Nilipotaka kujiunga nilielezwa kuwa nitakuwa nakatwa asilimia tatu (3%) ya mshahara wangu KWA MWEZI na mwajiri naye, yaani Serikali naye atanichangia asilimia 3 KWA MWEZI vilelile.
Kwenye kipengele hiki tu peke yake, unaweza kuona kasoro za wazi kabisa kama ifuatavyo.
MOSI: Kwa namna sheria za Bima zilivyo, kipengele hiki hakiko sahihi, na kingekuwa sahihi tu kama kile ninachokatia BIMA, ungekuwa ni mshahara.
PILI: Remiums ambazo watu wanatakiwa wachangie kwa ajili ya BIMA ya Afya ya NHIF, zinatakiwa kuwa sawa kwa watu wote, yaani inatakiwa kuwa flat rate kwa sababu risk ya wafanyakazi tuseme wa Banadri kuugua, ni sawa kwa wote, ukiondoa cases chache sana za watu abao huwa wanaugua mara kwa mara, lakini kwa wafanyakazi ambao huwa wanahudhuria ofisini siku zote na hawana matatizo peculiar ya kiafya, risk yao ya kuugua iko sawa na hivyo Premiums zao katika kulipia Bima ya Afya zinatakiwa zilingane bila kutofautiana hata senti moja.
TATU: Kulingana na sheria za Bima jinsi zilivyo, Serikali hailazimiki kulipia premiums za wafanyakazi wake wanaojiunga katika mfuko huu, kanma ilivyo kwenye mifuko mingine ya hifadhi kama PPF, NSSF, n.k. Huu mfuko una tofauti kubwa mno na mifuko hiyo na hivyo Serikali inaweza kuchangia iwapo tu ni yenyewe imeridhia kufanya hivyo. SERIKALI KUENDELEA KUCHANGIA KWENYE MFUKO HUU PIA, NI KUIPA MZIGO WA ZIADA AMBAO HAIKUSTAHILI KUUBEBA. Bima ya mfanyakazi wa Serikali haina uhusiano wowote na mwajiri wake na hivyo haina uhusiano na hela za Serikali. Kwa mfano mimi ninapokata Bima yangu ya Afya, ni sawa tu na ninavyokata Bima ya Gari langu, je Serikali au mwajiri ana ulazima gani wa kunichangia kwenye BIMA ya gari langu? Of course wakipenda wanaweza ila hawalazimiki kufanya hivyo.
NNE: Kwa policy niliyoongelea hapo juu ya ya 3% kwenye mshahara, Profesa tuseme aliye na msahara wa takribani million 7, analazimika kuchangia Tshs 210,000/= kwa mwezi sawa na Tshs 2,520,000/= kwa mwaka kitu ambacho ni hela nyingi mno kwa mwaka kwa sababu Serikali nayo tena inalazimika kumchangia kiasi hicho. Kwa uelewa wangu, the most expensive Bima ya Afya ambayo si ya NHIF, inaweza ikagharimu si zaidi ya Tshs 200,000/= kwa mwaka. Kwa hiyo unaweza kuona kuwa Profesa anatoa hela kwa mwezi ambayo ilikuwa inamtosha kulipia Bima ya Afya kwa Mwaka mzima, na bado tena Serikali nayo inatoa kiasi hicho.
HITIMISHO:
Huu mfuko ulitengenezwa katika namna ambayo ulipewa loopholes za kukusanya hela nyingi unnecessarily, huku ukiwaumiza wanachama na Serikali pia. Nashauri Serikali walifanyie kazi hili ili Premiums za NHIF ziwe kiwango kimoja kwa wanachama wote Tanzania nzima, na ikiwezekana wale wanaokatwa kwenye mshahara, wakatwe mara moja tu kwa mwaka na si kila mwezi. Watu wanakatwa mamillion kwa mwaka kwenye mshahara mpaka unaogopa, na Serikali nayo bado inakuwa imechangia tena kiasi kile kile kama ambacho amekatwa mwanachama. Mfuko huu unatengeneza cash nyingi mno ambayo iko idle na kwa vyvyote vile lazima watu walio na access na cash hizo wawe propmted kuzichukua.
Kawaida, BIMA ni mfuko unaokusanya pesa kidogo kidogo sana lakin kwa wanachama wengi sana, na huwa zinafikia kuwa nyingi sana kiasi kwamba haziwezi kuisha unless zimeibiwa au zimetumiwa kwa matumizi tofauti; na hizo hela tena ndiyo huwa zinatumika kurudisha huduma kwa baadhi tu ya wanachama hao, na kwa NHIF naweza kusema, mwanachama mmoja akichangia laki mbili (2) tu mwaka, halafu tuseme wanachama asilimia 80 wakawa wameugua kwa mwaka na kutumia hela hiyo, bado hela hiyo haiwezi kuisha na itaendelea kubaki, tena nyingi tu.
Kwa hiyo maoni yangu ni kuwa premium za NHIF napendekeza ziwe sawa kwa watu wote na zisizidi laki mbili (200,000/=) kwa mwaka, NA SERIKALI ISICHANGIE CHOCHOTE KWENYE MFUKO HUU. Vinginevyo tutazidi kuibiwa. Juzi mme na mke wamejiua Tabora kisa kukosa hela ya matibabu ya mtoto wao, na huwezi kujua pengine hata mtoto naye pia ameshafariki. Kwa mantiki hiyo tumepoteza watu watatu kwa kukosa hela ya matibabu, halafu leo tunaambiwa Billion 3 zimemeyeyuka tena kwenye mfuko ambao ulitakiwa wakati mwingine uwe unatoa huduma hata kwa watu ambao siyo wanachama ambao wana mahitaji ya kipekee kama hawa waliojiua.
UPDATE
Source https://www.ippmedia.com/sw/habari/bodi-ya-mikopo-yashindwa-kubaini-wakopaji-tril-146:
MALIPO HEWA BIMA YA AFYA
Prof. Assad pia alisema uchunguzi wa vitabu vya fedha, taarifa za benki na hati za malipo za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, ulibainika kuwapo kwa malipo ya kiasi Sh. bilioni tatu.
Kati yake, Sh. bilioni 2.61 ni malipo hewa, Sh. milioni 350.8 ni malipo ambayo walipwaji hawakubainika na Sh. milioni 42.6 hazikuthibitika kupokewa na walipwaji.
CAG alisema malipo hayo yalitakiwa kulipwa kwa watoa huduma za afya kwa kutumia hundi zilizofungwa, lakini yalifanywa kwa fedha taslimu kinyume cha Kanuni za Fedha za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Pia, makusanyo ya mwaka yanaendelea kuwa makubwa zaidi ya malipo ya huduma za bima ya afya, ambapo kwa sasa malipo ya huduma za afya yanakua kwa uwiano mkubwa mwaka hadi mwaka, zaidi ya uwiano wa kukua kwa mapato.
"Kutokana na hali hii, makisio ya madai ya huduma za bima ya afya pekee ifikapo mwaka wa fedha utakaoishia Juni 2024, yatakuwa ni asilimia 99.2 ya jumla ya makusanyo yote. Uwiano huu unakisiwa kuongezeka zaidi hadi kufikia asilimia 104.8 katika mwaka unaofuata.
"Hali hii inamaanisha kwamba madai ya huduma za bima ya afya yanaendelea kuongezeka na itafikia kipindi ambapo makusanyo na mapato kutoka katika uwekezaji hayataweza kukidhi madai na hivyo itaulazimu mfuko kuchukua hatua za dharura kama kuuza mali zake," alisema.