Gari kutokuwa Stika ya Nenda kwa Usalama Barabarani ni miongoni mwa Road Traffic Related Offences na upatikanaji wake uko vipi??

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Jana J'mosi tarehe 21/09/2019 nilikuwa nasafiri na gari yangu binafsi kutoka Shinyanga kwenda Bariadi (Simiyu) kikazi.

Kutoka Shinyanga utapita Maganzo (ulipo mgodi wa almas wa Mwadui) kisha mbele kidogo utakuta kijiji/mji mdogo wa Mwigumbi.

Hapa ni Njiapanda ya Mwanza/Bariadi.

Tuliachana na barabara kuu iendayo Mwanza na kuchepuka kulia kuelekea mashariki kaskazini ndiko iliko Bariadi makao makuu ya mkoa wa Simiyu.

Mpaka hapo Mwigumbi junction ya Mwanza/Bariadi ni umbali wa takribani 40km toka Shinyanga mjini.

Kufika hapo njiani katikati tulipita vizuizi vya polisi vitatu na kote huko kwa kuwa mimi ndiye nilikuwa dereva, sikuwa na tatizo lolote ili mradi unaendesha kwa ku - observe sheria za usalama barabarani unapoendesha gari yako.

Kutoka hapo junction Mwigumbi hadi Bariadi ni takribani 100km na ni takribani 140km ukitoka moja kwa moja Shinyanga - Bariadi.

Lakini kabla ya kufika huko utalazimika kupita mji wa Maswa (wilaya ya mkoa wa Simiyu) ambapo ni umbali wa takribani 55km toka hapo junction ya Mwigumbi.

All the way from Mwigumbi hadi Maswa hatukukutana na kizuizi cha polisi wa usalama barabarani hadi tulipokuwa tunaingia mjini Maswa.

Mwanzoni mwa mji wa Maswa, tulikutana nao hawa jamaa polisi wa usalama barabarani, wakatupiga mkono, tukasimama.

Sikuwahi kuona polisi wa ajabu kama hawa wa Maswa, yaani wanaosimamisha kila gari bila kujali umevunja sheria fulani ya usalama barabarani ama la.

Tulidhani wana ukaguzi maalumu siku hiyo, lakini baada ya uchunguzi wetu wa dakika chache, tuligundua kuwa hakuna kitu kama hicho.

Na kwa namna tulivyowaona kwa uwazi kabisa tuligundua kuwa hawa wana njaa kali na wanatafuta fedha tu hapa iwe jua ama mvua toka kwa madereva na siyo kusaidia madereva na kuchukua hatua kwa very very serious road traffic offences.

I was driving. Jamaa akasogea kwenye gari yetu akaangalia bima, akaona kuwa iko valid.

Akasogea dirishani kwa dereva, akaomba leseni na kadi ya gari, nikampa, ziko very valid.

Hakunirudishia na alibaki navyo kwa dakika kadhaa huku akiwa anaizunguka zunguka gari.

Baadaye akanirudia.Kilichofuata ni, kuniambia naomba nioneshe Fire Extinguisher na triangles.

Bahati nzuri, niko vizuri, ninavyo vyote hivyo nikamwonesha.

Akazunguka kwenye gari, baadae akanirudia tena akaja na hoja ya STIKA YA USALAMA BARABARANI.

Sio kwamba sikuwa nayo, ipo na imebandikwa mbele ya kioo sambamba na stika ya bima lakini ni ya mwaka jana 2018. hiyo ndiyo ikawa ishu na kosa langu.

Nikamwambia angalia hiyo hapo. Akasema nataka ya mwaka huu, 2019.

Nikamwambia mimi niliyonayo ni hiyo na kama mnazo hapo nipeni bandika hapo niwape hiyo 3,000 au 5,000 yenu mtuache sisi tuendelee na safari tunawahi majukumu.

Nilishangaa sana wale askari, kwani walikomaa mpaka balaa na tukajua wazi kuwa hawa watu ni njaa kali sana na wapo hapa kwa misheni ya kutafuta makosa tu hata ambayo hayapo ili mradi wapate fedha au "mpaka ueleweke tu" na uwaachie "hata ya maji tu" kwa lugha yao.

Baada ya kuzozana sana kwa muda kidogo na walipogundua huyu jamaa anaelewa mambo, baadye alikuja nadhani kiongozi wao pale.

Huyu kidogo alikuwa na busara fulani. Akatoa maelezo kuwa, Stika ya usalama barabarani inatolewa na Regional Traffic Motor Vehicle (RTO) baada ya kuwa ameikagua gari yako na kujiridhisha kuwa iko OK na ina sifa ya kuwa barabarani.

Akaendelea kuelimisha kuwa, ukifika Bariadi fika polisi, onana naye ukaguliwe na upate Stika mpya ya 2019.

Baada ya dakika kama 30 kuwepo pale, walituruhusu tukaendelea na safari, hatukulipa chochote wala kutuandikia faini nadhani ni baada ya kuzozana nao kwa hoja sana pale.

Sasa maswali yangu tunapojadili hoja hii ni haya yafuatayo na wenye ujuzi wa mambo haya mtusaidie kwa lengo la kuelimishana tu;

1. Hivi gari yako kutokuwa na Stika ya polisi ni miongoni mwa Road Traffic related offences?

2. Je, ni sahihi kweli stika hizi ziwe zinatolewa siku ya nenda kwa usalama barabarani tu ama kila dereva kwenda kumtafuta RTO eti ili akague gari yako na kukupa Stika hiyo?

3. Je, siyo vyema kuwa hawa polisi wanaosimama barabarani siku zote wakapewa mamlaka ya kugaua kila gari ambayo inakuwa haina Stika na wakajiridhisha kuwa iko OK wanatoa Stika hiyo hapohapo na mtu kulipia pesa yao badala ya jukumu hilo kuwa chini ya mtu mmoja tu aitwaye RTO?

Tulifanya shughuli yetu jana na kulala hukohuko Bariadi. Sikuwa na muda wa kwenda kuonana na RTO Bariadi eti ili anipe hiyo Stika. Nimefika nyumbani Shinyanga takribani masaa mawili yaliyopita na nilipita Maswa na safari hii hawakutusimamisha kabisa.

Kiukweli sikuupenda usumbufu huo na tulicheleweshwa kwa zaidi ya dakika 30 for no reason at all kwa sababu gari yangu iko very ok mechanically.

Naomba kuwasilisha na karibuni kwa mjadala.
 
Hayo aliyokuambia askari mwenye busara ni kweli.
Kimsingi kama hauna sticker inabidi uandikiwe mkeka. Ingawa hizi sticker hua zinauzwa elfu 10 bila kukagua gari.
Cha msingi ni kuhakikisha unakua na hiyo sticker.
Mi mwenyewe sina "sticker" kwa sababu gari hairushi maji kwenye "wiper".
Soon ntaenda kuwacheki nisije kupewa mkeka wa trafic.
 
Hizo stika ni ulaji mwingine wa polisi. Zinatolewa kijanja janja na fedha nyingi huishia mifukoni mwa polisi. Kama huyo polisi alivyoelezea lengo hasa la hizo stika ni gari kukaguliwa kwana na likionekana halina kasoro basi inatolewa. Lakini siku hizi wamekuwa wanaziuza bila kufanya ukaguzi wowote na baadhi ya fedha zinaishia njiani. Ni wakati sasa wa serikali kuziondoa kwani hazina manufaa yoyote.
 
Poleni sana huko mikoani...

Kwa hapa Dar raha sana... ukipigwa mkono huna hiyo sticker, unamwambia tu nipatie kama unayo, anakutolea unampa chakae unabandika shughuli imeisha...



Cc: mahondaw
 
Vipi kuhusiana na Stika wanazodsiplay watu fire tena Wakati mwingine unakuta siyo Askari wa Fire ni Jamaa tu wamevaa vizibao vya rangi ya njano
 
Ninachojua mimi ni kwamba hizo sticker zilishapigwa marufuku, kwa sasa ni sticker ya bima tu. Poleni huko mkoani.
 
Hayo aliyokuambia askari mwenye busara ni kweli.
Kimsingi kama hauna sticker inabidi uandikiwe mkeka. Ingawa hizi sticker hua zinauzwa elfu 10 bila kukagua gari.
Cha msingi ni kuhakikisha unakua na hiyo sticker.
Mi mwenyewe sina "sticker" kwa sababu gari hairushi maji kwenye "wiper".
Soon ntaenda kuwacheki nisije kupewa mkeka wa trafic.
Stika haina faini...
 
Kama ungeliinunua tu hiyo stika yao sidhani kama ungelipoteza muda wako dk 30. Si mchezo. Zaidi ya yote, ule usumbufu wa kipumbavu pale barabarani. Kukaa na mtu ofisini kwake dk 30 unamwangalia tu. Mtu ambaye unaweza amua kujiondokea na asikufanye lolote ila umeamua tu kuitii sheria bila shuruti.

Nenda kainunue hiyo stika kama unataka kusafiri kwa amani njiani. Lolote laweza kutoke ukajikuta umesafiri tena kwa hiyo hiyo gari kwenda sehemu ingine kwa haraka ukajikuta umesimamishwa tena na sasa ukapoteza saa 1 nzima na ukapigwa fine shs 30thou.

Hujiulizi, Triangle zina kazi gani kwenye gari yako ikiwa umepata breakdown porini?? Lakini wasio nazo huchojolewa 30thou bila hata huruma
 
Kama ungeliinunua tu hiyo stika yao sidhani kama ungelipoteza muda wako dk 30. Si mchezo. Zaidi ya yote, ule usumbufu wa kipumbavu pale barabarani. Kukaa na mtu ofisini kwake dk 30 unamwangalia tu. Mtu ambaye unaweza amua kujiondokea na asikufanye lolote ila umeamua tu kuitii sheria bila shuruti.
Nenda kainunue hiyo stika kama unataka kusafiri kwa amani njiani. Lolote laweza kutoke ukajikuta umesafiri tena kwa hiyo hiyo gari kwenda sehemu ingine kwa haraka ukajikuta umesimamishwa tena na sasa ukapoteza saa 1 nzima na ukapigwa fine shs 30thou.
Hujiulizi, Triangle zina kazi gani kwenye gari yako ikiwa umepata breakdown porini?? Lakini wasio nazo huchojolewa 30thou bila hata huruma

1. Ndicho nilichokitaka kukifanya, yaani wakague gari na kama wangejiridhisha kuwa iko okay, wanipe hiyo stika na ningelipa fedha hiyo iwe 3,000 ama 5,000 ama 10,000

2. Tatiza ikawa, hawana hata hizo stika zenyewe pale barabarani na kumbe zinakuwa kwa mtu mmoja tu RTO na wakaniambia nikamtafute, akague na ndipo atoe hiyo tiketi.....

3. Hoja yangu hapa siyo kupingana au kugomea hizo stika.

Hoja yangu kama umenisoma vizuri na kunielewa, ipo kwenye mfumo wa upatikanaji wake, kwamba siyo mzuri na umejaa ukiritimba....!!

Hiki ndicho wanachopaswa kukirekebisha

I hope, utakuwa umenielewa sasa na ndiyo maana nimeuliza, kama hili ni miongoni mwa makosa ya usalama barabarani au la.....

Bahati njema, kwa baadhi ya michango ya wadau, inaonekana kumbe ni kosa na unaweza kuwa charged kwa kutokuwa nayo....

Kama ndivyo, basi waweke mfumo rafiki na rahisi wa kuzipata....!!
 
Kwakweli wakati wa stika ukifika huwa naenda kwa VECO namgea pesa ya stickerz za magari yote ya ndugu wa karibu anaandika namba za magari yote mi nawapelekea jamaa zangu.
 
Sticker hizi za Nenda kwa usalama barabarani ni za lazima ila muda wa ukaguzi kama unayo au laa bado ni hadi 01 Oktoba na zinapatikana kwa RTO au Traffic Inspectors wa stendi ya mkoa husika
 
Mimi mwenyewe nilikuwa natembea na sticker ya 2018 kwa muda tu mpaka hapa juzi walipo nikomalia nitoe faini 30,000 nikagoma na kuwaambia ninayo ijua mimi ni hiyo niliyonayo sina habari ya hizo mpya wala sijasikia tangazo popote.
Tulipambana sana mpaka wakasimamisha gari nyingine ili nizione hizo sticker mpya na nilipoziona tukaafikiana nifuate utaratibu nikaifuate kama hiyo, nilipotulia siku kadhaa nilimtuma boda boda tu akaifuata.
 
Taffic wana njaa sana siku hizi, na toka wawe wanapewa % kwenye hiyo elfu 30 wamekuwa ni tatizo, kuna siku saa 5 asubuhi pale visiga seminary wamenipiga cheti kisa taa moja kati ya tatu za nyuma nyekundu ya breki ilikuwa haiwaki
 
Mimi kuna siku walinikamata wakanitafutia Makosa yote wakakosa

Kila kitu kimekamilika Mpaka Viatu vya Wazi nilivyovaa Vina Mkanda juu ya Kisigino, na kila kitu kipo wamenikagua sana Mpaka tyre

Wakaishia kuniambia Mzee tusaidie Vijana wako walau elf 5 tukapate Lunch

Ikabidi kwa huruma nikawapa Elf 10
 
Kama ndivyo, basi waweke mfumo rafiki na rahisi wa kuzipata....!!
Uliuanza vizuri uzi wako, ukaeleza jinsi ulivyowaona hao jamaa na njaa zao. Hivyo basi, elewa kuwa askari wa Tz hawana kuelekeza mtu wanajua tu kukuadhibu. Wanajua wazi kabisa kuwa RTO hana nafasi wala hivyo vifaa vya kuchunguzia magari yetu. Hivyo hizo stika hutolewa na maaskari hao hao kwa kipindi kifupi sana ili wapate chakula chao kwa wale watakao chelewa. Ukienda kipindi chake bei ni sh 5000/= hizo za 3000/= na sha 10000/= hizo za 5000/=. So, ni wewe uwe ukiulizia ikifika April - June kila mwaka. Maaskari wengi huwa nazo barabarani bora tu ujue namba ya gari lako.
 
Uliuanza vizuri uzi wako, ukaeleza jinsi ulivyowaona hao jamaa na njaa zao. Hivyo basi, elewa kuwa askari wa Tz hawana kuelekeza mtu wanajua tu kukuadhibu. Wanajua wazi kabisa kuwa RTO hana nafasi wala hivyo vifaa vya kuchunguzia magari yetu. Hivyo hizo stika hutolewa na maaskari hao hao kwa kipindi kifupi sana ili wapate chakula chao kwa wale watakao chelewa. Ukienda kipindi chake bei ni sh 5000/= hizo za 3000/= na sha 10000/= hizo za 5000/=. So, ni wewe uwe ukiulizia ikifika April - June kila mwaka. Maaskari wengi huwa nazo barabarani bora tu ujue namba ya gari lako.

Thank you very much....

Umeeleweka na tunaelewana vizuri tu rafiki yangu....

Mijadala inatakiwa kuwa hivi, bila matusi wala lugha ya kutwezana....

Asante sana....
 
Back
Top Bottom