Kumbe kubandika stika ya BIMA kwenye kioo cha gari ni lazima, hata kama umekata BIMA yako mtandaoni

torosi

JF-Expert Member
Aug 12, 2020
788
1,308
Wana JF,

Leo nlisimamishwa na traffic, akakagua kioo na kukuta sina stika ya BIMA, alivyoniuliza nikamwambia BIMA nshakataa mtandaoni, na kwenye system ya TIRA MIMS inaonyesha gari tayari nina BIMA.

Ila kilichonishangaza zaidi ni kuwa huyu jamaa aliniandikia faini, kosa langu ni KUTOKUBANDIKA STIKA YA BIMA kwa kioo cha gari. Kwa kweli hili limenishangza sana kwamba sasa tuna uwezo wa kukata bima kwa simu, na kupata bima yako instantly .! Ila sheria za traffic bado zinatubana kwamba ni lazima ubandike stika ya bima kwenye kioo!

Sijajua ni nani mwenye jukumu la kubadilisha hii sheria ila ni moja ya sheria ya kijinga sana kuendelea kuwepo, maana kunakuwa hakuna maana ya vifaa vya traffic kuunganishwa moja kwa moja na mfumo wa TIRA kama bado sheria inataka nibandike stika.

Waziri husika tunaomba uliangalie hili.
 
Umepigwa kwa ubwege wako... mimi kama nmeshakata bima na nina tembea na ile document ya kulipia ..hakyanani ntaenda kulala polisi mimi binafsi kioo cha gari ni cheupe pee maana hakina stika hata moja sio ya nenda kwa usalama wala ya nn...
 
Tatizo ni kubandika stika ya BIMA kwenye kioo, NI sheria kabisa na yeye alinionyesha inakutaka kubandika stika.
Sasa makampuni yamebadili utaratibu kwanini yeye alazimishe kutumia kanuni za zamani za kubandika stika na stika hazipo....

Ungemuuliza wakuu wako wa kazi hawajakwambia kuhusu utaratibu mpya au umeamua kuwa tapeli kwa kutumia vazi la uaskari....??!
 
Ukweli hiyo sheria ipo, inataka sticker ibandikwe mahala ambapo panaonekana. Lakini nadhani traffic nae ni kilaza regardless of sheria, kuna mabadiliko ambapo sasa hivi sticker hazitolewi ni kama zimekuwa digitalized kwa hiyo inaonekana online.

Kutokuwa na sticker sio kosa lako ila la serikal kutobadilsha hiyo sheria. Mtata kama mimi hiyo fine atalipa hiyo traffic mwenyewe.
 
Umepigwa kwa ubwege wako... mimi kama nmeshakata bima na nina tembea na ile document ya kulipia ..hakyanani ntaenda kulala polisi mimi binafsi kioo cha gari ni cheupe pee maana hakina stika hata moja sio ya nenda kwa usalama wala ya nn...
Mimi hata hardcopy document sina, nina soft copy kwenye simu, siku nikisimamishwa na traffic itabidi anielimishe kinachotakiwa kufanyika
 
Umepigwa mkuu... Mimi sio kipindi hiki tu hata kabla utaratibu haujabadilika sijawahi kubandika hiyo stickee kwenye kioo... Akitaka huwa namtolea huwa natembea nayo ndani ya gari
 
Issue sio kutokua na BIMA, issue ni sheria inayokutaka lazima ubandike stika ya BIMA hata kama unayo ndani ya gari traffic ana haki ya kukuandikia faini
Traffic hutaka Bima kwa lipi?
Na stika ni kwa lipi?
Wiki 2 askari amekamata hivyo hivyo lkn tulimkatalia Bima si imesoma.
Sasa hivi hakuna stika, askari wanajitoa ufahamu.
Utabandika A4 ya mtandaoni
 
Back
Top Bottom