Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,468
- 113,583
Wanabodi,
Kwa jinsi nilivyo mkereketwa wa demokrasia ya kweli, nilitakiwa niwepo Igunga kushuhudia ama historia mpya ya ukombozi wa Tanzania ikijiandika, ama historia ile ile ya ukandamizwaji na uminywaji wa demokrasia ikijirudia, lakini kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao, nimejikuta ndio kwanza nimelazimika kuwa eneo la Kirua Vunjo, huko Moshi Vijijini kwa tukio fulani.
Ni tukiwa tumekaa huku mgombani, sikutegemea uchaguzi wa Igunga ni main topic mpaka huku!. Ndipo siri za CCM zikaanza kuvuja!. Imeelezwa kuwa CCM inaihofia sana Chadema lakini haiihofi kabisa CUF. Pia adui mkuu wa CUF kwenye uchaguzi wa Igunga ni Chadema na sio CCM.
Kufuatia hilo, CCM imeamua kutumia ule mtindo wa 'Adui wa adui yako ni rafiki yako', hivyo wamejoin forces kwa siri against a common enemy Chadema!.
Mtoa habari huyu ndio akatoa siri kuwa hata ile helcopter ya CUF kule Igunga, imetolewa na CCM ili kuzipunguza kura za Chadema!. Kwa maneno mengine, CCM imeshagundua imepoteza mvuto na Chadema ndicho kinachong'ara, hivyo ili CCM ishinde nilazima ipige kampeni ya nguvu kwa CUF ili kuzi split kura za upinzani na yeyenywe kupeta kwa ushindi kiduchu!.
CUF kwa kukubali kusaidiwa na CCM, imeitumia ile kauli ya ' Baniani mbaya, kiatu chake dawa', kwa kuamini usaidizi huo wa CCM ni ili kukisaidia kushinda!. CUF kilitakiwa kutumia ' I fear the Greeks, especialy when they bring gifts!'.
Kama tetesi hii ni kweli, then ushindi wa CCM huko Igunga ni wazi, lakini ikitokea ikashindwa uchaguzi huu, basi CCM ndio basi tena, itakuwa ni ' La kuvunda hali hitaji ubani'!, safari ya kuelekea kaburini ndio itakuwa imeanza rasmi!
Naomba kuwasilisha
Pasco
Angalizo: Pasco wa jf sio mwanachama wala mshabiki wa chama chochote cha siasa na kwa vile hizi ni tetesi, sitarajii kuulizwa source, ukweli wa tetesi hizi utajihirika baada ya matokeo, maana watu lazima watashikana mashati!.