Kumbe Helicopter ya CUF huko Igunga, imetolewa na CCM!

Kama tetesi hizi zitakuwa kweli, Magamba ni wataalam wa mbinu za kimedani za Kisiasa. tutulie tuone hapo kesho matokeo wa wanaigunga ,
 
Imejulikana kwamba CUF walipewa helikopta na CCM ili kuongeza upingamizi igunga.
Kwa mtazamo huu kweli CUF ni chama kinacho jiendesha chenyewe au ni chama chini
ya CCM.
 
na ndio maana mtatiro kakimbilio JF jana hata kabla ya matokeo kutangazwa ili kuosha jina kumbe janja ya nyani
 
Never trust a Greek

Wanabodi,

Kwa jinsi nilivyo mkereketwa wa demokrasia ya kweli, nilitakiwa niwepo Igunga kushuhudia ama historia mpya ya ukombozi wa Tanzania ikijiandika, ama historia ile ile ya ukandamizwaji na uminywaji wa demokrasia ikijirudia, lakini kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao, nimejikuta ndio kwanza nimelazimika kuwa eneo la Kirua Vunjo, huko Moshi Vijijini kwa tukio fulani.

Ni tukiwa tumekaa huku mgombani, sikutegemea uchaguzi wa Igunga ni main topic mpaka huku!. Ndipo siri za CCM zikaanza kuvuja!. Imeelezwa kuwa CCM inaihofia sana Chadema lakini haiihofi kabisa CUF. Pia adui mkuu wa CUF kwenye uchaguzi wa Igunga ni Chadema na sio CCM.
Kufuatia hilo, CCM imeamua kutumia ule mtindo wa 'Adui wa adui yako ni rafiki yako', hivyo wamejoin forces kwa siri against a common enemy Chadema!.

Mtoa habari huyu ndio akatoa siri kuwa hata ile helcopter ya CUF kule Igunga, imetolewa na CCM ili kuzipunguza kura za Chadema!. Kwa maneno mengine, CCM imeshagundua imepoteza mvuto na Chadema ndicho kinachong'ara, hivyo ili CCM ishinde nilazima ipige kampeni ya nguvu kwa CUF ili kuzi split kura za upinzani na yeyenywe kupeta kwa ushindi kiduchu!.

CUF kwa kukubali kusaidiwa na CCM, imeitumia ile kauli ya ' Baniani mbaya, kiatu chake dawa', kwa kuamini usaidizi huo wa CCM ni ili kukisaidia kushinda!. CUF kilitakiwa kutumia ' I fear the Greeks, especialy when they bring gifts!'.

Kama tetesi hii ni kweli, then ushindi wa CCM huko Igunga ni wazi, lakini ikitokea ikashindwa uchaguzi huu, basi CCM ndio basi tena, itakuwa ni ' La kuvunda hali hitaji ubani'!, safari ya kuelekea kaburini ndio itakuwa imeanza rasmi!

Naomba kuwasilisha

Pasco

Angalizo: Pasco wa jf sio mwanachama wala mshabiki wa chama chochote cha siasa na kwa vile hizi ni tetesi, sitarajii kuulizwa source, ukweli wa tetesi hizi utajihirika baada ya matokeo, maana watu lazima watashikana mashati!.
 
CUF ni Mdudu mbaya anayeishi kwenye nguo zetu, tulishaikataa CCM lakini baadhi yetu tunaivaa CUF. Hawa ndio hao hao wanaonyonya damu zetu na kuwapelekea CCM. Ni jambo la kusikitisha kwamba wamekubali kuwa kupe wasiofaidi damu wanayoinyonya wenyewe, mwelekeo ni kwamba hii ya Igunga haiwezekani CUF wakawa na kura chache kiasi hicho kulingana na ushindani ulivyokuwa. Kinachoonekana hapa CCM waliwatumia sana CUF ili kura zitakazoenda CUF zihamishiwe CCM baadaye, na ndicho kilichofanyika hapo Igunga. Mh. Mahona anapendwa sana tangu hata alipopambana na Rostam, CUF wametumia sana Chopa na haiwezekani vituo vingi CUF wapate kura 1, au 5, au 3... haileti picha. Hii inaonyesha pia Mahona wa CUF siku ya mwisho alipigana kwa kuelekezwa, na atakuwa ameahidiwa jambo ambalo tutaliona matokeo yake sio siku nyingi.

CUF ni Mdudu anayeishi kwenye nguo zetu na kutunyonya damu anayowapa CCM tuliowakataa, CUF ni shetani anayeishi kwenye nyumba zetu anayeiba mali zetu na kuwapelekea CCM tuliowakataa. Sio kificho tena kwamba CUF = CCM, it's official now. Tumkatate huyu Mdudu ama Shetani anayeishi kwenye nyumba zetu kama ndugu yetu kumbe anatunyonya kwa siri.
 
ritz, mimi sina chama na sio mshabiki wa vyama bali maslahi ya taifa.

Niliwahi sema CCM imechokwa siku nyingi bado tuu kutapikwa, kuna ushauri niliutoa humu kwa CCM, wenyewe hawakujibu kitu ila tuu nilishuhudia utekelezaji ambao utakamilishwa na zoezi la kuvuana magamba.

Pia nilisema wengi wanaichagua CCM kwa mazoea tuu sio kwa sababu wanaipenda sana, ila pia nikasema watu hawakuipa Chadema kura za kutosha kwa sababu Chadema haijajipanga, kwa manazi wa Chadema humu niliishia kutukanwa!

Unaweza kuusoma ushauri wangu hapa




Mkuu Pasco, unajisumbua kumwambia ritz asome hapo, maana najua hawezi. Juhudi wanazofanya humu ndani na FF ni wazi wako kikazi zaidi. Utakuwa mwenda wazimu kuendelea kubisha leo hii kuwa CCM imechoka, na imechoka vibaya, wao bado sijui ni kwa utashi wao au kwa mengine tu wanayopata...
 
Back
Top Bottom