Joshua Bukuru
Member
- Apr 16, 2011
- 76
- 95
Lilikuwa jipu lililolelewa na kulewa madaraka. Limeachwa, likaiva na limetumbuliwa muda muafaka. Kuna Jemadari mmoja wa singida mashariki alisema kuwa " tabia za zamani hazifi haraka". Alitaka kufanya kama alivyokuwa anafanya utawala wa Kikwete, akasahau kuwa utawala wa "Maisha bora kwa kila mtanzania" haukuwa na tija kwa wabongo wengi. Sababu jamaa aliingizwa magogoni kwa mabunda ya noti za mafisadi, huyu tulienaye ameingia kwa machozi ya maskini wengi wa vijijini. Hayo aliyoyafanya ameyafanya sana kwenye utawala wa Kikwete.
Alitaka kumzunguka bosi wake akasahau kuwa jamaa alishasema ameamua kuwa " kondoo wa kafara" kwa watanzania. Anayecheza na huyu bwana mara mia akacheze na wajinga wa ukoo wake. Magu hazungukwi tumuombee awa na maisha marefu ili aendelee kutumbua majipu sawa sawa.
Mkuu wa kaya huyu hana utani na mzembe, hana mzaha na wanajirimbikizia mali kwa jasho la watanzania maskini na hana cha msalia mtume na mafisadi. Mimi natoa rai yangu teuzi zote za Kikwete azibwage chini pwaaaaa. Hawa ndiyo waliotutesa watanzania na Tanzania na nchi ikashindwa kusogea mbele kimaendeleo. Ni wale wale waliomuandalia Kikwete safari za nje akawa anapokelewa na wakuu wa shule, wakuu wa NGO's eti kwa kigezo kuwa safari zake zina tija kwa taifa. Baada ya kupiga hatua kwenda mbele, tukajikuta tunapiga hatua kwenda nyuma. Guess who's next?
Jipu lingine lilolowiva ni hili la Bumbuli na ni suala la muda tu. Ombeni na wachina, Bumbuli na waitaliano... litapasuka tu. Tunaomba pia atutumbulie Tegeta escrow Account...atupasulie walioficha noti zetu uswisi na kwingineko.
Maskini Ombeni Sefue atakimbilia wapi...? Atakuwa mgeni na mwenyeji wa nani? Kwa kasi hii ya hapa ni kazi tu, ndani ya miezi 18 atakuwa amemaliza nusu ya majipu yote. Hadi 2020 Bongoland itakuwa sehemu inayoheshimika. Jamaa anatisha...!