Kumbe Bw. Ombeni Sefue alikuwa Jipu..!

Kumbe Bw. Ombeni Sefue alikuwa Jipu..!

Lilikuwa jipu lililolelewa na kulewa madaraka. Limeachwa, likaiva na limetumbuliwa muda muafaka. Kuna Jemadari mmoja wa singida mashariki alisema kuwa " tabia za zamani hazifi haraka". Alitaka kufanya kama alivyokuwa anafanya utawala wa Kikwete, akasahau kuwa utawala wa "Maisha bora kwa kila mtanzania" haukuwa na tija kwa wabongo wengi. Sababu jamaa aliingizwa magogoni kwa mabunda ya noti za mafisadi, huyu tulienaye ameingia kwa machozi ya maskini wengi wa vijijini. Hayo aliyoyafanya ameyafanya sana kwenye utawala wa Kikwete.
Alitaka kumzunguka bosi wake akasahau kuwa jamaa alishasema ameamua kuwa " kondoo wa kafara" kwa watanzania. Anayecheza na huyu bwana mara mia akacheze na wajinga wa ukoo wake. Magu hazungukwi tumuombee awa na maisha marefu ili aendelee kutumbua majipu sawa sawa.

Mkuu wa kaya huyu hana utani na mzembe, hana mzaha na wanajirimbikizia mali kwa jasho la watanzania maskini na hana cha msalia mtume na mafisadi. Mimi natoa rai yangu teuzi zote za Kikwete azibwage chini pwaaaaa. Hawa ndiyo waliotutesa watanzania na Tanzania na nchi ikashindwa kusogea mbele kimaendeleo. Ni wale wale waliomuandalia Kikwete safari za nje akawa anapokelewa na wakuu wa shule, wakuu wa NGO's eti kwa kigezo kuwa safari zake zina tija kwa taifa. Baada ya kupiga hatua kwenda mbele, tukajikuta tunapiga hatua kwenda nyuma. Guess who's next?

Jipu lingine lilolowiva ni hili la Bumbuli na ni suala la muda tu. Ombeni na wachina, Bumbuli na waitaliano... litapasuka tu. Tunaomba pia atutumbulie Tegeta escrow Account...atupasulie walioficha noti zetu uswisi na kwingineko.
Maskini Ombeni Sefue atakimbilia wapi...? Atakuwa mgeni na mwenyeji wa nani? Kwa kasi hii ya hapa ni kazi tu, ndani ya miezi 18 atakuwa amemaliza nusu ya majipu yote. Hadi 2020 Bongoland itakuwa sehemu inayoheshimika. Jamaa anatisha...!
Umenena vema mwana wane,, heeee,, eti mengine ya kichina mengine ya kitaliano,, lakini kumbe yote ni MAJIPU,,
 
Ombeni Sefue kama kiongozi yeyote yule hakuandikiwa kukaa katika nafasi moja milele. Kama Kikwete alivyotoka, vivyo hivyo kwa Sefue muda wake ndio ulikuwa umekwisha. Tusifanye ni issue kuubwa sana.
 
Dhana ya hapa kazi tu sasa inageuka kuwa hapa ni fitina, majungu na kulipizana visasi ,mpaka mwaka unaisha tutashuhudia mengi

majipu yataota kama uyoga kila kukicha
watafukuzwa wangapi..?
 
Hiki ni mojawapo ya kilichomponza Sefue alivunja ndoa ya kijana mmoja wa kigogo akamchukua huyo Mke akampangishia Nyumba Masaki na kumpa Ajila kubwa kwenye kampuni ya Gesi na mafuta , hivyo mme wa huyo Mke alikwenda kulalamika live Kwa Magufuli akatoa ushahidi wa jinsi walivyoanza mahusiano pindi walipokutana na Sefue Uswiz wakati alipoenda kusoma huko na Sefue alikuwa huko kikazi , pia kuna Madili mengi kapiga 10% akiwa hapo ikulu na baya zaidi amekuwa akitoa Siri zote za ikulu Kwa Kikwete hivyo ndivyo vimemponza zaidi .
Dah hatari kweli kweli
 
Nikweli anatumbua lakini ni vijipu vidogo. Majipu makubwa kama mkurugenzi (uchaguzi wa meya wa jiji ),Jecha, uchaguzi Zanzibar, Mzee wa Malofa, Mzee wa Maisha bora kwa kila mtz, mzee wa vijisenti, kijana wa sembe, mama wa ml 10 ni hela ya mboga n.k
Hapo kidooogoo nitaanza na kuwa na imani. Lkn hivihivi hata twiga mmoja hajarudishwa halafu nianze kusifia? thubutuuuuu!!!!
 
Leo nilikuwa naagalia ITV habari wakati balozi Kijazi anaapishwa Sefue alikuwa anashuhudia na alihojiwa akamshukuru Raisi Magufuli kwa kumpa nafasi ya kulitumikia taifa kwa siku chache na kwa kumwamini afanye kazi katika kipindi hiki cha mpito.

Bado alikuwa na lile lile tabasamu lake.

Binafsi nimeona ameonyesha ukomavu mkubwa sana na uana diplomasia uliyo tukuka kwa kuhudhuria na kumshukuru Raisi.

Mengine mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni
 
Lilikuwa jipu lililolelewa na kulewa madaraka. Limeachwa, likaiva na limetumbuliwa muda muafaka. Kuna Jemadari mmoja wa singida mashariki alisema kuwa " tabia za zamani hazifi haraka". Alitaka kufanya kama alivyokuwa anafanya utawala wa Kikwete, akasahau kuwa utawala wa "Maisha bora kwa kila mtanzania" haukuwa na tija kwa wabongo wengi. Sababu jamaa aliingizwa magogoni kwa mabunda ya noti za mafisadi, huyu tulienaye ameingia kwa machozi ya maskini wengi wa vijijini. Hayo aliyoyafanya ameyafanya sana kwenye utawala wa Kikwete.
Alitaka kumzunguka bosi wake akasahau kuwa jamaa alishasema ameamua kuwa " kondoo wa kafara" kwa watanzania. Anayecheza na huyu bwana mara mia akacheze na wajinga wa ukoo wake. Magu hazungukwi tumuombee awa na maisha marefu ili aendelee kutumbua majipu sawa sawa.

Mkuu wa kaya huyu hana utani na mzembe, hana mzaha na wanajirimbikizia mali kwa jasho la watanzania maskini na hana cha msalia mtume na mafisadi. Mimi natoa rai yangu teuzi zote za Kikwete azibwage chini pwaaaaa. Hawa ndiyo waliotutesa watanzania na Tanzania na nchi ikashindwa kusogea mbele kimaendeleo. Ni wale wale waliomuandalia Kikwete safari za nje akawa anapokelewa na wakuu wa shule, wakuu wa NGO's eti kwa kigezo kuwa safari zake zina tija kwa taifa. Baada ya kupiga hatua kwenda mbele, tukajikuta tunapiga hatua kwenda nyuma. Guess who's next?

Jipu lingine lilolowiva ni hili la Bumbuli na ni suala la muda tu. Ombeni na wachina, Bumbuli na waitaliano... litapasuka tu. Tunaomba pia atutumbulie Tegeta escrow Account...atupasulie walioficha noti zetu uswisi na kwingineko.
Maskini Ombeni Sefue atakimbilia wapi...? Atakuwa mgeni na mwenyeji wa nani? Kwa kasi hii ya hapa ni kazi tu, ndani ya miezi 18 atakuwa amemaliza nusu ya majipu yote. Hadi 2020 Bongoland itakuwa sehemu inayoheshimika. Jamaa anatisha...!
Hapo mimi napita njia
Cc jingalao
 
Mchepuko wake umesikitika sana maana nyumba aliyompangia Masaki Kodi yake ni kubwa Sasa anapanga kwenda Mbezi beach kuomba msamaha warudiane na mme wake anaona Sefue hana mamlaka tena wala pesa za kuendelea kumgharamia.
Time will tell.Some stories are difficult to believe.
 
Dhana ya hapa kazi tu sasa inageuka kuwa hapa ni fitina, majungu na kulipizana visasi ,mpaka mwaka unaisha tutashuhudia mengi

majipu yataota kama uyoga kila kukicha
watafukuzwa wangapi..?
Fikra finyu
 
mwancheni mzee atengeneze inchi ili mafisadi wapya tukiingia tupate hela ya mboga
 
Ambaye bado anafikri Magufuli ni wa mzaha mzaha namuonea huruma
 
Hiki ni mojawapo ya kilichomponza Sefue alivunja ndoa ya kijana mmoja wa kigogo akamchukua huyo Mke akampangishia Nyumba Masaki na kumpa Ajila kubwa kwenye kampuni ya Gesi na mafuta , hivyo mme wa huyo Mke alikwenda kulalamika live Kwa Magufuli akatoa ushahidi wa jinsi walivyoanza mahusiano pindi walipokutana na Sefue Uswiz wakati alipoenda kusoma huko na Sefue alikuwa huko kikazi , pia kuna Madili mengi kapiga 10% akiwa hapo ikulu na baya zaidi amekuwa akitoa Siri zote za ikulu Kwa Kikwete hivyo ndivyo vimemponza zaidi .
Hilo la kutoa siri kwa Kikwete ndiyo sababu kila Katibu Mkuu kiongozi wa serikali ya awali hukaa kidogo tu kwenye serikali mpya na baada ya handover hutolewa.

Mwinyi alipata tatizo hilohilo kwa Timothy Apiyo. Apiyo alikuwa anatoa habari zote za Ikulu kwa Nyerere. Mwinyi akamuondoa na kumuweka Rupia.

Imekuwa kawaida kila rais akitoka, baada ya handover, Katibu Mkuu kiongozi naye hutolewa.
 
Leo nilikuwa naagalia ITV habari wakati balozi Kijazi anaapishwa Sefue alikuwa anashuhudia na alihojiwa akamshukuru Raisi Magufuli kwa kumpa nafasi ya kulitumikia taifa kwa siku chache na kwa kumwamini afanye kazi katika kipindi hiki cha mpito.

Bado alikuwa na lile lile tabasamu lake.

Binafsi nimeona ameonyesha ukomavu mkubwa sana na uana diplomasia uliyo tukuka kwa kuhudhuria na kumshukuru Raisi.

Mengine mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni
Ilikuwa ni lazima ahudhurie haikuwa hiari yake.

Mojawapo ya sura ya mnafiki ni tabasamu wakati ana uchungu moyoni.
 
Hiki ni mojawapo ya kilichomponza Sefue alivunja ndoa ya kijana mmoja wa kigogo akamchukua huyo Mke akampangishia Nyumba Masaki na kumpa Ajila kubwa kwenye kampuni ya Gesi na mafuta , hivyo mme wa huyo Mke alikwenda kulalamika live Kwa Magufuli akatoa ushahidi wa jinsi walivyoanza mahusiano pindi walipokutana na Sefue Uswiz wakati alipoenda kusoma huko na Sefue alikuwa huko kikazi , pia kuna Madili mengi kapiga 10% akiwa hapo ikulu na baya zaidi amekuwa akitoa Siri zote za ikulu Kwa Kikwete hivyo ndivyo vimemponza zaidi .

Funza....huyu Kijana ndio Yule genius anaesimamia secta ya Dot com?
 
Wakuu, Mimi nipo taasisi Fulani nyeti sana, Kosa kubwa la Ombeni Sefue ni Kutoa Siri za Ikulu na za Bwana Mkubwa kwa Kikwete, hajui au hakumbuki kwamba wapo wanaosikiliza na kufuatilia mawasiliano...hivyo alisikika akitoa siri za bwana mkubwa na Ikulu kwa mstaafu.
 
Lilikuwa jipu lililolelewa na kulewa madaraka. Limeachwa, likaiva na limetumbuliwa muda muafaka. Kuna Jemadari mmoja wa singida mashariki alisema kuwa " tabia za zamani hazifi haraka". Alitaka kufanya kama alivyokuwa anafanya utawala wa Kikwete, akasahau kuwa utawala wa "Maisha bora kwa kila mtanzania" haukuwa na tija kwa wabongo wengi. Sababu jamaa aliingizwa magogoni kwa mabunda ya noti za mafisadi, huyu tulienaye ameingia kwa machozi ya maskini wengi wa vijijini. Hayo aliyoyafanya ameyafanya sana kwenye utawala wa Kikwete.
Alitaka kumzunguka bosi wake akasahau kuwa jamaa alishasema ameamua kuwa " kondoo wa kafara" kwa watanzania. Anayecheza na huyu bwana mara mia akacheze na wajinga wa ukoo wake. Magu hazungukwi tumuombee awa na maisha marefu ili aendelee kutumbua majipu sawa sawa.

Mkuu wa kaya huyu hana utani na mzembe, hana mzaha na wanajirimbikizia mali kwa jasho la watanzania maskini na hana cha msalia mtume na mafisadi. Mimi natoa rai yangu teuzi zote za Kikwete azibwage chini pwaaaaa. Hawa ndiyo waliotutesa watanzania na Tanzania na nchi ikashindwa kusogea mbele kimaendeleo. Ni wale wale waliomuandalia Kikwete safari za nje akawa anapokelewa na wakuu wa shule, wakuu wa NGO's eti kwa kigezo kuwa safari zake zina tija kwa taifa. Baada ya kupiga hatua kwenda mbele, tukajikuta tunapiga hatua kwenda nyuma. Guess who's next?

Jipu lingine lilolowiva ni hili la Bumbuli na ni suala la muda tu. Ombeni na wachina, Bumbuli na waitaliano... litapasuka tu. Tunaomba pia atutumbulie Tegeta escrow Account...atupasulie walioficha noti zetu uswisi na kwingineko.
Maskini Ombeni Sefue atakimbilia wapi...? Atakuwa mgeni na mwenyeji wa nani? Kwa kasi hii ya hapa ni kazi tu, ndani ya miezi 18 atakuwa amemaliza nusu ya majipu yote. Hadi 2020 Bongoland itakuwa sehemu inayoheshimika. Jamaa anatisha...!
Kesho ukisikia mzee kaenda NSSF kuwa mkurungenzi ndio utaamin sio jipu
 
Back
Top Bottom