Mkuu ukichunguza vizuri sio kwamba Azamtv kuna udini bali wanafanya tofauti na tulivyozoea,kiukweli tumezoea kuona vipindi vyenye maudhui ya kikristo na tushaona ni jambo la kawaida,hebu chukua mfano wa tamthilia iliyokuwa ikilalamikiwa ya Sultan kwamba ina mambo ya kiislamu halafu kumbuka ni movie filamu ngapi za kinigeria zimeoneshwa itv zenye maudhui ya kikristo na hatukuona kwamba itv wana udini watu waliangalia na kuburudika bila kujari imani ila Azamtv kuweka tamthilia ya yenye mambo ya kiislamu imekuwa ni jambo tofauti na mazoea yetu ni kitu kipya.
Ile tamthilia ya siri za familia iliyokuwa ikirushwa na kituo cha eatv ilikuwa kutwa makanisani hasa mwishoni mwishoni mwa tamthilia ila kwa kuwa ni vitu ambavyo tumevizoea basi haikuwa shida hakukuwa na malalamiko yeyote kwa eatv. Hiyo chaneli ya taifa tu huwa wanapiga kwaya muda wowote wakiamua hata kama sio jumapili ila hakuna malalamiko ya udini italalamikiwa kwa mambo mengine.
Hiyo filamu ya Yesu watu wa imani zote walikuwa wanaangalia kila Xmass inawekwa ila sasa Azamtv kuweka ile filamu ya kiislamu imekuwa tabu ni kwa sababu hatujazoea,channel 10 imejaa vipindi vya makanisani ila mwenye kutaka kuangalia ataangalia asiyeweza atatoa hakuna lawama ila ajabu Azam anaonekana kaleta udini kumbe sivyo mkuu bali watu tulishazoea udini wa upande mmoja.