Kulipwa mshahara wa Ubunge huku ukiwa huna sifa kikatiba ya kuwa Mbunge siyo uhujumu uchumi?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Endapo mtu atalipwa mshahara na posho Kama Mbunge huku kikatiba akiwa Hana sifa ya Ubunge awezi kushtakiwa kwa kosa la uhujumu uchumu pale atakapoingia kiongozi mzalendo na anayesimamia katiba?

Kama haiwezekani kushtakiwa kwanini watumishi wa Umma wanaokosa sifa zakuendelea kuwa watumishi kwa mujibu wa katiba na sheria wasiendelee kulipwa posho na mishahara pale katibu mkuu kiongozi na hazina watakapojisikia kuwalipa?

Ni sahihi kila kiongozi akawa na mamlaka yakuelekeza matumizi ya fedha za umma hata Kama Kuna ukiukwaji wa sheria na katiba?
 
Mtoa mada uko sahihi lakini nchi hii kwa sasa haijulikani tunaamini Kwenye uhalali or Uharamia. Ni kama viongozi wetu wamelogwa na mchawi amekufa kabla kuwazindua.

Angalia Katiba ndio Sheria mama ya nchi lakini Inachangaza Spika anajiapiza Kulinda Haramu. Kwa ufupi Kwa sasa Hatujui tunaongozwa na Katiba plus Sheria zake or Utashi wa wachache Kwa maslahi yao na chama Chao.
 
Sheria za Uhujumu Uchumi (Zisizo na dhamana) nchi hii zimeanzishwa maalum kwaajili ya kuwasulubu raia na wafanyabiashara tu.

Ukiwa na cheo serikalini ni ruksa kwako kuiba hela za umma, hata kuvamia ofisi/nyumba za raia na mitutu ya bunduki au hata mabomu ya kurusha ni ruksa.

Uwezo wako tu wa kufanya uliwezalo, pia kama unaweza hata kuvamia ofisi za raia kwa kutumia vifaru na ndege za kivita, fresh tu.
 
Endapo mtu atalipwa mshara na posho Kama Mbunge huku kikatiba akiwa Hana sifa ya Ubunge awezi kushtakiwa kwa kosa la uhujumu uchumu pale atakapoingia kiongozi mzalendo na anayesimamia katiba?...
Walipo jiongezea kinga yakutoshtakiwa, walikuwa tayari na dhamira ya uasi dhidi ya katiba na sheria za nchi. Na hali itaendelea kuwa hivyo adi siku wananchi tutakapo acha uoga/unafiki nakuirudisha nchi katika mstari sahihi.
 
Endapo mtu atalipwa mshara na posho Kama Mbunge huku kikatiba akiwa Hana sifa ya Ubunge awezi kushtakiwa kwa kosa la uhujumu uchumu pale atakapoingia kiongozi mzalendo na anayesimamia katiba?

Kama haiwezekani kushtakiwa kwanini watumishi wa Umma wanaokosa sifa zakuendelea kuwa watumishi kwa mujibu wa katiba na sheria wasiendelee kulipwa posho na mishahara pale katibu mkuu kiongoz na hazina watakapojisikia kuwalipa?

Ni sahihi kila kiongoz akawa na mamlaka yakuelekeza matumiz ya fedha za umma hata Kama Kuna ukiukwaji wa sheria na katiba?
Maoni yako yanaheshimika. siasa muda wake umekwisha. tuchape kazi kwa bidii, tulipe kodi wabunge walipwe vizuri waendeshe nchi ikifika siku ya siku una dead na unazikwa huko ndiko kuna mambo bul bul
 
450908765.jpg
 
Endapo mtu atalipwa mshahara na posho Kama Mbunge huku kikatiba akiwa Hana sifa ya Ubunge awezi kushtakiwa kwa kosa la uhujumu uchumu pale atakapoingia kiongozi mzalendo na anayesimamia katiba?

Kama haiwezekani kushtakiwa kwanini watumishi wa Umma wanaokosa sifa zakuendelea kuwa watumishi kwa mujibu wa katiba na sheria wasiendelee kulipwa posho na mishahara pale katibu mkuu kiongozi na hazina watakapojisikia kuwalipa?

Ni sahihi kila kiongozi akawa na mamlaka yakuelekeza matumizi ya fedha za umma hata Kama Kuna ukiukwaji wa sheria na katiba?
Uko sahihi kabisa kwa asilimia 100

Hawa wabunge ambao wamefukuzwa uanachama wao na Chadema, hivi sasa hawana sifa za kiwa wabunge.

Hiki kiburi anachofanya Spika Ndugai ya kulazimisha kuwatambua wabunge hao ni uhujumu wa hali ya juu wa uchumi wetu.

Ila kwa kuwa nchi yetu kwa sasa haiendeshwi tena kwa Katiba ya nchi wala kwa sheria nyinginezo za nchi, Bali nchi hii kwa hivi sasa inaendeshwa na zidumu fikra za Mwenyekiti wa chama cha CCM, basi inatubidi tuwe wapole, kwa kuwa keshapewa mingine mitano tena!
 
Huu nao ni uhujumu uchumi kama ulivo mwingine ila viongozi wao hii sheria hazifanyi kazi kwao coz wao wanajiona ndio wenye nchi pekee yao na wako juuya sheria wanatudandanya kuapa kuilinda katiba lakini wao ndo wnaiingoza kwa kuisigina
 
Ni dharau za wenye mamlaka kwa Katiba na wananchi.

Hawa viongozi wanaosigina katiba, hawajali viapo walivyoapa vya kuinda na kutetea katiba kwa kunyanyua biblia, wewe waache tu laana itawatafuna
 
Kwani Ndugai anasemaje?
Inawezekana na yeye amepewa maelekezo kutoka juu yake.
Makosa ni ya Chadema, walipowafukuza wakawaambia wakate rufaa na wamekata. Rufaa yao ikikataliwa ndo watakuwa wamefukuzwa rasmi ila kwa Sasa bado wanachama.
 
Endapo mtu atalipwa mshahara na posho Kama Mbunge huku kikatiba akiwa Hana sifa ya Ubunge awezi kushtakiwa kwa kosa la uhujumu uchumu pale atakapoingia kiongozi mzalendo na anayesimamia katiba?

Kama haiwezekani kushtakiwa kwanini watumishi wa Umma wanaokosa sifa zakuendelea kuwa watumishi kwa mujibu wa katiba na sheria wasiendelee kulipwa posho na mishahara pale katibu mkuu kiongozi na hazina watakapojisikia kuwalipa?

Ni sahihi kila kiongozi akawa na mamlaka yakuelekeza matumizi ya fedha za umma hata Kama Kuna ukiukwaji wa sheria na katiba?
Sasahivi tunaendeshwa na mtu na siyo sheria na taratibu
 
Back
Top Bottom