Kulikoni Hospitali ya Temeke

mmakonde

JF-Expert Member
Dec 26, 2009
965
66
Kibasika.jpg



Jamani karne ya 21,kwa nini Watanzania tunaruhusu wagonjwa kulala kitanda kimoja hospitalini?
Kumbuka Temeke iko jijini,je huko Mtwara,Kigoma ,Shinyanga na Singida itakuwaje?

Tuliona Super Model Naomi Campbell alipotembelea martenity ward hapo,na kukuta akina mama wajawazito wanalala chini.

Je sisi watanzania ni wazima vichwani?Tunasubiri Wazungu watupe msaada wa vitanda?Kama ni capacity,hatuna pesa za kujenga hospital nyingine?i dont think so!
 
Unatakiwa ujiulize ni nini vipaumbele vya Serekali, cha kufurahisha watawala wameshagundua kamradi ka India hata wakipata mafua wanaenda India,
 
kwanza inatakiwa wilaya za temeke, kinondoni, na ilala kuwe na more than 3 hospitals in each ambazo zina uwezo mkubwa wa vitanda na wodi za wagonjwa. Lakini watawala hilo haliko kichwani mwao, wanawaza kwenda kutibiwa nje halafu wakirudi wanajua watapokelewa uwanja wa ndege.
 
Hivi kwani mafundi welding wakipewa kamradi kakutengeneza vitanda watashindwa?
Mbona wanatengeneza vitu vingine vya quality nzuri tu?
I wish ningekuwa na mamlaka fulani kweli ningefanya hivyo. Si lazima kuwa na vitanda vya hospitali kama vya Magharibi!! Kwani wao walianzia wapi?

Ni ufinyu na utumwa wa mawazo!!

Natamani tungekuwa na Kagame wetu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom