Kule Zanzibar serikali na dini ya kiislamu vina unasaba?

Kule Zanzibar serikali na dini ya kiislamu vina unasaba?

Tunaizungumzia Zanzibar na itikadi zake Za kusoma quran katika hafla tafauti zinazofanyika zanzibar hatuizungumzii Tanganyika,uongozi wa Serikali ya mapinduzi zanzibar unajua kuwa Magufuli ni mkatoliki na Tanzania haina dini lakini kutokana na utamaduni na mila za zanzibar kuran lazima isomwe katika hafla yoyote ya kiserikali,hayo hayajanza Leo wala jana,yameanza kabla Tanganyika haijaungana kisiasa na Zanzibar,wamishionari wa kwanza waliopita zanzibar kwenda kutanganza Ukristo Tanganyika waliosomewa kuran ili waweze kifanikiwa katika safari yao ya kwenda kutanganza dini yao Tanganyika,Democracy isn't
Umeibua mada mpya. Hiyo siku nyingine nikumbushe nitaandika tena. Sitaki kitu kiitwacho utamaduni. Kusomewa kitu ambacho hukiamini sidhani kama kinasaidia. Umesema ni mkatoliki halafu asomewe kitu asichokiamini tena? Huko sitaki kwenda zaidi. Itachafua jukwaa
 
Nakubaliana na wewe,je kuna majina ya kikiristo au ni majina ya kizungu
Kote kuna makosa. Ndio maana mimi naitwa Ngalikivembu. Maana yake kwenye lugha yako ni NimebakiPekeyangu.
 
Kaka isiwe tabu kuungana nanyi,tuachieni mila na tamaduni zetu,kama hampendi mila na tamaduni zetu si mtuache tu,shida ya nini
Mtaweza nyie kweli kubaki peke yenu? Tushawazoesha kuwalisha kijiko cha uji.
 
Nipo zenji
Asilimia 99.99 ni waislamu, hivyo hoja kama yako haina maana.
Zanzibar ukimkuta mkristo jua ni mtanganyika.
Wazanzibar wakristo katika watu 10000 atapatikana mmojaa
 
Wimbo wa taifa unataja neno Mungu..
Je wale wasio kuwa na imani kuhusu huyo Mungu nao wadai litolewe kisa kuna watu hawaamini kuwa yupo?
 
Mtaweza nyie kweli kubaki peke yenu? Tushawazoesha kuwalisha kijiko cha uji.
kwanini mmetumia nguvu za jeshi kutengua uchaguzi......,wazanzibari walipokataa uji wenu wa kijiko kwa njia ya kura,kwa kumchagua wanaemtaka
 
Umeibua mada mpya. Hiyo siku nyingine nikumbushe nitaandika tena. Sitaki kitu kiitwacho utamaduni. Kusomewa kitu ambacho hukiamini sidhani kama kinasaidia. Umesema ni mkatoliki halafu asomewe kitu asichokiamini tena? Huko sitaki kwenda zaidi. Itachafua jukwaa

Sifikirii kama wazanzibari wamefanya vile kumfurahisha Magufuli,mawazo yangu wamesoma kruan kujifurahisha nafsi zao,kama Magufuli anaamini au haamini kazi kwake
 
Zanzibar asilimia 98 ni waislam
na dini sio imani tu ni culture pia.....
Huyo ndo THE BOSS mzee wa facts hakuna chenchenga. Ukija na vihoja vya kichovu kama huyu mleta mada, anakuchana live. Thanks bro you're the boss.
 
Ungekuwepo huo ukristo usingeanzisha hii thread
hata Egypt kuna Ukristo lakini umewahi sikia Egypt viongozi wanazungumza usawa wa dini?

naona mvaa kipedo umepata pa kupumulia Leo, huku bara hatuwatambua hasa awamu hii
 
Nipo zenji
Asilimia 99.99 ni waislamu, hivyo hoja kama yako haina maana.
Zanzibar ukimkuta mkristo jua ni mtanganyika.
Wazanzibar wakristo katika watu 10000 atapatikana mmojaa
Mtanganyika au Mtanzania? Hakuna tanganyika kwa sasa. Huko wote ni watanzania. Wapeni haki yao hiyo asilimia unayoiona ndogo. Tuna mapadre na maaskofu wetu huko. Hatuwezi kupeleka askofu kwa waamini wanane. Huko wakristo wapo wengi tu na ndio maana ni jimbo kamili hilo kwetu. Sio kigango. Tuheshimuni jamani
 
kwanini mmetumia nguvu za jeshi kutengua uchaguzi......,wazanzibari walipokataa uji wenu wa kijiko kwa njia ya kura,kwa kumchagua wanaemtaka
Hilo ni jimbo letu lazima tulicontrol. Na lazima uamini kuwa hiyo sio nchi. Ni sehemu ya Tanzania. Lazima tuhakikishe usalama uko sawia. Tukiwaachia peke yenu mtaanza kutoana macho bure huko
 
Huyo ndo THE BOSS mzee wa facts hakuna chenchenga. Ukija na vihoja vya kichovu kama huyu mleta mada, anakuchana live. Thanks bro you're the boss.
Mbona ameshindwa kuniambia sensa ya lini hizo takwimu zake? Ameshindwa pia kusema kama Zanzibar sio sehemu ya tanganyika. Hizo sifa unazo mpa nadhani unamtwisha mzigo sio wake. Najua hapo ni pagumu na ndio maana anasema kwao dini ya kiislamu ni culture. What's culture in the country?
 
Hilo ni jimbo letu lazima tulicontrol. Na lazima uamini kuwa hiyo sio nchi. Ni sehemu ya Tanzania. Lazima tuhakikishe usalama uko sawia. Tukiwaachia peke yenu mtaanza kutoana macho bure huko

Hahaha kutojiami kwenu,mnatoa sababu zisizokuwa za msigi,kuweni makini na chadema,moto wa kuotea mbali,wazanzibari tayari wameshajua nini wanataka hakuna wa kuazuia,hivi unajua nini kinaendelea hivi sasa Gabon na Viezuela....
 
naona mvaa kipedo umepata pa kupumulia Leo, huku bara hatuwatambua hasa awamu hii
Hoja zimekuishia umebaki kubwabwaja humuwezi the boss.hueleweki halafu kwa taarifa yako wewe sio mbara peke yako,sisi sote ni watanzania bara na visiwani.
 
Hahaha kutojiami kwenu,mnatoa sababu zisizokuwa za msigi,kuweni makini na chadema,moto wa kuotea mbali,wazanzibari tayari wameshajua nini wanataka hakuna wa kuazuia,hivi unajua nini kinaendelea hivi sasa Gabon na Viezuela....
Hakuna Mtanzania anayeweza kusimama mbele ya mtutu na maji ya washa washa. Gabon is a different country with different people though we are in the same continent. Mlio wa baruti tu Mtanzania anashtuka sembuse risasi. Kuiondoa ccm hadi vyombo vya dola vitakapo ichoka. Zanzibar litakuwa tu koloni letu na rais wa kugombea huko anajulikana huku bara.
 
Nani kamwambia serikali ya TZ haina dini? Mapumziko yawe Friday/Saturday basi kwa miaka 50 ijayo?
hivi na yale majoho tunayovaa siku ya graduation vyuoni ni utamaduni wa dini ipi? .na hilo la mapumziko kuwa jumamosi na jumapili aseme halijaakisi udini.mimi ni mkristo lakini kuna vitu tuviache maana sidhani kama vina madhara vikiachwa bali vinaweza leta madhara vikizungumziwa kama hivi.quran ikisomwa kuna tatizo gani?

ukisema Zanzibar ni sehemu ya Tanzania basi ukristo umetawala zaidi katika hii Tanzania, Sehemu ndogo kama zanzibar ambayo kimsingi population yake kubwa ni waislamu kukiwa na uislamu sioni tatzo.

Halafu sio kila kitu kinachoendelea serikalini huwa tunaambiwa,vingapi hatujaambiwa? na sioni kama kuambiwa kutabadilisha chochote.Nadhani huwezi ondoa elements zote za udini serikalini maana dini ni Historia inayofatwa na kutumika milele.
 
Hakuna Mtanzania anayeweza kusimama mbele ya mtutu na maji ya washa washa. Gabon is a different country with different people though we are in the same continent. Mlio wa baruti tu Mtanzania anashtuka sembuse risasi. Kuiondoa ccm hadi vyombo vya dola vitakapo ichoka. Zanzibar litakuwa tu koloni letu na rais wa kugombea huko anajulikana huku bara.

Hayo ni mawazo yako,Omar Bongo katawala miaka 50,wagaboni walikuwa wapole lakini mwisho woga uliwatoka wakaamua kuingia barabarani,kwani unafikiri Gaboni yakuna jeshi au polisi,ni sifa binadamu akisha choka maisha hudanya kisichotegemewa
 
Back
Top Bottom