Ngalikivembu
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,959
- 876
Rais Magufuli ameenda Zanzibar kutoa neno la shukrani. Kwa siku mbili amekuwa akifanya mikutano huko akianzia Pemba na leo alikuwa unguja. Lakini katika kufuatilia ziara yake kila mara husomwa kwanza quran. Sijajua tukio hilo lina maanisha nini huko visiwani. Unguja pia leo kabla jambo lolote imesomwa quran tena. Kusemaje huko dini na serikali ni kitu kimoja? Vina unasaba?
Nafahamu Zanzibar kuna dini zote. Kwanini sasa kisomwe Kitabu kimoja tu? Au waanglikana huko hawatambuliki? Wakatoliki huko hawatambuliki? Uislamu huko ni bora zaidi kuliko wengine? Je serikali ya Zanzibar ina dini? Najua nimewakera, nitawakera pia. Labda kama sina taarifa za kutosha kuwa serikali ya Zanzibar ina dini lakini huku bara serikali haina dini. Najiuliza wale wanao hudhuria mikutano ya Magufuli ni waislamu tu? Maana hata salamu huko ni moja tu. Kuna unasaba gani huko? Naomba kuelimishwa kama sina taarifa basi nipewe tu nitapokea.