Kula ugali usiku nacho ni kipimo cha umaskini

bila ugal uck wife nae hapat chakula ya uck, nmejenga iman kuwa ugal ndo kila kitu
 
Babu yangu na bibi na hata wazee wengi wa kwetu, walikula ugali na makande miaka hao yote, lakini waligonga miaka themanini na zaidi.Wewe na elimu yako uchwara uliyopata, ukifika miaka arubaini na tano utakuwa na bahati sana.

Hizi ni dharau na tambo za kijinga.Kula ugali au chochote kile usiku, ni chaguo la mtu na mara nyingi ni swala la mazoea,mila na desturi,wala halihusiani na umaskini au utajiri.
 
Duh Ndio nimetoka kutupia dona, spinach, ng'ombe, nyanya, nyanya chungu, vitunguu, chumvi na mtindi Lol!
 
Kibaya zaidi, hata huo ugaliwengi tunakoboa mahindi na kuondoa protein yote, tunakula wanga mtupu ambao zaidi ya kuwa na energy, hauna virutubisho.

Tunakula kushiba tu (energy),lakini ugali waunga uliokobolewa (mweupe) hauna virutubisho.

Ugaliwenye protein ni wa dona,wa mahindi ambayo hayajakobolewa, ambao unaonekana ni wa kimasikini kwa sababu ya rangi, kumbe ile rangi ndiyo virutubisho vyenyewe.

Hili ni kweli usiku au mchana.
 
Mtoa mada shule ni Bashite. Ulivyotaja vyote ni wanga. Na mmeng'enyo wa wanga huanzia kinywani. Your so foolish
Matusi ya Nini sasa?

Nionavyo mimi Asili ya vyakula hivyo ni moja Ila vinatofauti hasa kwenye umeng'enyaji.

Jamani, Tambi utafananisha na Ugali?
 

Nakula ugali kwa interest na uchaguzi, sasa sijui unatoa wapi kauli yako kwamba ni chakula cha kimaskini?
 
Mtoa mada naona unawa support wanaume wa Dar wanaopenda kulalia chips na vitu vilaini laini. Sisi wa mikoani tutaendelee kula ugali wetu wa dona, hata usiku wa manane ikibidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo digital watu wengi walivyosikia ugali mawazo yao sembe hiyo ndio hukaa tumbon zaidi ya masaa24 sababu hata kabla hujala hyo ni takataka kula usio kobolewa ni dk45 kwisha viinlishe huenda mahali pake haraka Sana Nadhan nimeeleweka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kula vyakula vyenye wanga zaidi ya aina zingine ndio uashiria mzuri wa umasikini au kipato kidogo.

Na hilo linatuangukia wengi, ugali nusu kilo, maharage kidogo, hakuna mboga mboga wala nyama wala matunda. Hiyo ndio ishara kuwa tu masikini.
 
Imetusaidia kujua kuwa chakula chako cha jioni unakula kuanzia saa mbili usiku na kuendelea. Ushauri wa bure, kula chakula chako cha jioni/usiku kabla ya saa 10 jioni, ugali inclusive.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kuna watu wana mapenzi na ugali, kuna mzee wangu mdogo hata kwenye sherehe kama hakuna ugali basi ataenda kuutafuta mgahawani/hotelini.
 
Usiku wa leo nimekula ugali kwa mbaazi zilizoungwa kwa mafuta ya mbabe wa meza. Hapa nakunywa maji tu! Kitumbo ndiiii!! Kila mtu anapenda ugali.

Arage Jekundu.
 
Hata kama hiyo ndiyo iliyokuwa maana yake mkuu,his presentation is ecxtremely poor.
 
Daah hapa nipo nakandamiza nguna yangu na sato wa kupaka, mara paa, naona bandiko hili!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…