Kukutwa na hatia na kuhukumiwa kwa 'Malkia Wa Pembe za Ndovu' ni kielelezo cha Nia, jitihada na umakini Wa Serikali katika kulinda rasilimali zetu

Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,556
2,000
Hatimaye Malkia Wa Pembe za Ndovu amekutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka kumi na Saba (17) gerezani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Ni pamoja na wenzake wawili.

Nikiwa mtanzania mzalendo, najitokeza hadharani kuipongeza Serikali kwa hatua ya kesi hii. Pamoja na uwezekano Wa uwepo Wa rufaa Mahakama Kuu, itoshe kusema kuwa hukumu ya Leo itakuwa funzo tosha.

Mosi, ujumbe unatumwa kwa wote kuwa Serikali Ina Nia thabiti na inaisimamia Nia hiyo ya kulinda rasilimali za taifa hili kupitia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo. Serikali kupitia Ofisi ya Mkurugenzi Wa Mashtaka na vyombo vya dola imefanya kazi kubwa kuipata hukumu ya Leo.

Pili, hukumu ya Leo imetuma ujumbe kuwa kwenye Nia, msimamo na usimamizi thabiti Wa Sheria Wa Serikali hakuna mkubwa wala mdogo atakayebaki salama. Kila mkosaji, hasa kwenye rasilimali za taifa, ataguswa na kushughulikiwa.

Tatu, hukumu ya Leo imetuma ujumbe kuwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini viko macho muda wote katika kutekeleza majukumu yao. Hukumu ya Leo itume onyo kwa wanaoendelea au wanaopanga kujihusisha na biashara haramu ya nyara za Serikali na kadhalika.

Nne, najua kuwa kuendesha na kuthibitisha shtaka LA jinai si kazi nyepesi. Ndiyo maana naipongeza Serikali kupitia kwa Mkurugenzi Wa Mashtaka nchini kwa kazi kubwa kufanikisha kutumwa kwa ujumbe Wa Leo.

Mali zote za Malkia Wa Pembe za Ndovu zitataifishwa. Funzo kwa wengine. Onyo kwa wanaotamani au kuendelea na kutenda jinai.

Serikali iko macho na haina mchezo 'on serious national matters'!
 

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
12,172
2,000
We fikiria huyo bibi alikuwa akisafirisha meno ya tembo tangu miaka ya 70!

Ni watu wangapi wamefaidika na biashara hiyo?

Ni watu wangapi wamepokea rushwa kuruhusu nyara hizo za serikali kupitishwa kwenye viwanja vyetu vya ndege na mipakani?
 

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
12,172
2,000
malkia alikuwa akichukua pembe za ndovu chini ya serikali ya CHADEMA..
kasukumeni ndege ving'ang'anizi wa madaraka !
Huku mtaani wanasema nafuu utawala wa mbwa kuliko utawala wa ccm unaoteka hadi raia wake na kuwauwa !

Sent using Jamii Forums mobile app

Sawasawa mkuu,

Unamaanisha ule utawala wa mbwa "dog eat dog situation"?

Fikiria hizo kero zitazokuwepo hapo.

Maendeleo hayana vyama.

Sasa tunaelewa kwamba kumbe mtu kama huyo mama anaweza kufungwa kabisa bila mizengwe.
 

chinembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
5,670
2,000
Huwa nashangaa,Tanroad wanamudu kuwekea beacon maeneo ya barabara nchi nzima,na wanafanya ukaguzi was Mara kwa Mara,watu wa maliasili hii kazi imewashinda,huwezi jua hifadhi ni wapi,maeneo ya kijiji yanaishia wapi! Na wanatamba kukusanya matrilioni

Sijui kama maliasili wana drones za kufanya patrol au wamekomaa na patrol za magari,manually,

Sijui kama wametambua maeneo korofi kwa uwindaji haramu wakaweka kamera za siri kurekodi matukio maeneo hayo

Mahusiano ya vijiji na hifadhi yakoje? Hifadhi zinashirikisha jamii kiasi gani?zinachangia kwenye elimu kwa kujenga madarasa? Kununua madawati? Afya na mengine? Wakijua faida ya kuwa jirani na hifadhi watawafichua majangili!

Hifadhi ya Serengeti kubwa kweli,kwa nini hawana ofisi ndogo mwanza,Mara,bunda,lamadi,busega, watu wanahisi hiyo mbuga na masuala mazima ya maliasili ni kazi ya wana arusha na kilimanjaro,hivyo hata wakiua wanyama sio ishu
 

Mina cute

JF-Expert Member
Sep 18, 2018
1,205
2,000
We fikiria huyo bibi alikuwa akisafirisha meno ya tembo tangu miaka ya 70!

Ni watu wangapi wamefaidika na biashara hiyo?

Ni watu wangapi wamepokea rushwa kuruhusu nyara hizo za serikali kupitishwa kwenye viwanja vyetu vya ndege na mipakani?
Lol, kumbe ni Mkongwe Kwenye iyo biashara, ila akikata rufaa nahis ataongezewa kifungo, bora akubari matokeo
 

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
12,172
2,000
Turushieni kapicha kake huyo fisadi mnene

Safi sana Magu
1550596785045.png

Huyo ndo Malkia wa tembo au "Ivory Queen"
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
26,790
2,000
atu, hukumu ya Leo imetuma ujumbe kuwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini viko macho muda wote katika kutekeleza majukumu yao. Hukumu ya Leo itume onyo kwa wanaoendelea au wanaopanga kujihusisha na biashara haramu ya nyara za Serikali na kadhalika.
Wakili? Mh! Ila la Lisu na upelelezi wake limewashinda hata chembe. halafu unawasifia, Wakili! Wakili, wakili!
 

Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
13,966
2,000

sheiza

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
5,201
2,000
malkia alikuwa akichukua pembe za ndovu chini ya serikali ya CHADEMA..
kasukumeni ndege ving'ang'anizi wa madaraka !
Huku mtaani wanasema nafuu utawala wa mbwa kuliko utawala wa ccm unaoteka hadi raia wake na kuwauwa !

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani unadhani chadema ya mbowe ingefanana na chadema ya zitto? Au chadema ya mashinji inafanana na chadema ya dr silaa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom