Kukutwa na hatia na kuhukumiwa kwa 'Malkia Wa Pembe za Ndovu' ni kielelezo cha Nia, jitihada na umakini Wa Serikali katika kulinda rasilimali zetu

wakamatwe na wale ambao wamefanya mpango wa kujenga uwanja wa ndege chato maana hela hazijapangiwa bajeti na bunge ko wote ni wezi tu inabidi na wao watiwe ndani....
ivi yule mdogo/kaka wa rostam vp jamani au hana hatia au zile ni ng'ombe au ndo kuhongwa channel ten
 
Nimekuelewa hasa hiyo ya tanroad kuweka alama nchi nzima ila hawa wachaga wa kaskazini wameshindwa kazi kurundika ndugu zao na watu wa ukanda wao tu kazini

Sent using Jamii Forums mobile app
Wapuuzi sana hawa watu katika suala la kazi (official duties) nawakubali tu kwny private business mfn kujali mteja. Kwny utumishi wa umma na utumishi wa serikali HAMNAZO KABISA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shinikizo tuu toka nje ,mbuzi wa sadaka wengine wengi wanapeta uraiani ndani ni ........... Wakifanya bado
Sawasawa mkuu,

Unamaanisha ule utawala wa mbwa "dog eat dog situation"?

Fikiria hizo kero zitazokuwepo hapo.

Maendeleo hayana vyama.

Sasa tunaelewa kwamba kumbe mtu kama huyo mama anaweza kufungwa kabisa bila mizengwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upuuzi mtupu mtu kaua zaidi ya tembo 80 mnamfunga miaka 10+.. Wakati watanzania wenzetu wakikutwa na gram kadhaa za madawa ya kulevya wananyongwa huko china.

Hao walipaswa kufungwa miaka 50



Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Namba 3 naweza kukuchallenge.
Mama ameua tembo MAMIA.....yaani mnamkamata baada ya mamia ya TEMBO sasa huo UMAKINI unatoka wap?
Hatimaye Malkia Wa Pembe za Ndovu amekutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka kumi na Saba (17) gerezani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Ni pamoja na wenzake wawili.

Nikiwa mtanzania mzalendo, najitokeza hadharani kuipongeza Serikali kwa hatua ya kesi hii. Pamoja na uwezekano Wa uwepo Wa rufaa Mahakama Kuu, itoshe kusema kuwa hukumu ya Leo itakuwa funzo tosha.

Mosi, ujumbe unatumwa kwa wote kuwa Serikali Ina Nia thabiti na inaisimamia Nia hiyo ya kulinda rasilimali za taifa hili kupitia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo. Serikali kupitia Ofisi ya Mkurugenzi Wa Mashtaka na vyombo vya dola imefanya kazi kubwa kuipata hukumu ya Leo.

Pili, hukumu ya Leo imetuma ujumbe kuwa kwenye Nia, msimamo na usimamizi thabiti Wa Sheria Wa Serikali hakuna mkubwa wala mdogo atakayebaki salama. Kila mkosaji, hasa kwenye rasilimali za taifa, ataguswa na kushughulikiwa.

Tatu, hukumu ya Leo imetuma ujumbe kuwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini viko macho muda wote katika kutekeleza majukumu yao. Hukumu ya Leo itume onyo kwa wanaoendelea au wanaopanga kujihusisha na biashara haramu ya nyara za Serikali na kadhalika.

Nne, najua kuwa kuendesha na kuthibitisha shtaka LA jinai si kazi nyepesi. Ndiyo maana naipongeza Serikali kupitia kwa Mkurugenzi Wa Mashtaka nchini kwa kazi kubwa kufanikisha kutumwa kwa ujumbe Wa Leo.

Serikali iko macho na haina mchezo 'on serious national matters'!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom