Kukutwa na hatia na kuhukumiwa kwa 'Malkia Wa Pembe za Ndovu' ni kielelezo cha Nia, jitihada na umakini Wa Serikali katika kulinda rasilimali zetu

Nikiwa mtanzania mzalendo, najitokeza hadharani kuipongeza Serikali kwa hatua ya kesi hii. Pamoja na uwezekano Wa uwepo Wa rufaa Mahakama Kuu, itoshe kusema kuwa hukumu ya Leo itakuwa funzo tosha.
We jamaa nasikia ni Wakili, kweli au uongo?! Anyway, sio issue! Kwahiyo kumbe hukumu ya Ivory Queen imetolewa na serikali?! Halafu; na zile kesi zenye maslahi kwa taifa ambazo watuhumiwa huwa wanakutwa hawana hatia itakuwa ni sahihi na hapo tukiihusisha serikali?
 
Hatimaye Malkia Wa Pembe za Ndovu amekutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka kumi na Saba (17) gerezani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Ni pamoja na wenzake wawili.

Mosi, ujumbe unatumwa kwa wote kuwa Serikali Ina Nia thabiti na inaisimamia Nia hiyo ya kulinda rasilimali za taifa hili kupitia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo. Serikali kupitia Ofisi ya Mkurugenzi Wa Mashtaka na vyombo vya dola imefanya kazi kubwa kuipata hukumu ya Leo.

Pili, hukumu ya Leo imetuma ujumbe kuwa kwenye Nia, msimamo na usimamizi thabiti Wa Sheria Wa Serikali hakuna mkubwa wala mdogo atakayebaki salama. Kila mkosaji, hasa kwenye rasilimali za taifa, ataguswa na kushughulikiwa.

Tatu, hukumu ya Leo imetuma ujumbe kuwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini viko macho muda wote katika kutekeleza majukumu yao. Hukumu ya Leo itume onyo kwa wanaoendelea au wanaopanga kujihusisha na biashara haramu ya nyara za Serikali na kadhalika.

Nne, najua kuwa kuendesha na kuthibitisha shtaka LA jinai si kazi nyepesi. Ndiyo maana naipongeza Serikali kupitia kwa Mkurugenzi Wa Mashtaka nchini kwa kazi kubwa kufanikisha kutumwa kwa ujumbe Wa Leo.

Serikali iko macho na haina mchezo 'on serious national matters'!
Umeandika kama vile wote tunaifahamu hicho kisa cha "Malkia wa pembe za ndovu".

Ungefunguka ni nani, huyo Malkia? Alishikwa wapi? Na pembe ngapi? Hao wenzake ni akina nani? Walishikwa lini?

Hukumu yao ilikuwa kifungo tu bila faini?

Maana kuna mtu tulisikia kashikwa na pembe za ndovu lakini kalipishwa faini na kuwachiwa huru. Sasa vipi huyu Malkia afungwe?
 
kama huyu ana wateja, basi kuna hatari sana! Nina mashaka nauwezo wake wa kufikiri kama mwanasheria/wakili!
Kwenu nyie mtu mwenye akili ni mpaka aanzishe mada za kumsifia yule mzee, mgonjwa wetu ma-harambee.
 
serikali hii kiboko ya vibopa, zamani wenye pesa walikuwa wakishinda kesi kirahisi na kulipwa fidia wakati wamekwiba kila kitu, walaaniwe mawakili feki wanaotumia midomo yao kusema uongo ili mtu atoke ili hali mtu huyu ni mwizi wahedi.
 
Umeandika kama vile wote tunaifahamu hicho kisa cha "Malkia wa pembe za ndovu".

Ungefunguka ni nani, huyo Malkia? Alishikwa wapi? Na pembe ngapi? Hao wenzake ni akina nani? Walishikwa lini?

Hukumu yao ilikuwa kifungo tu bila faini?

Maana kuna mtu tulisikia kashikwa na pembe za ndovu lakini kalipishwa faini na kuwachiwa huru. Sasa vipi huyu Malkia afungwe?
Nashangaa faizafoxy huna habari za malkia wa tembo wakati amekamatwa toka enzi ya kikwete na habari zake zipo hata hapa jf
 
We jamaa nasikia ni Wakili, kweli au uongo?! Anyway, sio issue! Kwahiyo kumbe hukumu ya Ivory Queen imetolewa na serikali?! Halafu; na zile kesi zenye maslahi kwa taifa ambazo watuhumiwa huwa wanakutwa hawana hatia itakuwa ni sahihi na hapo tukiihusisha serikali?
Soma mada nzima uelewe kabla ya kuchangia. Huo ndio uungwana. Halafu, uwakili wangu unahusikaje kwenye mada hii?
 
Unahusika. Unategemea iwe mada ya utabibu kisha MTU anayejinadi kuwa ni daktari aandike humo kama mie mbumbumbu wa fani hiyo watu wataacha kumshangaa?
Anyway Kwa vile unajinadi ni Wakili sasa kuwa wazi una practice wapi ili tuelewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma na nimeelewa!UNAISFIA SERIKALI baada ya watuhumiwa kukutwa na hatia, PERIOD! Kwahiyo jibu maswali yangu sasa!! Kama watuhumiwa kukutwa na hatia kwenye hii kesi basi serikali inapaswa kupongezwa kwa kuonesha nia habiti ya kulinda raslimali za taifa; vipi kuhusu zile kesi ambazo watuhumiwa hawakutwi na hatia?! Na zenyewe zigo la lawama wapewe serikali?! Au nawe ni wale ambao mazuri ni ya serikali lakini mabaya haiyahusu serikali bali watendaji wake?!

REF: Kakake Rostam Azizi ambae alikuwa na zigo la tuhuma including uuzaji meno ya tembo, utakatishaji pesa na uhujumu wa uchumi kabla hatujamuona RA akiwa na Mheshimiwa Rais! Pamoja na bwana huyo kuwa na tuhuma za madai ambayo hukumu yake haiwezi kuwa faini lakini sote tumeshuhudia akilipishwa faini na kusepa!!
 
....... halafu ni kama sehemu nimesoma ama alipe faini 27bilion...
Ni kweli kaambiwa au alipe faini yenye thamani na meno aliyokamatwa nayo yaani hizo bilioni ambazo anakadiliwa aliua tembo 430 ili kupata idadi ya meno aliyokutwa nayo
 
Unahusika. Unategemea iwe mada ya utabibu kisha MTU anayejinadi kuwa ni daktari aandike humo kama mie mbumbumbu wa fani hiyo watu wataacha kumshangaa?
Anyway Kwa vile unajinadi ni Wakili sasa kuwa wazi una practice wapi ili tuelewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wapi nimejinadi kuwa ni Wakili ndugu? Kwenye mada hii nimefanya uchambuzi Wa kisheria? Mimi kuwa Wakili ni fact na haina haja ya kujinadi
 
Wakili? Mh! Ila la Lisu na upelelezi wake limewashinda hata chembe. halafu unawasifia, Wakili! Wakili, wakili!
Seuze hilo la Tundu Lissu; ni wiki chache tu zilizopita kakake Rostam alipelekwa mahakamani na mashitaka yakiwa uuzaji wa meno ya tembo, uhujumu uchumi pamoja, utakatishaji pesa pamoja na kukutwa na risasi kadhaa kinyume na sheria! Sasa Wakili Msomi Petro E. Mselewa atuambie ikiwa kesi kama hiyo hukumu yake inaweza kuwa ni faini!
 
Hatimaye Malkia Wa Pembe za Ndovu amekutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka kumi na Saba (17) gerezani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Ni pamoja na wenzake wawili.

Nikiwa mtanzania mzalendo, najitokeza hadharani kuipongeza Serikali kwa hatua ya kesi hii. Pamoja na uwezekano Wa uwepo Wa rufaa Mahakama Kuu, itoshe kusema kuwa hukumu ya Leo itakuwa funzo tosha.

Mosi, ujumbe unatumwa kwa wote kuwa Serikali Ina Nia thabiti na inaisimamia Nia hiyo ya kulinda rasilimali za taifa hili kupitia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo. Serikali kupitia Ofisi ya Mkurugenzi Wa Mashtaka na vyombo vya dola imefanya kazi kubwa kuipata hukumu ya Leo.

Pili, hukumu ya Leo imetuma ujumbe kuwa kwenye Nia, msimamo na usimamizi thabiti Wa Sheria Wa Serikali hakuna mkubwa wala mdogo atakayebaki salama. Kila mkosaji, hasa kwenye rasilimali za taifa, ataguswa na kushughulikiwa.

Tatu, hukumu ya Leo imetuma ujumbe kuwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini viko macho muda wote katika kutekeleza majukumu yao. Hukumu ya Leo itume onyo kwa wanaoendelea au wanaopanga kujihusisha na biashara haramu ya nyara za Serikali na kadhalika.

Nne, najua kuwa kuendesha na kuthibitisha shtaka LA jinai si kazi nyepesi. Ndiyo maana naipongeza Serikali kupitia kwa Mkurugenzi Wa Mashtaka nchini kwa kazi kubwa kufanikisha kutumwa kwa ujumbe Wa Leo.

Serikali iko macho na haina mchezo 'on serious national matters'!
Kama wafungwa hawa wakitaka kukata rufaa mahakama ya juu na wakahitaji huduma yako ya uwakili kwa malipo manono uko tayari kuwatetea mahakama ya juu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na kuficha ukweli wa 1.5 Tillion ni maelekezo cha nini?
Halafu independence ya mahakama kumbe serikali inaweza ku influence ?aya
 
Unawezaje kuanzisha mjadala wa kijinga kakama huu Eti mahakama kufanya kazi yake au jaji kutimiza wajibu wake tunsifie?Nisawa mtu aje hapo Lumumba akusifie kwakumpelea mwano shule inangia akilini kweli?
 
Ukabila, ukanda, udini, uchama, upendeleo na kufisad nchi na mali zetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hisia na mihemko!!
Na nyie msio wachaga mjipatie nyadhifa sio wivu na chuki za kijinga tu, pambana na hali yako waacheni wachaga daily mnawasema as if wanawazuia nanyi kufanya kazi kujiletea maendeleo yenu.
Mmepita kiasi cha wivu, chuki na roho mbaya dhidi ya wachaga ebu waaacheni mkijua ya kuwa binadamu wote wameumbwa kwa nafasi sawa hivyo nanyi jifunzeni kupambana muwafikie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom