Kuku wako manati ya nini?

Kuku wako manati ya nini?

Si kingine bali ni wivu, wivu mkali wa kupindukia. Wivu huwakilisha kijitabia cha kutojiamini ktk mambo yako.

Nimeshaona au kusikia watu wengi wake kwa waume wenye tatizo la kutojiamini au kuwaamini wapenzi wao hivyo kuona njia pekee ni kumchunga Mpenzi wake, au ukaguzi wa simu zilizoingia na kutoka ikiwa ni pamoja ujumbe mfupi wa maneno.

Wanaume wengine wanadiriki hata kuwaachisha kazi wenzi wao,wengine hata kwenda makwao tu kusalimia utasikia Mume anatoa kisingizio cha nani ataangalia nyumba na watoto.

Huu wote ni uchochezi wa wivu usiodhibitiwa.

Mwanamke anaweza akawa na wivu ila usivuke mipaka vilevile mwanaume unapokuwa na wivu kupita kiasi inakuwa ni aibu tena aibu kubwa sana.

Mwanamke anapenda mwanaume anayejiamini, vinginevyo jiandae kudharauliwa, kuibiwa na mwishowe kuachwa kabisa.

Wote mna wajibu wa kuwa waaminifu, kama humuamini kwanini kupoteza muda wako kwake?

leo asubuhi nlikuwa na kesi ya kujibu.." naona WhatsApp last seen yako ni sa desh desh ulikua unachati na nani???? halafu mbona umeamka hujanisalimia upo bize na nani???
 
Boss tafadhali kwa mwendo huo wa alikuwa wapi? alikuwa na nani? hata kama alikuwa hana nia ya kukusaliti ataanza tabia mbaya, wivu tuwe nao ila usiwe wivu mkali.

where have you been? nataka kuwa taidume to you soon..
 
where have you been? nataka kuwa taidume to you soon..

hha haaa haha.....utakuwa mine taidume kama tu utazijua tabia za Taijike na ukaweza kukidaka kijiti kabla hakijafika chini.
 
Back
Top Bottom