Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 704
- 1,143
Ni ukweli utakaopokelewa kwa hisia tofauti, lakini ndio uhalisia wa hali ya kisiasa ya nchi yetu ulivyo sasa, uchaguzi wa rais 2025, uliisha Aprili 12, 2025 kanuni za uchaguzi ziliposainiwa.
Hii ni tarehe ambayo itakumbukwa kwa CHADEMA kuwa ilikuwa "kusimama nchale, kukaa nchale." Kama wangesaini kanuni za maadili, wangekuwa wamesaliti agenda yao ya "No reform no election" na kugoma kusaini kulimaanisha "Kususia uchaguzi" Ya Rabi nafsi yangu, wakachagua kususa.
Huu ni uamuzi ambao kwa maoni yangu, lilikuwa ni kosa la kimkakati, kwani lilizingatia taswila ya chama chao ya muda mfupi badala ya faida za muda mrefu. CHADEMA walikuwa na nafasi ya kuiga busara ya Mwalimu Nyerere, TANU ilipotakiwa kushiriki uchaguzi wa kura tatu kwa maslahi ya muda mrefu ya chama chao.
To put things in perspective, this move was an ego massage! Na kwakweli mpaka sasa uamuzi huu umeacha hisia zilizogawanyika kwa wafuasi wa CHADEMA, ila kwa CCM jambo moja ni dhahiri, hii ni fursa ya CCM "Kupita bila kupingwa" Na ni dhahiri CCM wamejipanga kuitumia kwa dhati.
Ni mwendawazimu peke yake anayeweza kuamini kuwa kuna mpinzani "serious" nje ya CHADEMA anaweza kumpa mgombea wa CCM changamoto yoyote ya maana katika uchaguzi wa rais 2025.
Kwakuzingatia muktadha wa hali ya kisiasa ya sasa ilivyo, na ukweli kwamba Tume ya uchaguzi imeshatangaza marufuku kwa CHADEMA kushiriki uchaguzi, sioni sababu yoyote ya kutumia mabavu ya Dola kushughulika na CHADEMA.
Kimsingi tangazo la tume ya uchaguzi limeshamaliza uchaguzi, kama siyo Tanzania nzima basi angalau Tanzania bara.
Kwamaoni yangu ni vyema serikali ingeelekeza nguvu kuandaa uchaguzi, badala ya kushughulikia na CHADEMA. Ikiendelea hivi, ipo hatari ya CHADEMA kutumia kisiasa nguvu kubwa inayotumika dhidi yao kutafuta huruma ya jumuiya ya kimataifa na hata kwa wananchi wa Tanzania jambo ambalo kwa namna moja au nyingine litaitia doa taswila ya nchi yetu.