Kuku wako manati ya nini?

Kuku wako manati ya nini?

Mtoa mada we ndo utakuwa unachapiwa tu. Wivu?! Kama n mke/mme ni wangu ninahaki ya kuhoji mambo yake. Watu wengine bhana mnapotosha sana
 
Si kingine bali ni wivu, wivu mkali wa kupindukia. Wivu huwakilisha kijitabia cha kutojiamini ktk mambo yako.

Nimeshaona au kusikia watu wengi wake kwa waume wenye tatizo la kutojiamini au kuwaamini wapenzi wao hivyo kuona njia pekee ni kumchunga Mpenzi wake, au ukaguzi wa simu zilizoingia na kutoka ikiwa ni pamoja ujumbe mfupi wa maneno.

Wanaume wengine wanadiriki hata kuwaachisha kazi wenzi wao,wengine hata kwenda makwao tu kusalimia utasikia Mume anatoa kisingizio cha nani ataangalia nyumba na watoto.

Huu wote ni uchochezi wa wivu usiodhibitiwa.

Mwanamke anaweza akawa na wivu ila usivuke mipaka vilevile mwanaume unapokuwa na wivu kupita kiasi inakuwa ni aibu tena aibu kubwa sana.

Mwanamke anapenda mwanaume anayejiamini, vinginevyo jiandae kudharauliwa, kuibiwa na mwishowe kuachwa kabisa.

Wote mna wajibu wa kuwa waaminifu, kama humuamini kwanini kupoteza muda wako kwake?

Dume ni dume tu, mchekshie jogoo hataki wenzake wasogee, ng'ombe dume hataki wenzake wamsogelee jike. Hivyo wivu ulopitiliza ni sehemu uanaume ila kukaba hadi penaati sasa hapo shughuli!
 
Si kingine bali ni wivu, wivu mkali wa kupindukia. Wivu huwakilisha kijitabia cha kutojiamini ktk mambo yako.

Nimeshaona au kusikia watu wengi wake kwa waume wenye tatizo la kutojiamini au kuwaamini wapenzi wao hivyo kuona njia pekee ni kumchunga Mpenzi wake, au ukaguzi wa simu zilizoingia na kutoka ikiwa ni pamoja ujumbe mfupi wa maneno.

Wanaume wengine wanadiriki hata kuwaachisha kazi wenzi wao,wengine hata kwenda makwao tu kusalimia utasikia Mume anatoa kisingizio cha nani ataangalia nyumba na watoto.

Huu wote ni uchochezi wa wivu usiodhibitiwa.

Mwanamke anaweza akawa na wivu ila usivuke mipaka vilevile mwanaume unapokuwa na wivu kupita kiasi inakuwa ni aibu tena aibu kubwa sana.

Mwanamke anapenda mwanaume anayejiamini, vinginevyo jiandae kudharauliwa, kuibiwa na mwishowe kuachwa kabisa.

Wote mna wajibu wa kuwa waaminifu, kama humuamini kwanini kupoteza muda wako kwake?

Mapenzi ni wivu ndugu, ukiona unapokea simu na kuongea na wanaume kwa uhuru kabisa (hata kama ni marafiki tu) wala hajawahi kujishughulisha kukuuliza ulikuwa unaongea nani, usiku wewe busy whatsapp lakini hajawahi hata siku moja kukuuliza unachat na nani, unachelewa kurudi nyumbani na ukirudi umetupia kilaji lakini hajawahi kukuuliza ulikuwa wapi, anakuona mara kwa mara jamaa mmoja anakupa lift na kuja kukushusha hapo nje lakini hahangaiki nae basi ujue kuna mawili: 1. Huenda huyo bwanaako ni bwabwa 2. Huyo bwanaako hana chembe ya mapenzi na wewe kwa hiyo haguswi na chochote.
 
Mkuu CYBERTEQ Nakubaliana nawe ila nisome vizuri kati ya mistari "wivu uliovuka uliopitiliza mpaka unakuwa kiyuko mbele ya jamii hata kazi inakushinda unakalia kuchunga mke/mme, huu sio wivu tena bali ni dhambi. Tunafunzwa kuwa na kiasi ktk kila jambo.
 
Last edited by a moderator:
Sijui kama nakosea ila navyo elewa wivu ni kitu chetu cha kiasili, ambacho tumelithishwa. Labda tuulizane wivu ni nini? mi naweza kusema ni ubinafsi usiokuwa na uvumilivu uliobebwa na hisia kali za dhana ya umiliki, kifupi hali hii imegawanyika kulingana na chanzo cha ubinafsi huo.

Kuna wivu wa ki MUNGU ambao sitaugusa kabisa. Nitabaki katika mapenzi baini ya wenza, ili ninate na beat ya uzi, matukio mengi mabaya hutokea endepo ustaimilivu wa wivu wa mapenzi unapokuwa mdogo na ukakaa kwa mwenza kwa muda mrefu katika fikira. Ikiwa hali hii itakuganda muda mrefu kwa asili yake utajikuta unaanza kutazama kila jambo kwa hisia zako bila uhalisia. Kuanzia hapo kila kitu ndio huanza kuharibika.

Kipi kifanyike: Jambo la kwanza unalohitaji kufanya ni kufungua njia za mawasiliano na mpenzi wako. Mwambie mpendwa wako kwa utulivu na uwazi kwamba unampenda lakini, unahisia za wasiwasi kuhusu uhusiano wenu ukieleza kipi hasa kinakupa wasiwasi.

Kwa kufanya hivyo kutatoa sura ya kukomaa kwa imani yako kwake kuhusu uhusiano wenu. Mwache akueleze hali ilivyo na ikiwa kwake ni jambo ambalo analiona ni lakawaida mweleze kwamba hulifurahii na mtafute njia nzuri ya kulikabili hapa kutegemea na uzito wa swala lenyewe linalokutia hisia za wivu.

Anza kufikiria kwa nini uhusiano wako upo na ufanye nini kuuboresha hivyo utakuwa umepunguza muda wa kufikiria kinyume, mfano mtaachana lini? Marafiki wa jinsia tofauti na mwenza wako wanaweza kuwa na madhara gani? Kwa sababu wakati mwingine wivu ukizidi hupasisha uovu na kumfanya anaetuhumiwa hataka tuhuma si za kweli kuamua kukamilisha ili alaumiwe kihalali. Na hivyo wivu mkali kuwa chanzo cha kusambalatisha uhusiano.
 
Si kingine bali ni wivu, wivu mkali wa kupindukia. Wivu huwakilisha kijitabia cha kutojiamini ktk mambo yako.

Nimeshaona au kusikia watu wengi wake kwa waume wenye tatizo la kutojiamini au kuwaamini wapenzi wao hivyo kuona njia pekee ni kumchunga Mpenzi wake, au ukaguzi wa simu zilizoingia na kutoka ikiwa ni pamoja ujumbe mfupi wa maneno.

Wanaume wengine wanadiriki hata kuwaachisha kazi wenzi wao,wengine hata kwenda makwao tu kusalimia utasikia Mume anatoa kisingizio cha nani ataangalia nyumba na watoto.

Huu wote ni uchochezi wa wivu usiodhibitiwa.

Mwanamke anaweza akawa na wivu ila usivuke mipaka vilevile mwanaume unapokuwa na wivu kupita kiasi inakuwa ni aibu tena aibu kubwa sana.

Mwanamke anapenda mwanaume anayejiamini, vinginevyo jiandae kudharauliwa, kuibiwa na mwishowe kuachwa kabisa.

Wote mna wajibu wa kuwa waaminifu, kama humuamini kwanini kupoteza muda wako kwake?

Ukiona mtu hakagui simu yako,haulizi nani kakupigia,hafoki ukichelewa kupokea simu,

Ujue hakuna mapenzi hapo wote mnaigiza lkini hamjui kama mnaigiza.
 
Hujambo mpenzi bubu. Ya kizee hayanaga mbitambita au sio?

Wivu kidogo ni muhimu ktk kuboresha penzi ila unapozidi hapo ndo huzaliwa Gubu, kwani mara atakuwa anahisi kama we unamdharau, humpendi, humheshimu na mengine mengi ili mradi tu kujipa unyonge wa hiari.

Sijambo binti kiziwi.... hebu twende PM tukatongozane bila wivu
 
Back
Top Bottom