Kukoroma usingizini: Fahamu chanzo na tiba yake

Faith

Member
Jul 9, 2008
52
11

BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU TATIZO HILI
Nina mtoto wangu wa kike ana mwaka mmoja na miezi sita, kila alalapo huwa anakoroma sana yaani unaweza ukahisi ni mtu mzima huo mkoromo wake!

Je, hii husababishwa na nini? Naweza kumsaidiaje mwanangu aache kukoroma alalapo, maana hata kama ameanza kukoroma nikamstua/kumtingisha na kumlaza vizuri akilala hukoloma tena.

Iila, pia ninae sista wangu nae ni mkoromaji sana tu, je inawezekana amerithi ama? Naye huyu nitamsaidiaje japo ameshakua mtu mzima?

Msaada wenu wana JF unahitajika!
---
---

UFAFANUZI WA JUMLA WA TATIZO HILI

Kukoroma ni tatizo linalowapata watu wengi wakati wanapolala ambalo linaweza kuwatokea watu wa kila umri ingawa hutokea mara nyingi kwa wanaume au watu wanene. Kukoroma huzidi kwa kadri umri unavyoongezeka na

asilimia 54 ya watu wazima hukoroma baadhi ya wakati huku asilimia 25 ya wengine wakiwa na tabia ya kukoroma kila wakati. Kukoroma baadhi ya wakati kwa kawaida sio tatizo kubwa na mara nyingi huleta tu karaha

kwa mtu anayelala karibu na mkoromaji. Hata hivyo kukoroma huko sio tu kwamba huharibu usingizi wa anayekoroma bali pia huwasumbua na kuwakeresha wanaolala karibu na mkoromaji. Wale wenye tabia ya

kukoroma, hukoroma kila wanapolala na mara nyingi huchoka wanapoamka, na watu wa aina hii hushauriwa kumuona daktari na kushauriwa kuhusiana na tatizo hilo. Lakini kabla hatujaendela mbele ni bora tujue kukoroma hasa ni nini au hutokea vipi?

Mtu huwa anakoroma pale kunapokuwa na kitu au sababu yoyote itakayoziba kuingia au kutoka kwa hewa mdomoni na katika pua. Kuta za koo hutikisika wakati wa kupumua na matokeo yake ni sauti inayosikika ya kukoroma. Kuingia au kutoka kwa hewa huweza kuzuiwa na sababu mbalimbali kama vile:

Kuziba tundu za pua kusiko kamili ambako husababisha nguvu zaidi zitumike katika kupitisha hewa kwenye pua wakati mtu akiwa amelala. Kitendo hicho hupelekea nyama laini za pua na koo zijikusanye na kusababisha mkoromo. Kuna baadhi ya watu wanakoroma tu kipindi cha allergy (allergy season) au wanapatwa na matatizo ya sinus.

Baadhi ya matatizo kama vile kupinda pua (deviated septum) au ukuta unaotenganisha tundu za pua na polyps za pua pia huweza kufanya pua zizibe na kusababisha kukoroma. Watu wengi wanaofanya operesheni za pua pia hupatwa na tatizo la kukoroma.

Kuwa na misuli dhaifu katika koo na ulimi. Misuli au nyama za koo na ulimi zinapokuwa dhaifu sana hulegea na kuanguka upande wa nyuma wa sehemu inayopita hewa. Suala hilo hutokea pale mtu anapolala fofofo au kuwa na usingizi mzito na kusababisha kukoroma.

Kuwa na misuli minene ya koo. Hii ni kwa wale watu wanene ambao hata nyama zao za koo pia hunenepa na kupanuka na suala hilo husababisha kukoroma, Pia watoto wenye tonsesi kubwa na adenoids baadhi ya wakati hukoroma.
Kuwa na kilimi kikubwa ni mojawapo ya sababu zinazosababisha kukoroma. Kilimi kirefu kinaweza kuzuia koo na pale kinapotikisika wakati hewa inapita kwa msukumo husababisha kukoroma.

Sababu nyinginezo zinazoweza kumsababishia mtu akorome anapolala ni kuwa na umri mkubwa au uzee, imeshuhudiwa kuwa watu wa makamo na wazee hukoroma, kwani misuli na nyama za koo huanza kuzeeka na kulegea kadri umri unayoongezeka. Vilevile wanaume wanakoroma zaidi kuliko wanawake hii ni kutokana na wanaume kuwa na njia nyembamba zaidi ya hewa kuliko wanawake. Kukoroma pia kunaweza kuwa ni tatizo la kurithi.

Pombe, kuvuta sigara na matumizi ya baadhi ya dawa pia husababisha misuli ya koo ilegee na hivyo hupelekea mtu akorome. Kulala vibaya pia husababisha kukoroka kama vile kulala kichalichali, kwani hufanya nyama za koo zilegee na kuziba hewa.


Je, Dawa ya kukoroma ni nini?
Swali hilo limeuliwa sana na mimi katika kulijibu ningependa kusema kuwa, kujua sababu inayosababisha mtu akorome na kuitatua au kuiondoa sababu hiyo ndiko kunakotibu kukoroma. Sote tunajua adha inayotokana na

kukoroma, na sauti hiyo inavyosumbua hasa iwapo anayekoroma ni mtu wako wa karibu kama vile mumeo, mwenzi wako au yoyote yule inayekubidi ulale naye karibu au katika kitanda kimojana hata chumba kimoja. Kukoroma pia huathiri usingizi wa mkoromaji kwani anayekoroka humbidi aamke mara kadhaa usingizini akijua au

bila kujua kutokana njia zake za hewa kufunga kwa sekunde kadhaa ambapo usingizi pia hukatika. Wanaokoroma pia hushindwa kulala vizuri suala linalopelekea asubuhi wawe wamechoka na kutofanya majukumu yao vyema, na pia wale wanaolala nao karibu hupatwa na matatizo kama hayo. Vilevile tunapaswa kujua kuwa kukoroma kuna

athari za kiafya za muda mrefu kwa mtu anayekoroma hivyo si jambo la kufanyia mzaha na ni tatizo ambalo linapaswa kushughulikiwa na kutatuliwa.

Wataalamu wanatuambia kuwa ili kujua kukoroma kwako kunasababishwa na nini ni bora ushirikiane na mwenzi wako au yoyote unayelala naye ili akuchunguze pale unapolala na kujua jinsi mwili wako unavyokuwa pale unapokoroma. Ni bora aandae orodha na kuchunguza yafuatayo:

1. Kufunga mdomo na kukoroma kunaonyesha kuwa kuna matatizo ya ulimi.
2. Kufungua mdomo na kukoroma kunaonyesha unaweza kuwa na tatizo katika misuli au nyama za koo.
3. Kukoroma unapolala kichalichali kunaonyesha kuwa pengine kwa kubadilisha namna unavyolala kukoroma nako kunaweza kwisha.
4. Kukoroma wakati unapolala kwa kila mlalo kunaonyesha kwamba tatizo lako ni kubwa na pengine kunahitajia tiba kubwa zaidi.

Iwapo umebadilisha namna unavyolala na haikusaidia, unashauriwa ujaribu yafuatayo:
; Punguza uzito
; Safisha njia yako ya hewa. Kuwa na pua iliyoziba hufanya kupumua kuwe kugumu na kusababisha kukoroma. Unaweza kufanya hivyo kwa kutumia dawa za kusaidia kupumua kwa urahisi (nasal decongestants) zinazopatikana kwa urahisi katika maduka ya dawa.
; Wacha kuvuta sigara.
; Lala mapema na pata usingizi wa kutosha kila mara huku ukijiepusha na kuchoka sana. Kunyanyua kichwa kwa nchi 4 huweza kupunguza kasi ya kupumua na kusaidia ulimi na taya kwenda mbele hali ambayo hupunguza kukoroma. Fanya hilo kwa tumia mito maalum ya kupunguza kukoroma au lala bila mto.

Wataalamu pia wanasema kwamba unaweza kupunguza kukoroma kwa kutokula baadhi ya vyakula au dawa kabla ya kulala ambavyo huongeza kukoroma. Vitu hivyo ni kama vile
o Kutokula mlo mkubwa kabla ya kulala.
o Kutokula vyakula vinavyotokana na maziwa au maziwa ya soya.
o Kutokunywa pombe kabla ya kulala.
o Kutotumia dawa aina ya antihistamines.
o Kutotumia vyakula au vinjwaji venye kafeini.

Vilevile wanaokoroma wanashauriwa kufanya mazoezi ya koo ambayo ni pamoja na kuimba, kusoma kwa kurudia rudia voweli (a,e,i,o,u) kwa nguvu kwa dakika tatu mara kadhaa kwa siku, kuweka ncha ya ulimi chini ya meno ya mbele na kurudisha ulimi nyuma kwa dakika 3 kila siku au huku mdomo ukiwa wazi pelekea taya yako upande wa

kulia na wacha ibakie katika hali hiyo kwa sekunde 30. Huku mdomo ukiwa wazi, kaza misuli ya nyuma ya koo na rudia kitendo hicho kwa sekunde thelathini. Unaweza kutizama kwenye kioo na kuona jinsi kilimi kinavyokwenda juu na chini.

Iwapo kukoroma hakutoisha kwa kutumia njia hizo tofauti zilizoelezwa, usife moyo jaribu kumuona daktari na akupe ushauri wa kitiba kuhusiana na tatizo hilo. Madakatari wataalamu wa magonjwa ya pua, masikio na koo au ENT wanaweza kukusaidia zaidi kutatua tatizo hilo. Siku hizi kuna vifaa mbalimbali vinavyotumiwa mahospitalini ili kuondoa kukoroma kama vile kifaa kinachowekwa kwenye meno, CPAP, kidude kinachowekwa mdomoni au hata kufanyiwa operesheni ili kuondoa tatizo hilo.

Dawa ya kukoroma Fanya hivi: Fungua mdomo wako mpaka mwisho, toa ulimi na usukume nje mpaka mwisho,rudisha ulimi ndani mpaka mwisho-rudia mara 20. Ukimaliza utahisi kuna misuli nyuma

na pembeni ya koo umeifanyisha kazi,sasa misuli hii ikilegea ndio inayosababisha kukoroma. Fanya zoezi hili mara 2 mpaka 3 kwa siku na tatizo hili litaisha baada ya siku 10-20 kutegemea mtu hadi mtu.

BAADHI YA MICHANGO NA UFAFANUZI ULIOTOLEWA NA WADAUI
---
---
---
---
---
---
 
Jaribu kumpeleka kwa specialist wa koo na pua waangalie uwezekano wa kuwa ameota nyama kwa ndani inazuaia kupumua vizuri hasa ukiwa umelala...ingawa sababu zaweza kuwa zaidi ha hayoo. Kama uko Dar nenda Mwembechai kuna specialist anaitwa Prof Ekenywa nyuma ya BP MWembechai.

uliza utapaona...
 
Pia kukoroma kunaletwa na uwingi wa mafuta mwilini na ulalaji vibaya.
 
Kukoroma kunaletwa na misuli ya koo kutokua na nguvu na njia rahisi ya kuimarisha misuli hii na kuondoa tatizo la kukoroma ni kutoa ulimi mpaka mwisho mara 20 kutwa mara 2 au 3 kwa siku.Baada ya wiki utaona tafauti kubwa na kupona kabisa baada ya wiki 2 au 3.

Hii ni njia rahisi ambayo inaweza kufanywa na mtu yoyote na mimi mwenyewe nilipona kwa njia hii.
 
Sorry lagatege kutoa ulimi nje kivipi kama unaramba ice-cream au unatoa tu kama nyoka anataka kutema sumu? clarify please...
 
..Sorry lagatege kutoa ulimi nje kivipi kama unaramba ice-cream au unatoa tu kama nyoka anataka kutema sumu? clarify please...

Unafungua mdomo na kutoa ulimi mpaka mwisho[sukuma nje] hebu hapo hapo jaribu mara 20,sasa misuli hiyo unayo isikia ndiyo inayoleta kukoroma kama imelegea
 
Sasa huyo mtoto wa mwaka unusu atayaweza haya mazoezi ya kutoa ulimi nje mara 20?
 
Sasa huyo mtoto wa mwaka unusu atayaweza haya mazoezi ya kutoa ulimi nje mara 20?

Mtoto wa mwaka 1 unusu mbona mkubwa na unafanya nae kama mchezo vile nawe ukifanya.Kama uonavyo njia hii hujaenda kwa daktari wala kumeza dawa zozote na tatizo umeliondoa daima.
 


Ndugu yangu asante kwa ushauri nimejaribu kumwambia atoe ulimi nje kwa kumuoneshea kwa vitendo yaani nami nikawa natoa maajabu anacheka/ananichekea tu hatoi nadhani kwakua mtoto tumeshindwa kuelewana sijui waweza kunipa mbinu/tiba mbadala?
 
Angalizo!

Makala hii nimeinakili kutoka katika blogu ya ISSA MICHUZI, kwa hiyo mwanzilishi wa mada sio mimi.
Endelea...

Habari za kazi mheshimiwa Michuzi,

nilipitia hapa kwenye blog yako nikakuta bwana Chumaka wa Korogwe akiomba msaada wa namna ya kutatua tatizo lake la kukoroma ambalo linamnyima mkewe usingizi.Majibu mengine niliyoyasoma yalikua ya ajabu na pia hayakuweza kumsaidia bwana Chumaka.

Na vifaa vingi vilivozungumzwa kwa mtu aliyopo Korogwe sidhani angevipata kwa urahisi. Kwakua kulikua na comments zaidi ya 35 nikahisi nikiweka na yangu pale wengi hawataiona,naomba uiweke peke yake ili iweze kusaidia watu kama mimi ilivyonisaidia.

Niliwahi kusafiri na mzee wa kijapani kwenda mikoani kikazi na katika safari zetu kuna siku ilibidi tulale kwenye mji mdogo ambao tulikosa vyumba na kupata kimoja tu ambacho kilikua na vitanda viwili.Watu wengi walishaniambia kuwa nakoroma sana nilalapo usiku.Siku ya pili tulipokua tunapata kifungua kinywa yule mzee akaniambia nina tatizo la kukoroma na atanifundisha namna ya kulitatua bila kutumia dawa,mbinu ambayo wanaitumia kwao.

Fungua mdomo wako mpaka mwisho, toa ulimi na usukume nje mpaka mwisho,rudisha ulimi ndani mpaka mwisho-rudia mara 20.

Ukimaliza utahisi kuna misuli nyuma na pembeni ya koo umeifanyisha kazi,sasa misuli hii ikilegea ndio inayosababisha kukoroma.Fanya zoezi hili mara 2 mpaka 3 kwa siku na tatizo hili litaisha baada ya siku 10-20 kutegemea mtu hadi mtu.

Mzee huyu aliniambia mtu anaekoroma mwili wake haupati mapumziko ya kutosha na mara nyingi huamka huku bado akihisi uchovu na husababisha watu wengine kunenepa sana na wengine kukonda ikitegemea mwili wa muhusika na homoni zake.

Tatizo langu liliisha kabisa baada ya wiki 2 lakini naendelea na mazoezi hata mara mbili kwa wiki ili misuli isilegee tena.Kwakua naishi peke yangu ilibidi nimchukue waifu wa siku 2-3 anihakikishie sikoromi kabisa.Nikiamka siku hizi sihisi uchovu ule wa zamani.

Mdau Ibrahim,D'salaam.

Chanzo: MICHUZI
 
Tafadhali nisaidieni kama kuna yeyote anafahamu dawa iwe ya kisasa au kitamaduni ya kuzuia kukoroma. Tafadhali nisaidieni tafadhali sana.
 
Tafadhali nisaidieni kama kuna yeyote anafahamu dawa iwe ya kisasa au kitamaduni ya kuzuia kukoroma. Tafadhali nisaidieni tafadhali sana.
Mkuu unakoroma kama gari bovu?

teh teh teh,

Hopefully watu watakupa mawazo ya namna ya kuondokana na tatizo...
 
1. Know ur slpng position-kuna styl ukilala lazima ukorome, kwa mfano ukilala kifo cha mende lazima kitu kijipe.
2. Unakororma kipindi gani? ukiwa umelewa au usiku wa manane? ukiwa umechoka sana au inakutokea tu soon unavyoingia kitandani.
 
Thanks Nguli kwa kweli huwa inanitokea kila siku nilalapo niwe nimekunywa au la licha ya kuwa tatizo hilo awali sikuwa nalo lilianza siku za karibuni tu.
 
Thanks Nguli kwa kweli huwa inanitokea kila siku nilalapo niwe nimekunywa au la licha ya kuwa tatizo hilo awali sikuwa nalo lilianza siku za karibuni tu.

Kwa wanaJF wa siku nyingi bila shaka watakumbuka kwamba kuna member mmoja aliwahi kuleta suala hili hapa akiomba msaada. Alipewa majibu kibao lakini alijitokeza member mmoja aliyeeeleza kwamba akiwa safarini siku moja na mchina, walifika mahali wakalazimika kutokuendelea na safari na kuamua kutafuta guest house ili walale pale.

Kwa bahati mbaya kulikuwa na chumba kimoja double ambacho hawa wawili walilazimika kukishare. Huyu Bwana alisema alikuwa anakoroma SANA na kesho yake mchina alimwambia ni kipi cha kufanya ili aondokane na tatizo hilo. Juzi nilikutana na mtu eti anaenda kufanyiwa operation ili kutibu kukoroma. Nilimwambia hao wanataka pesa zake hawana chochote.

Dawa hii hapa: Fanya mazoezi ya kuachama na kuutoa ulimi nje kwa nguvu kama mara ishirini au 30 kwa siku. Zoezi hili linasaidia kuirelax mishipa ambayo ikigangamala, inasababisha mtu kukoroma. Nilikuwa na tatizo kama lako lakini tangia mdau alipotoa ushauri wake hapa, kukoroma kwangu sasa imekuwa ni ndoto na hata ndugu zangu walishangaa ni kitu gani kimetokea mpaka nikaacha kukoroma. Just give a try and come back with the results. I believe you will successed.

Tiba
 
Tafadhali nisaidieni kama kuna yeyote anafahamu dawa iwe ya kisasa au kitamaduni ya kuzuia kukoroma. Tafadhali nisaidieni tafadhali sana.


Mkuu maelezo haya kutoka moja ya hospital maarufu duniani Mayo clinic, habari ni ndefu lakini kuna maelezo muhimu.

http://www.mayoclinic.com/health/snoring/DS00297

SNORING
Loud and frequent snoring can be more than just a nuisance to your partner. Snoring may indicate a serious health condition, and it can disrupt your household. Snoring is common. Almost half of adults snore at least occasionally. Snoring occurs when air flows past relaxed tissues in your throat, causing the tissues to vibrate as you breathe, creating hoarse or harsh sounds.

Lifestyle changes, such as losing weight, avoiding alcohol close to bedtime or sleeping on your side, can help stop snoring. In addition, surgery is available that may reduce disruptive snoring. However, surgery isn't suitable or necessary for everyone who snores. As you doze off and progress from a lighter sleep to a deep sleep, the muscles in the roof of your mouth (soft palate), tongue and throat relax. The tissues in your throat can relax enough that they vibrate and may partially obstruct your airway. The more narrowed your airway, the more forceful the airflow becomes. Tissue vibration increases, and your snoring grows louder. Snoring may be an occasional problem, or it may be habitual.

What contributes to snoring
A variety of factors can lead to snoring, including:

§ Your mouth anatomy. Having a low, thick soft palate or enlarged tonsils or tissues in the back of your throat (adenoids) can narrow your airway. Likewise, if the triangular piece of tissue hanging from the soft palate (uvula) is elongated, airflow can be obstructed and vibration increased. Being overweight contributes to narrowing of your airway.

§ Alcohol consumption. Snoring can also be brought on by consuming too much alcohol before bedtime. Alcohol relaxes throat muscles and decreases your natural defenses against airway obstruction.

§ Nasal problems. Chronic nasal congestion or a crooked partition between your nostrils (deviated nasal septum) may be to blame.

§ Sleep apnea. Snoring may also be associated with obstructive sleep apnea. In this serious condition, your throat tissues obstruct your airway, preventing you from breathing. Sleep apnea is often characterized by loud snoring followed by periods of silence that can last 10 seconds or more. Sometimes, complete obstruction does not occur, but rather, while still snoring, the airway becomes so small that the airflow is inadequate for your needs. Eventually, the lack of oxygen and an increase in carbon dioxide signal you to wake up, forcing your airway open with a loud snort or gasping sound. This pattern may be repeated many times during the night...

When to seek medical advice
Seeing your doctor about your snoring can help both you and your partner. For you, snoring may indicate another health concern, such as obstructive sleep apnea, nasal obstruction or obesity. .. If your child snores, ask your pediatrician about it. Children, too, can have obstructive sleep apnea, though most don't. Nose and throat problems, such as enlarged tonsils, and obesity often underlie habitual snoring in children. Treating these conditions could help your child sleep better

Tests and diagnosis
Your doctor likely will perform a physical examination and take a medical history. Your partner may need to answer some questions about when and how you snore to help your doctor assess the severity of the problem.

Your doctor may then refer you to an ear, nose and throat (ENT) doctor (otolaryngologist) or sleep specialist for additional studies and evaluation. This may require that you stay overnight at a sleep center to undergo an in-depth analysis of your sleep habits by a team of specialists.

Complications
Habitual snoring may be more than just a nuisance and a cause of daytime sleepiness. Untreated, persistent snoring caused by obstructive sleep apnea may raise your lifetime risk of developing such health problems as high blood pressure, heart failure and stroke. In children, obstructive sleep apnea may increase the risk of attention-deficit/hyperactivity disorder(ADHD).

Treatments and drugs
Your doctor will likely first recommend lifestyle changes, such as losing weight, avoiding alcohol close to bedtime and changing sleeping positions. If lifestyle changes don't eliminate snoring, your doctor may suggest:
§ Oral appliances
§ Traditional surgery
§ Laser surgery
§ Radiofrequency tissue ablation (somnoplasty)
§ Continuous positive airway pressure (CPAP)
 
Duh pole sana, maana unanikumbusha nilipokua shule ya bweni kuna jamaa alikua anakoroma utafikiri wale chura magamba, sasa wakiwa wawili ndio ndio wanapokezana, kama mwenzangu na mimi hualali usiku kucha
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…