MpiganajiNambaMoja
Member
- Sep 20, 2007
- 69
- 2
Jamani tatizo langu ni kukojoa mara kwa mara ninapokunywa kimiminika chochote. Hali hii hunikosesha raha maana kama nina mkutano inabidi nisinywe chai wala maja.
Kitendo cha kunywa glass moja ya maji au kikombe cha chai kinanifanya nihudhurie maliwatoni kila baada ya dk 7 hadi 10 mara 3 au 4 ndo nakuwa sawa.
Nikinywa bia hali ndio inakuwa mbaya zaidi... Hali hii inaninyima raha sana. Je ni tatizo gani na nifanye nini?
==
==
=====
Kitendo cha kunywa glass moja ya maji au kikombe cha chai kinanifanya nihudhurie maliwatoni kila baada ya dk 7 hadi 10 mara 3 au 4 ndo nakuwa sawa.
Nikinywa bia hali ndio inakuwa mbaya zaidi... Hali hii inaninyima raha sana. Je ni tatizo gani na nifanye nini?
==
Wanajamvi mko salama na mnaendelea na ujenzi wa taifa letu?
Kama Kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, ni kwamba karibu ni mwezi mzima sasa nimekùwa nikisumbuliwa na tatizo la kukojoa mara kwa mara inafikia kiasi ndani ya saa moja nakuwa nimekwenda kukojoa zaidi ya mara mbili na Mkojo unakuwa zaidi ya nusu lita kila ninapokwenda kukojoa.
PIA kwa siku huwa nakunywa maji lita 3 hadi 4.
KIKUBWA NINACHOWAOMBA WAKUU NI KUTAKA KUFAHAMU KAMA HILI NI TATIZO GANI NA PIA USHAURI WENU JUU YA HILI TATIZO.
Ninatanguliza shukran kwa Msaada wenu. +ME
==
Nina tatizo la kuamka usiku hata mara 6 kwa haja ndogo, Nina miaka 37. Huwa sinywi maji wakati wa kulala na mwanaume.
Tatizo hili lina mwaka sasa,nilienda hospital nikapima mkojo na sukari hamna kitu lakini tatizo linaendelea na kunikera sana.
Nyie madaktari wa JF Doctor, tatizo langu ni nini?
=====
Wadau,
Home kwangu naishi na Kijana mmoja, shemeji yangu ambae yuko likizo. Leo ni siku ya nne ananiambia amekuwa akibanwa na haja ndogo kila mara, tuseme kila baada ya dakika 10-15 au hata 20 sometimes. Nimemuona hata nikiwa nae anaenda sana Chooni.
Nimejaribu kuangalia life style yake, jamaa anakunywa sana Juice na Maji but hii sio mara yake ya kwanza kuja kuishi kwangu, na kujipendelea juice na maji vya kutosha, huko kabla hakuwahi kuwa na hii problem.
Leo asubuhi kaniambia kajaribu kuonja mkojo wake akakuta mtamu mtamu, sasa issue ni kwamba huu ni ugonjwa au kawaida? Why now na sio kabla while life style ya juice anayo toka kabla?
Msaada please!!