Kukojoa mara kwa mara kunatokana na nini?

Sep 20, 2007
69
2
Jamani tatizo langu ni kukojoa mara kwa mara ninapokunywa kimiminika chochote. Hali hii hunikosesha raha maana kama nina mkutano inabidi nisinywe chai wala maja.

Kitendo cha kunywa glass moja ya maji au kikombe cha chai kinanifanya nihudhurie maliwatoni kila baada ya dk 7 hadi 10 mara 3 au 4 ndo nakuwa sawa.

Nikinywa bia hali ndio inakuwa mbaya zaidi... Hali hii inaninyima raha sana. Je ni tatizo gani na nifanye nini?

==
Wanajamvi mko salama na mnaendelea na ujenzi wa taifa letu?

Kama Kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, ni kwamba karibu ni mwezi mzima sasa nimekùwa nikisumbuliwa na tatizo la kukojoa mara kwa mara inafikia kiasi ndani ya saa moja nakuwa nimekwenda kukojoa zaidi ya mara mbili na Mkojo unakuwa zaidi ya nusu lita kila ninapokwenda kukojoa.

PIA kwa siku huwa nakunywa maji lita 3 hadi 4.

KIKUBWA NINACHOWAOMBA WAKUU NI KUTAKA KUFAHAMU KAMA HILI NI TATIZO GANI NA PIA USHAURI WENU JUU YA HILI TATIZO.

Ninatanguliza shukran kwa Msaada wenu. +ME

==
Nina tatizo la kuamka usiku hata mara 6 kwa haja ndogo, Nina miaka 37. Huwa sinywi maji wakati wa kulala na mwanaume.

Tatizo hili lina mwaka sasa,nilienda hospital nikapima mkojo na sukari hamna kitu lakini tatizo linaendelea na kunikera sana.

Nyie madaktari wa JF Doctor, tatizo langu ni nini?

=====

Wadau,

Home kwangu naishi na Kijana mmoja, shemeji yangu ambae yuko likizo. Leo ni siku ya nne ananiambia amekuwa akibanwa na haja ndogo kila mara, tuseme kila baada ya dakika 10-15 au hata 20 sometimes. Nimemuona hata nikiwa nae anaenda sana Chooni.

Nimejaribu kuangalia life style yake, jamaa anakunywa sana Juice na Maji but hii sio mara yake ya kwanza kuja kuishi kwangu, na kujipendelea juice na maji vya kutosha, huko kabla hakuwahi kuwa na hii problem.

Leo asubuhi kaniambia kajaribu kuonja mkojo wake akakuta mtamu mtamu, sasa issue ni kwamba huu ni ugonjwa au kawaida? Why now na sio kabla while life style ya juice anayo toka kabla?

Msaada please!!
 
Ndugu yangu Mpiganaji..

Kabla hujamtafuta mchawi wako nenda kapime Kisukari. Hizo ni dalili tosha za kisukari; Kama huna kisukari basi njoo tena hapa utuambie level ya sukari yako ni ngapi kwenye mwili wako ndipo tuendelee na mangine.

Njimba
 
Hapo unaweza kua na kisukari au maambukizi ya njia ya mkojo.Pima mkojo na utajua ni lipi kati ya haya
 
Nilisha enda hospitali nikapima, blood sugar iko normal na mkojo pia ukawa safi. Daktari akanipa madawa fulani nitumie, nikamaliza lakini hali ikawa hivyo hivyo. Majibu ya hospitali siko zote yamekuwa sina tatizo. Lakini mimi nikijilinganisha na watu wengine naona nina tatizo. Au kibofu kangu cha mkojo kidogo nini, te he he he.
 
Umejaribu kucheck prostate cancer? Kukojoakojoa mara kwa mara ni dalili ya prostate cancer pia. Kama ujacheck ningakushauri ufanye hivyo.
 
Kukojowa Mara kwa Mara pia kunasababishwa na Mawazo jaribu pia kupnguza mawazo uliyokuwa nayo kichwani mwako mimi pia nina matatizo hayo ya kukojowa kila mara haswa nikinywa chai au maji ya moto huwa nakwenda ****** kila wakati na nimekwenda kupima kwa Doctor kasema sina ugonjwa wowote najaribu kupunguza kunywa chai na maji ya moto na Mawazo pia ndio Dawa yake hakuna Dawa ingine.
 
Hivi ni kipi kinachosababisha watu wenye kisukari kukojoa mara kwa mara?
Na je kuna kitu kingne kinaweza kusababisha hali hiyo?
 
Wanajamvi mko salama na mnaendelea na ujenzi wa taifa letu?

Kama Kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, ni kwamba karibu ni mwezi mzima sasa nimekùwa nikisumbuliwa na tatizo la kukojoa mara kwa mara inafikia kiasi ndani ya saa moja nakuwa nimekwenda kukojoa zaidi ya mara mbili na Mkojo unakuwa zaidi ya nusu lita kila ninapokwenda kukojoa.

PIA kwa siku huwa nakunywa maji lita 3 hadi 4.

KIKUBWA NINACHOWAOMBA WAKUU NI KUTAKA KUFAHAMU KAMA HILI NI TATIZO GANI NA PIA USHAURI WENU JUU YA HILI TATIZO.

Ninatanguliza shukran kwa Msaada wenu. +ME
 
Pole sana. Na je, maji unakunywa sana? Nenda hosp watashauri zaidi inawezekana ni diabetes kama walivyo hisi watangulizi
 
Mkuu wala huna tatizo kabisa,Tatizo pekee ni kwamba unakunywa maji mengi sana hata kama huna kiu hapo lazima utakojoa mara kwa mara wala sio ugonjwa mkuu,punguza kunywa maji mengi kupita kiasi
 
Huna Tatizo
Hata Mimi Nakunywa Maji Lt 5 Kwa Siku
Nakojoa Lt Moja Na Nusu Kila Baada Ya Masaa 5
Nishazoea Kwani Nina Miaka Mitano Ktk Unywaji Wa Maji!
 
nafikil wanajamvi mko salama na mnaendelea na ujenzi wa taifa letu, Kama Kichwa cha habar kinavyojieleza hapo juu, ni kwamba karibu ni mwez mzima sasa nmekùwa nikisumbuliwa na tatizo la kukojoa mara kwa mara inafikia kiac ndan ya saa moja nakuwa nmekwenda kukojoa zaid ya mara mbili na Mkojo unakuwa zaid ya nusu lita kila ninapokwenda kukojoa PIA kwa siku huwa nakunywa maji lita 3 hadi 4 ,KIKUBWA NINACHOWAOMBA WAKUU NI KUTAKA KUFAHAMU KAMA HILI N TATIZO GAN NA PIA USHAUR WENU JUU YA HILI Tatizo na ninatanguliza shukran kwa Msaada wenu. +ME

Ndugu hilo ctatizo bal ni maji unayokunya ni mengi naunajua maji yanasharabiwa tumbon na kama unasikia kiu mara kwa mara ctahid kuchanganya maji na chumvi au sukar ilkufanya usharabiwaji kuwa kwa kiasi kidogo.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom