Kukojoa mara kwa mara baada ya kupata kinywaji

Figo zako zinakimbelembele/zinapiga kazi kwa kasi ya 4G.

Usithubutu kuanza kutumia madawa utasababisha matatizo mengine.

Tatizo lako ni dogo ila ukilikuza ukakutana na hawa madokta wa mchongo wakakupa dawa zao itakula kwako.
 
UTI sina, Kisukari sina, (majibu ya vipimo mara kwa mara)

Kwa nini napokunywa kinywaji maji au juice kidogo tu napata haja kali ya kukojoa, na kuvumilia inakuwa ngumu na changamoto zaidi. Pia sitaenda mara moja, bali mara mbili au tatu baada ya muda.

Tatizo ni nini, nisaidie
Figo zako ziko njema hazitaki kukaa na sumu

Sent from my LM-V500N using JamiiForums mobile app
 
Nitazingatia mkuu, Kwa hyo boss huu sio ugonjwa bali ni mabadiriko tu ya kimwili.
Viungo vyetu vimetofautiana. Mfano MTU mwingine anakula Milo mitatu kwa siku ila haja/choo anapata Mara moja tu. Mwingine anajisaidia Mara 3 kwa siku haja kubwa. Hii ni kwa sababu mifumo yetu ya mmeng'enyo imetofautiana kulingana na MTU na mtu. Hivyo sishauri MTU kukimbilia hospitali kisa unapata mkojo Mara 2 au 3 baada ya kinywaji. Sikilizia kwanza.

Ingekuwa nje ya nchi kama India sawa hospitali zipo advanced, sasa hizi zetu za michongo inabidi uende kwa tahadhari wasije wakakupa sawa ukaongeza tatizo jingine.
 
Kwa kawaida binadamu, kibiolojia mwishoni kwenye kibofu cha mkojo kuna kitu wanaita "sphincter muscles" hii ni misuli ambayo inasaidia kushikilia mkojo usitoke hata kama umebanwa sana. Sasa ikitokea misuli hii kwa namna yoyote ile imepoteza nguvu, uwezo wa kushkilia mkojo unakua mdogo hvyo, kiasi kidogo tu cha mkojo kwenye kibofu kitapelekea ujiskie kwenda haja.

Hvyo basi, misuli hii inaweza kuimarishwa kwa kufanya mazoezi aina ya "kegel" pitia mtandaoni utaona yanafanyika vipi.

Pia unaweza ukawa unafanya simple exercise ya kustop na kuachia mkojo mara kadhaa pindi unapokua unakojoa. (Kwa wanaume). Hii itasaidia kwa kiasi fulani kuimarisha misuli hii.

Ngoja wajuzi zaidi waje kuongezea maarifa.
 
Back
Top Bottom