DOKEZO Kukatika ovyo kwa umeme hasa msimu wa senene Muleba

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kumekuwa na changamoto ya kukatika Kwa umeme ovyo au umeme kuwa mdogo sana kipindi cha msimu wa senene. Hali hii inatokea sana wakati wa usiku ambapo muda huo ndo wakazi wengi wa Muleba wanategemea huo umeme Kwa ajili ya kutega senene kama chanzo chao cha kipato.

Kabla ya msimu huu wa senene kuanza, wanaojihusisha na shughuli hii waliitwa kikao na TANESCO Muleba na kuhakikishiwa kwamba hakutokuwa na tatizo la umeme kwa msimu huu, lakini mambo yamekuwa ndivyo sivyo.

Hali hii imekuwa kero sana na imepelekea ugumu wa maisha kwani ni msimu ambao watu wengi huutegemea kupata kipato ili kujiendeleza kiuchumi, kutunza familia na kutimiza haja zao za kila siku.

Wengine wamekopa wakiwekeza katika utegaji wa senene lakini kutokana na umeme kuwa wa shida hakuna matumaini tena ya kurejesha mikopo hiyo.

Ninaomba mamlaka husika hasa TANESCO Muleba waliangalie hili kwani haya maisha sio kukomoana maana hiki ni chanzo kikubwa Cha kipato Kwa msimu huu wa senene Kwa wakazi wa Muleba, kwani sio wote wana uwezo wa kutumia genereta pindi umeme unapokatika au kuwa mdogo.
 
Back
Top Bottom