Kukamatwa, kupigwa risasi Lissu: Chama cha Wanasheria Uingereza chamlima barua Rais Magufuli

Hawa wakoloni wanafikiri Tanzania bado ipo chini ya himaya yao? Unamuandikia Rais wa nchi barua alafu unapeleka nakala kwa waziri wake huu ni upuuzi

Hahaha, kwanini waziri asipelekewe nakala. Inategemea barua yenyewe inahusu nini. Hiyo ni sawa na kumuandikia email bosi wako mkubwa na ukamkopy mshauri wake.

Hapo kila kitu kinawekwa peupe ili msije kusema hamkuambiwa. Halafu kwao rais wa nchi ni mtu wa kawaida sana, sio kwenu huku rais anakuwa ni 'mungu' kabisa wakumtolea mpaka sadaka.
 
Yamezidi zaidi ya Maymar(Indonesia)
Yamezidi zaidi ya Palestine?
Yamezidi zaidi ya Congo?

Tujitahidi kuwa makini saana na hawa wenzetu, wameingilia saana..yametosha!

Ni vyema tukawa tunabishana wenyewe kwa wenyewe kuliko hawa jamaaa...Kuna vitu wanavikosa ndio maana inakuwa hivi

Turudi nyuma kwa tawala zilizopita; wapinzani hawakuanza leo kugandamizwa, kubishiwa, kupuuzwa na hata kuchukuliwa hatua... Vipi walikuwapo hao jamaa? Nini walisema kuhoji mamlaka? Unajua kwanini?

Sasa hili na haya ni ya kwetu, watuachie wenyewe tutajua ni kwa vipi tutamkamata mchawi...

TUFANYE KAZI!!!
Ndg acha kushabikia wauwaji.
Hata kama ni wenzetu ni wauwaji tuu!!
Amepigwa risasi President wa TLS au hukuelewa repurcion yake kimataifa ulidhani watanyamaza ??
 
Hizo pesa wanazotoa ni mikopo hakuna cha bure, vya bure wanavyotoaga ni vyandarua na condom kwa kupitia NGOs zao zinazohamasisha ushoga, na uelewa hili tamko sio la serikali ya UK ni UWAMA wa UK ambao hata hawajui Tanzania ipo Bara gani.

Mikopo? Mpaka sasa nchi yako inadaiwa kiasi gani? Na mmesharudisha kiasi gani exactly? So unakiri nchi yako inaendeshwa kwa fedha za mikopo. Sasa kesho mkikosa kwa kukopa mmejipanga vipi?
 
Mikopo? Mpaka sasa nchi yako inadaiwa kiasi gani? Na mmesharudisha kiasi gani exactly? So unakiri nchi yako inaendeshwa kwa fedha za mikopo. Sasa kesho mkikosa kwa kukopa mmejipanga vipi?
Hata Marekani inakopa China hilo lisikusumbue.
 
definitely,you are one of our best brainwashed and westernised impressive diaspora!!!
Predictably, Magufuli administration's sympathizers, like you, are resorting to "whataboutism". You are not addressing the issue directly. Instead, you are pathetically trying to air your feelings about your perceived crimes of western nations that are rightly pointing out our current administration's failures to protect Tanzanians' safety and human rights.
 
Uhai wa Mtu ni wa thamani. Tuheshimiane kama tunavyoheshimu nafsi zetu! Kitendo cha kumpiga risasi Rais wa Wanasheria wa Tanganyika ni kitendo kibaya sana cha kuwadharau wanasheria wote. Yaani wanasheria hawana maana yoyote! Kibaya zaidi ni kitendo cha kuambiwa waliompiga risasi kinyama hawajulikani. Kivipi? Siku hiyo wapiga tochi hawakuwepo barabarani?CCTV hazikuwa hewani? nk? Tunahitaji kuhakikishiwa usalama na huu ni wajibu wa Serikali kwa mujibu wa katiba ibara ya.....................

MUNGU MKUBWA, Hakuna jiwe litakalobakia juu ya jiwe, kwani wote walioagiza, waliopanga na waliotekeleza kumpiga risasi ili kutaka kumuua Mh. Tundu Lissu woote wataangamia kabisa kabisa katika JINA LA YESU.
 
MKUTANO WA MBOWE NA WAANDISHI WA HABARI UMEACHA MASWALI MENGI:

1. Inakuwaje mnasema ni suala la kitaifa lakini kujua afya yake ni siri na haki ya mgonjwa? Kama ni la Taifa basi Taifa lijulishwe hali yake pia ya kiafya ilivyo kiundani Let's Pray 4 Him

2. Maombi ni kwa Lissu tu, mbona hawakuhimiza kufanya maombi kwa waliokuwa wakiuawa Kibiti au kwa yule Meja Jenerali aliyepigwa risasi? Double Standard ni mbaya sana

3. Mbowe: "Vyombo vya Ulinzi na Usalama ndio suspect namba moja"
Ina maana Mbowe anajua waliompiga risasi? Kuna haja ya Mbowe kuisaidia Polisi maana anaonekana anajua mengi

4. Hizi ni dharau sasa Mbowe anazoonyesha, ina maana vyombo vya ndani havina utaalamu wa kiuchunguzi?

5. Mwanzo Mbowe walituambia wametumia Tsh. Milioni 100 kwa siku 2; Prof. Safari akasema wanatumia Milioni 10 kwa siku; Leo hii Mbowe anasema wametumia Mil 167. Ipi ni kauli sahihi? Naona Wanazidi kujichanganya
Kweli Pesa haijawahi kumwacha Mtu salama

6. Inavyoonyesha Mbowe anaona Serikali ikimtibia Lissu itapata credit, Shame! Chadema wasilete siasa kwenye maisha na uhai wa Watu, Mbowe anaona siasa ni bora kuliko maisha ya Lissu? Let's Pray 4 Him

7. Naona Mbowe hakujipanga kujibu risasi ngapi zimempata Lissu! Kigugumizi cha kutaja risasi ngapi zimempata inatoka wapi? Hili si suala wanalofanya la Kitaifa, mbona kuna ufichwaji wa taarifa sahihi?

8. Mbowe: "Hali ya kiafya ya Lissu ni Confidential lakini anaendelea vizuri" .... Kauli mbili tofauti

Haswaa nilichokiona ni Mbowe kutokwa na jasho jingi mwanzo mwisho. Kiukweli Watanzania wanahitaji kupata taarifa sahihi, kamili na kwa wakati.
 
let's assume statement yako ni ya kweli, Marekani wanaua; kwa hiyo ni sawa na sisi kufanya unyama huo wa kuua watu at will? Kwa sababu tu wana mitazamo tofauti na sisi?

- Kuua ni kuua haijalishi sababu, my point is Wazungu hawana hiyo authority ya kuingilia mambo yetu ya ndani!

le Mutuz
 
Wamalize matatizo yao kwanza, sasa hivi Hawana hata morrow authority yoyote ya kuchangamkia ya wenzao wakati wao, inter Alia, wanandoa za jinsia moja aibuuuuuuuuu
 
- Kuua ni kuua haijalishi sababu, my point is Wazungu hawana hiyo authority ya kuingilia mambo yetu ya ndani!

le Mutuz
Inabidi udefine una maana gani unaposema mambo yenu ya ndani, kama yapi, unaweza kuyataja hapa? Kwenye mikataba ya kimataifa ambayo nchi imeridhia ni lazima ku-comply, mfano right ya mtu kuishi, short of that watakudhibiti, na hutawafanya lolote. Refer madikteta wa dunia hii.
 
Inabidi udefine una maana gani unaposema mambo yenu ya ndani, kama yapi, unaweza kuyataja hapa? Kwenye mikataba ya kimataifa ambayo nchi imeridhia ni lazima ku-comply, mfano right ya mtu kuishi, short of that watakudhibiti, na hutawafanya lolote. Refer madikteta wa dunia hii.

- Sasa Tanzania ni lini tuliingilia mambo ya ndani ya UK au USA? Madikteta huwa hawachaguliwi na wananchi wanajipachika tu madaraka, Tanzania hatujafikia huko poleni sana.

le Mutuz
 
- Sasa Tanzania ni lini tuliingilia mambo ya ndani ya UK au USA? Madikteta huwa hawachaguliwi na wananchi wanajipachika tu madaraka, Tanzania hatujafikia huko poleni sana.

le Mutuz
Kwamba TZ ukaingilie mambo ya ndani ya UK au USA! Serious? Wao wakiwa na interest kwa jambo lolote wataingilia tu na huwafanyi chochote. Hili liko wazi kabisa.
 
Back
Top Bottom