Kukamatwa, kupigwa risasi Lissu: Chama cha Wanasheria Uingereza chamlima barua Rais Magufuli

I knew an international uproar was coming. Matukio ya uvunjifu wa amani na haki za binadamu nchini yamezidi kwa kiwango kinachoishangaza dunia.
Acha uongo dunia haishangai kwa matukio hayo bhana. Watu zaidi ya 20 waliuwawa Kibiti hatukuona barua kama hizi. Wameandika coz jamaa wana maslahi nae, wangekuwa kweli wameguswa na mauaji yanayoendelea hata kwenye hiyo barua yao wangegusia hata kibiti kidogo. Ukitaka kujua haki za binadamu zinakiukwa nenda Burma, Gaza.
 
Mbona huko wenyewe wanauana tena wazi kabisa na hatuoni hizi barua?,kwanini kwa jambo kama hili tuseme ulimwengu ujue kuwa Tanzania si kisiwa cha amani tena?,wangapi wameuawa na kupotea na hatujaona hatua yoyote tokea huko panapoitwa Ulaya?,mbona huko yanafanyika mabaya kuliko hili na wanasema wana amani?,
Tatizo hili suala limechukuliwa kisiasa sana na ikumbukwe hakuna mahali mzungu aliwahi kusema neno isipokuwa ana maslahi hapo au kwa mtu anaesemewa ana maslahi nae;
Wewe si ungesema tu kwa nafsi yako kuwa ".....hili wala haitasaidia kuzuia majaribio ya mauaji ya Magufuli and his government critics kama haya kuendelea ktk Tanzania "

Na kukusaidia tu ni kuwa, dunia hii ya leo ni kijiji mkubwa na wanadamu tunaishi kwa kutegemeana, mataifa yanategemeana, taasisi zinategemeana nk nk....

Taasisi na mataifa kuliona hili hata kulaani, si jambo dogo la kupuuzwa....

Nchi yetu kwa muda mrefu imekuwa na sifa ya kuwa "kisiwa cha amani na upendo", lakini kwa matukio haya ya mauaji ya kinyama hata kupata publicity kubwa nje ya mipaka ya nchi yetu, inatuondolea sifa hii njema ya nchi yetu na kutuweka ktk risk ya kuharibu mahusiano yetu na mataifa mengine na wakati huohuo tukiita wawekezaji eti kuja kuwekeza ktk nchi yetu...

Mwekezaji gani makini anayeweza kwenda kuwekeza ktk nchi ambayo kiusalama si salama?

Unaweza kusema, hili tu la Tundu Lissu ndilo lituchafue?

Jibu ni, NDIYO kwa sbb hata lile limti likubwa liitwalo "mbuyu", lilianza mithiri ya mchicha tu mwisho likakua likawa likubwa kama ulionavyo leo...!!

Kwa maelezo haya, nadhani sasa mimi naweza kujibu swali lako hili....

Kwamba, hii inasaidia sana kwa mataifa mengine pamoja na taasisi za kimataifa kama hii kuujuvya ulimwengu kuwa, Tanzania si kisiwa cha amani tena kama inavyosemwa....

Inasaidia kwa sisi wenyewe kama taifa huru kujichunguza na kujirekebisha kwa kuhakikisha kuwa hali hii inarekebishwa mara moja kwa kuwatia mbaroni watekelezaji wa unyama huu unaolenga kuchafua Image na sifa njema ya taifa hili ya "kisiwa cha amani" na kuhakikisha kuwa hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi yao...

Hili litasidia kwa njia hiyo. Umeelewa?
 
Upuuzi mtupu nimeanza amini Hii ni vita ya kiuchumi lakini kwa upuuzi huu ndio utatufanya tuwe imara zaidi na kubuni mbinu nzuri zaidi za kupaa kiuchumi
Mkianza kumwinywa mbavu mna pa kutokea bora N. Korea wanayo manyuklia wanafurumusha at least dunia inajua wapo na inawajadili. Nyie na ccm yenu sijui mtafanya nini mkiminywa sanasana mtaishia kuwa km Mugabe !
 
Mnaonywa kwani mnaleta kiburi kwa misaada yao, unapoona Mwingireza ameongea, ujue nchi zoote za Ulaya nazo hazitaenda kinyume naye, na Usa lazima naye atatia neno.
Hii siyo dalili njema, mkumbuke Wazungu hutafuta sababu ya kukuletea vikwazo, so hili silo la kubeza labda mpumbavu pekee
Uingerza haijatoa tamko lolote, huo ni upotoshaji au kiinglishi hukijui. Kwani tls wakiwatetea wenzao wa, let say India, ndio itakuwa kauli ya Tz.
 
Mbona huko wenyewe wanauana tena wazi kabisa na hatuoni hizi barua?,kwanini kwa jambo kama hili tuseme ulimwengu ujue kuwa Tanzania si kisiwa cha amani tena?,wangapi wameuawa na kupotea na hatujaona hatua yoyote tokea huko panapoitwa Ulaya?,mbona huko yanafanyika mabaya kuliko hili na wanasema wana amani?,
Tatizo hili suala limechukuliwa kisiasa sana na ikumbukwe hakuna mahali mzungu aliwahi kusema neno isipokuwa ana maslahi hapo au kwa mtu anaesemewa ana maslahi nae;

Nisome tena na tena utanielewa...

Unataka number ya waliouwawa ndiyo akili ikusogee na uamini kuwa Tanzania siyo kisiwa cha amani, siyo?

Uko serious kabisa mkubwa kuuliza swali kama hili??

Nimesema ktk comment yangu uliyoikwoti hapo juu kuwa, hata mbuyu ulianza kama mchicha hadi ukawa mti mkuuubwa kama uunavyo leo...!!

Sasa wewe kama unataka "numbers" ya waliokufa........kalaghabhaho hadi utakapokumbuka shuka la kujifunika wakati huo kutakuwa kumeshakucha..

Halafu unauliza mbona kwao yanafanyika kama haya na huoni barua kama hii?

Looh, wewe sijui unaishi sayari na ulimwengu upi tu....

Huko wenzetu ktk dunia ya kwanza, viongozi wao ama awe Rais, waziri mkuu ama spika hawafanyi ujinga wa ku violate sheria na taratibu za nchi na wakabaki salama na kuendelea na nyadhifa zao kwa raha zao kama hapa Afrika na hususani Tanzania!!

Huna hata kumbukumbu kuwa David Cameron (PM) kabla ya huyu mama aliyepo sasa alilazimika kuachia ngazi baada ya kushindwa ku deliver alichowaahidi wananchi wake. Magufuli anaweza hilo?

Unaweza kusema David Cameron kuachia madaraka yake kabla ya wakati hakukutokana na sababu za mauaji....

Then, kama haya ndiyo mawazo yako, nashawishika kuamini kuwa, huna ufahamu wa kutosha juu ya mambo haya...!!
 
Akili yangu hapa ilipo haipimwi kwa kusogea wala kutetemeka wala njia yeyote iliyo kichwani kwako;,sawa nimekubali hayo 'mawazo yako' kuwa Tanzania sio kisiwa cha amani maana ndivo ulivofikiri na ni haki yako kuwaza hivo,ila nakumbusha tu kuwa lazima tuwe tunajaribu kuwaza zaidi ya uelewa wetu wa kawaida ndio tutapata majibu ya kila swali gumu;
Huwa haifai kuhitimisha lolote kwa jambo lenye msisimko;
Nisome tena na tena utanielewa...

Unataka number ya waliouwawa ndiyo akili ikusogee na uamini kuwa Tanzania siyo kisiwa cha amani, siyo?

Uko serious kabisa mkubwa kuuliza swali kama hili??

Nimesema ktk comment yangu uliyoikwoti hapo juu kuwa, hata mbuyu ulianza kama mchicha hadi ukawa mti mkuuubwa kama uunavyo leo...!!

Sasa wewe kama unataka "numbers" ya waliokufa........kalaghabhaho hadi utakapokumbuka shuka la kujifunika wakati huo kutakuwa kumeshakucha..
 
Impact ya hiyo baruaa ni.....
1.Ummy mwalimu kujitokeza na kujitia unafiki kuwa WaPo tayari mumtibu Lissu,
2.jaji mkuu kujitia unafiki na uzandiki na kuja hadharani na kuongea unafiki....hawa wazungu ni bora watusaidie kuling'oa hili dubwana madarakani utakuwa vyema sanaa
 
Akili yangu hapa ilipo haipimwi kwa kusogea wala kutetemeka wala njia yeyote iliyo kichwani kwako;,sawa nimekubali hayo 'mawazo yako' kuwa Tanzania sio kisiwa cha amani maana ndivo ulivofikiri na ni haki yako kuwaza hivo,ila nakumbusha tu kuwa lazima tuwe tunajaribu kuwaza zaidi ya uelewa wetu wa kawaida ndio tutapata majibu ya kila swali gumu;
Huwa haifai kuhitimisha lolote kwa jambo lenye msisimko;

Haihitaji kuhitimisha lolote kwa "Jambo lenye msisimko"......

Unasisimkwa na jambo gani mkubwa?

Back to the topic...

Hapana, sina hitimisho lolote miye ktk jambo lolote isipokuwa nimetoa maoni yangu tu referring to your comments....

Na kumbuka, huu ni ukumbi wa majadiliano na kubadilishana mawazo...

Hakuna ugomvi, na tuendelee na mjadala
 
Rwanda kila Siku Watu wanapigwa Chuma wakileta U maku maku, Kenya kapigwa Chuma Mkuu wa ICT wa Tume
Kama vikwazo angeanza kuwekewa Kagame!

Ethiopia kuanzia ya Meles Zenawi mpaka ya Sasa Watu wanapigwa Vyuma vya kichwa wakileta Udwanzi the same to Eritrea lakin Maisha yanaendelea!

Huko Africa ya Kati ndio usiseme kwa Ubabe, Wazungu wanajua haya Mambo kwa Africa ni ya kawaida sana sana
Jaribu kufikiria kabla hujaandika,unataka tufanane na Rwanda wanavyouana kikabila au Kenya walivyouana kikabila au central Africa Eritrea etc,usijaribu kujilinganisha na walioshindwa hata siku moja
 
Jaribu kufikiria kabla hujaandika,unataka tufanane na Rwanda wanavyouana kikabila au Kenya walivyouana kikabila au central Africa Eritrea etc,usijaribu kujilinganisha na walioshindwa hata siku moja

Ukiwa unasoma comments soma na comments iliyokuwa 'quoted ' ili ujue Muktadha wa hiyo comments otherwise unaweza usielewe!
 
Lazima uwe taahira hasa kuamini kuwa unaweza kupaa kiuchumi kwa kwenda kinyume na Dunia. Kati ya mambo yanayoweza kukufanya uonekane hopeless kabisa ni pale unaposhindwa kutekeleza hata uliyoyaahidi mwenyewe.

Sisi kama nchi tumetia saini mikataba mbalimbali inayohusiana na maisha ya binadamu, halafu bila aibu tunakiuka. Tunapokumbushwa, kwa wendawazimu mkubwa tunajifanya vichwa maji. Kama nchi tunatakiwa kujitafakari, na kuchukua hatua, ambazo kiuhalisia zinatusaidia sisi wenyewe.

Kwa sasa Tanzania haiwezi kushinda vita yoyote kwa sababu wananchi wamegawanyika. Wapo wanaoshabikia siasa na uongozi wa kibabe na wale wanaounga mkono utawala wa kistaarabu, unaolinda misingi ya utu wa binadamu. Hawa wawili hawawezi kushikamana.
Mkuu wewe upo upande upi? Unashabikia siasa na uongozi wa kibabe au unaunga mkono utawala wa kistaarabu?
Mana nawasiwasi na wewe kipindi cha raisi wa awamu ya nne ulikuwa mmoja wa wale waliokuwa wanadai Tanzania inatakiwa ipate raisi mbabe na dikteta ndo itaendelea..
 
Back
Top Bottom