Kukabiliana na upweke

Nadhani watu wanaitumia upweke wao vyema ndio wanaweza kubuni au kugundua vitu vipya.

Tofauti kabisa na mtu ambaye yuko kijiweni anabishana tu kuhusu mechi ya kesho ya Simba na Yanga.
Nakubaliana nawe. Upweke unaweza kuwa nafasi ya kuichunguza nafsi, kutafakari na kuzaa mawazo mapya. Tofauti haipo kwenye kuwa peke yako, bali kwenye unachokifanya ukiwa peke yako. Hata hivyo, si kila mazungumzo ya kijamii ni kupoteza muda; muhimu ni kuwa na uwiano kati ya kujiburudisha na kujijenga.
 
Katika aina hizo tatu, upweke upi unaongoza kuleta athari au faida kwa binadamu?
 
Katika aina hizo tatu, upweke upi unaongoza kuleta athari kwa binadamu?
Kwa mtazamo wangu, upweke wa kihisia una athari kubwa zaidi, kwa sababu unaweza kuwa na watu wengi wanaokuzunguka lakini ukakosa mtu wa kukuelewa kwa dhati. Kukosa mtu wa kuzungumza naye mambo yaliyo moyoni kunaweza kumchosha mtu kisaikolojia kuliko kuwa peke yake kimwili.
 
Kabisa! Kwa utafiti wangu mdogo nimegundua kuwa watu wanaokaa peke yao mara nyingi hawaendeshwi na mitazamo ya watu wengine (hawaamini kitu kwa sababu kinaungwa mkono na watu wengi).
 
Kabisa! Kwa utafiti wangu mdogo nimegundua kuwa watu wanaokaa peke yao mara nyingi hawaendeshwi na mitazamo ya watu wengine (hawaamini kitu kwa sababu kinaungwa mkono na watu wengi).
Umegusa jambo la msingi sana. Wakati mwingine kuwa peke yako kunakupa nafasi ya kufikiri kwa uhuru, kuhoji mambo na kujenga msimamo wako bila kushinikizwa na wengi. Si kila anayekwenda na wengi anaamini wanachoamini, na si kila anayesimama peke yake amepotea. Muhimu ni kuwa na sababu za kuamini unachoamini, si kupinga au kukubali kwa sababu tu ya idadi.
 
Na zipi faida za upweke?
Faida kubwa ya upweke ni kukupa nafasi ya kujitambua, kufikiri kwa kina na kufanya maamuzi bila presha ya watu. Unajifunza kujitegemea kihisia, kukuza ubunifu na kutofautisha unachotaka wewe na kile ambacho jamii inataka uamini. Lakini upweke una faida pale unapouchagua kwa kujijenga, si pale unapogeuka gereza linalokutenga na dunia.
 
Kabisa mkuu.
 
Huo tunauita upweke wa kiutafiti.

Je, unawaelezea vipi wale watu wapweke wanaoutumia huo upweke kupiga nyeto? 😹
 
Upweke ni hisia hasi zinazotokana na utofauti kati ya maisha ya kijamii uliyonayo na yale unayotamani.
 
Upweke ni nini kwa mtazamo wako?
Kwa mtazamo wangu, upweke ni hisia ya kukosa uhusiano wa maana—hali ya kutotambuliwa, kutosikilizwa au kutokuwa karibu kihisia na wengine kwa namna unayoihitaj.

Upweke unaweza kuwa tofauti kwa kila mtu kulingana na mahitaji yake, mahusiano yake na mazingira anayopitia.

Kuwa peke yako kimwili si sawa na kujihisi mpweke.

Mtu anaweza kukaa peke yake na akahisi utulivu, uhuru na ukamilifu; mwingine anaweza kuwa katikati ya familia, marafiki au wafanyakazi wenzake lakini bado akahisi kuwa hakuna anayemwelewa kwa undani.
 
Kwahiyo mtu akitamani kuwa tajiri huku maisha yake ya kijamii hayamruhusu ni UPWEKE?
Upweke unahusu social connection. Mfano mtu anayehitaji mpenzi lakini anakosa.

Pesa ni jambo dogo sana. Sio kila tatizo la kijamii linatatulika kwa pesa.
 
Ukijua kutumia muda wako vizuri huwezi kuwa mpweke.

Kwa mfano
. ukaweka muda wa kufanya kazi
. ukaweka muda wa kupumzika
. kufanya mazoezi
. kujifunza mafundisho mbalimbali
.ukaweka muda wa kufanya meditation

Kila dakika kwako ikiwa na maana upweke utausikia tu ni matatizo ya watu wengine.

Upweke ni matokeo ya kushindwa kujua ufanye nini na muda wako.

Hekima ana ongea mwenyewe kwani alikuwepo kabla watu hawajazaliwa

Naye ni jibu katika kila jambo.
 
Kwanini upweke uwe kwenye mapenzi na sio pesa?

Je, pesa haiwezi kutatua tatizo la kimapenzi?
Upweke ni social issue. Lazima uhusu mahusiano na watu kwanza.

Yatakuwepo matatizo yanayotatulika na pesa, ila naamini ni machache yanayotatuliwa na pesa pekee.

Pesa ni kipimo cha thamani ya bidhaa/huduma, ukiihusisha na thamani ya mtu unaharibu kuliko kujenga.
 
Nimeipenda hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…