Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 710
- 1,163
Katika utumishi wa umma huwa tunaelekezwa kuzingatia maslahi ya umma katika kutekeleza majukumu yetu.
Utashi huu ni muhimu kwasababu pamoja na kuchochea ufanisi, ubora wa huduma kwa wateja na mahusiano mema mahali pa kazi, husaidia kujenga taswila chanya ya taasisi zetu pamoja na serikali kwa ujumla.
Sina uhakika kama tathmini sahihi huwa inafanyika haswa katika kukabiliana na wananchi wenye mwelekeo wa kuipinga serikali. Wenye dhamana na masuala hayo wakati mwingine wanatuachia maswali kama wanazingatia maslahi ya umma katika utekelezaji wa majukumu yao.
Nadhani tuna kila sababu ya kwenda kujifunza, haswa kwa mzee wetu Rais Kikwete maadam yupo hai. Katika uongozi wake huyu mzee alisemwa sana, lakini hatukusikia makesi yenye ukakasi. Pamoja na mapungufu ya hapa na pale waliowengi wanakubali kuwa kwenye demokrasia alifanya vizuri.
Natamani ifike mahala tuachane na kesi ambazo zinaichafua demokrasia na uhuru wa watu kutoa mawazo katika nchi yetu.