Kujifukiza kiholela kutaleta athari kubwa baada ya Covid 19: Wizara ya Afya itupe mwongozo wa mchanganyiko sahihi haraka

Nyaka-One

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
4,315
5,985
Kwenye kipindi hiki cha covid 19 kumekuweko na shuhuda na maelezo mbalimbali kuhusu aina za michanganyiko ya viungo, majani au mitishamba ya kutumia kwa kunywa au kujifukiza na wakati mwingine maelezo yamekuwa yakipishana. Michanganyiko ambayo imekuwa ikitajwa sana na wengi inajumuisha vitu kama tangawizi, karafuu, kashwagara majani ya mwembe, majani ya mpera, muarobaini, mchaichai, limau, ndimu, mikaratusi na vingine vingi tu.

Madhali rais wetu na waziri wa afya wameshatoa kauli za kuwahimiza watu wasikimbilie kwenda hospitali na badala yake wabakie majumbani na kujifukiza na kauli hizo kupokelewa vizuri na wananchi ni wazi kwamba wale waliokuwa wakipinga ufukizaji hoja yao imeshindwa kihalali.

Hata hivyo baada ya wananchi kuchangamkia ufukizaji kama njia ya kuzuia au kutibu covid 19 kumekuwepo na maelezo yanayotolewa na wanaoonekana kuwa wataalamu na wazoefu huku kwa kiasi fulani yakiwa yanapingana au kutofautiana kwa kiasi kikubwa.

Mfano wakati watu wengine wamekuwa wakituma shuhuda mbalimbali kwenye social media wakidai kupona au kusaidia wengine kupona kwa kuchanganya pamoja idadi kubwa ya hivyo viungo, majani au mitishamba na kuvitumia kwa muda fulani na mara kadhaa ndani ya kipindi fulani (siku au wiki) jana kuna mtaalamu wa mitishamba kutoka wizara ya afya kadai pamoja na kufaa kwa ufukizaji lakini idadi ya vitu vya kuchanganya ili kujifukiza haipaswi kuzidi vitu vitatu na kwamba vikizidi hapo vitapunguza nguvu ya dawa na hata kuwa na athari za kiafya.

Hivyo kwa maoni yangu kwa vile covid 19 ni tishio kubwa na watu wanazidi kujifukiza kila kukicha bila kujua usahihi wa michanganyiko hiyo ambayo kila mmoja anaambiwa na kuamini kivyake wizara ya afya ingechukua hatua za haraka sana ili kuratibu utambuzi wa mchanganyiko au michanganyiko iliyo sahihi wa vitu hivyo vinavyofaa kuchanganywa na kutumika kwa pamoja pasipo kuleta athari yoyote kiafya kwa wanaojifukiza.

Wizara inaweza kutoa options zaidi ya moja ili iwe rahisi kwa wananchi kujichagulia option mojawapo ya mchanganyiko ambao majani au vichanganyishio vyake vinapatikana kirahisi katika mazingira anayoishi. Hili la kila mtu kutoa idadi yake na aina ya vitu vya kuchanganya ili kujifukiza na pia muda tofauti wa kujifukiza likiachwa liendelee kufanyika kiholela bila ya wizara kutoa mwongozo wowote linaweza kutuachia madhara makubwa kama taifa baada ya covid 19 kuondoka.
 
Dozi kwa umri
Ingredients
Nyuzi joto za kuchemsha
Muda wa kujifukiza na how
..........
.........
Najaribu kuwaza manake hata mimi sina majibu sahihi
Nami nasubiri wataalamu waje.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taifa sasa limekuwa na waganga wa kienyeji badala ya wataalamu wa afya. INASIKITISHA SANA.

kama hujaelewa soma comments.
 
Wanaume wa Dar acheni uoga, kujifukiza huku mikoani tumekuwa tukifukizwa tangu tuna miaka 5 nashangaa na bado tunadunda ... Nyie kujifukiza muaroaini mmeamua kukimbilia kufungua nyuzi ....


Shame on you.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wadaslam wana matatizo hawa!kwa hiyo hamjui" nyungu," aka" ikibhira"!
Acheni zenu bana hii tiba ipo kitambo hata bibi alinifundisha kutibu homa kihivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom