Kujenga nyumba na kununua magari ni sababu mojawapo ya Umasikini

Yote kwa yote maisha hayana formula. sometimes philosophy tunazotumia haziendani na context ya mazingira yetu. kumwambia mmbongo anaye anza maisha huenda ameajiriwa eti afanye biashara badala ya kujenga nyumba anaweza akakushangaa. Kwa mazingira yetu biashara zina misukosuko mingi. 1. Kuna kufilisika. 2. kuna kutapeliwa 3. Kuna kukosa soko la bidhaa 4. Fitina etc. Japo kufanya biashara kwanza halafu akaanza kujenga ni vizuri zaidi, lakini ni ngumu kueleweka. Yote kwa yote kila mtu afanye jambo analoona ni sahihi, tutakutana mbele ya safari
 
Habari,

"Tafuta kiwanja, Jenga, Oa/Olewa, nunua mkoko", njia hii na mawazo haya yamekuwa kwa vijana wengi wanaoanza maisha, hususani waliobarikiwa kupata ajira au biashara zao binafsi ambazo zinawapa kipato flani cha kuendesha maisha yao. Kwa uzoefu wangu hii imekuwa kati ya sababu moja kubwa zinazosababisha watu kuwa maskini na kushindwa kufikia uhuru wa kifedha.

Lakini tujiulize swali la msingi, kwanini watu wengi wameamua kuchagua njia hii ya maisha. Nimefanikiwa kuwahoji watu wengi kidogo kuhusu hili na majibu niliyoyapata mengi yalikuwa kama ifuatavyo:

  • Gharama ya kupanga nyumba ziko juu sana, ni bora kujenga ya kwako.
  • Nyumba ni asset.
  • Usafiri ni shida sana eneo niliko jenga ni bora kuvuta gari yangu.
  • Mama/baba mwenye nyumba ana gubu sana.
  • Nikiwa na kwangu nakuwa na uhuru mkubwa sana.
  • Siku nikifukuzwa kazi au biashara ikiyumba nibaki na pakulala na familia yangu.

Sababu hapo juu nyingi ni za maana kabisa ila tatizo ni kwamba njia zilizotumika kutatua hizo changamoto zinaongeza changamoto zaidi, kivipi?. Ngoja tujadili mambo machache kuhusiana na maisha ya watu wengi hususani mijini (e.g. Dar):

- Wengi wananunua viwanja maeneo ya mbali kutoka mahali wanapofanyia shughuli zao zinazowapa kipato.
- Baadhi ya hayo maeneo yana changamoto za miundombinu ya maji, umeme, barabara na hata kiusalama.
  • Wengi wanajenga kwa kuunga unga sana, unaweza jenga nyumba hata miaka sita au zaidi. Kuna msemo wanasema "nyumba haiishi".
  • Nyumba nyingi wanazojenga watu kukaa zinakuwa ni kubwa na za kifahari bila kukumbuka lengo la mwanzo lilikuwa ni makazi tu na sio jengo la maonesho (Hapo utajibiwa kuwa tunajenga mara moja ya kuzeekea)

Kuzingatia hizo hoja hapo juu, yafuatayo yanakuwa ni matokeo ya gharama za maisha baada ya huyu mtu kuhamia kwake:

  • Gharama za usafiri au mafuta zinakuwa juu ukilinganisha na awali.
  • Mazingira yanakuwa sio rafiki kwa familia kuishi, maana nyumba nyingi zinakuwa bado hazijaisha (Wengine wanasema unakuwa unaishi site).
  • Kama una gari, gharama za matengenezo zinakuwa juu kwa sababu ya pengine barabara kuwa mbaya, lakini kwa kuwa unasafiri umbali mrefu kila siku, basi hata service ya gari utafanya mara nyingi zaidi.
  • Pia kama una gari utalazimika kuendesha gari umbali mrefu kila siku, hii si nzuri kwako kiafya.
  • Gharama za umeme na maji pia zinaweza kuongezeka kwa kuwa nyumba ni kubwa sasa na pengine maji hayajafika.
  • Maeneo mengine hata watu hawajahamia wengi hivyo hata usalama unakuwa hatarini.
  • Mara nyingi unaweza ukajikuta mbali na huduma bora za kijamii ikiwemo hospitali, shule, n.k.

***NOTE: Gharama zinaweza kuongezeka ukilinganisha na mwanzo.

Kwanini kuna hofu ya kuwekeza hizo pesa?

Tujiulize swali hili la msingi. Ni kweli baadhi ya watu wanatamani sana kuffanya biashara, lakini wengi wanasema, BIASHARA HAZITABIRIKI. Ni kweli kabisa, lakini ukweli ni kwamba hilo sio tatizo la watu kutokuwekeza.
SHIDA KUBWA NI WATU KUTOKUWA NA ELIMU YA FEDHA. Hili ni jambo la muhimu sana kwa vijana kupata elimu. kwanza kabisa sio kweli kwamba ukitaka kuwekeza ni lazima ukafanye biashara fulani kama kuuza nguo, vinywaji au duka la mangi. Unaweza ukafanya uwekezaji kwa njia nyingi sana ambazo hazitahitaji your active time kuweza kusimamia ila mwisho wa siku ukaja kuwa na uchumi mkubwa kabisa. Uwekezaji huu ni kama mifano ifuatayo:

  • Kununua viwanja na mashamba (Kumba muda unavyokwenda ardhi inapanda thamani lakini nyumba inashuka thamani)
  • Kununua hisa za makampuni
  • Tressury Bonds and Bills
  • Mifuko ya uwekezaji ya pamoja (e.g. UTTAMIS)
  • Fixed deposits accounts
  • Kuwekeza kwenye elimu (Hii sio lazima zile za darasani, inaweza kuwa hata kujiendeleza katika fani flani)
  • N.k.

La muhimu ni kupata elimu sahihi ya mambo ya fedha ili ujue jinsi ya kufanya maamuzi ni vipi utumie pesa yako.


Ngoja nitoe mfano halisi mmoja ulio hai kabisa kwa lengo la kupata uhalisia wa ninacho kisema:

Mwaka 2013 niliajiriwa mahali na tulikuwa kama waajiriwa sita wapya katika hiyo kampuni, mwenzetu mmoja alikuwa na uelewa mkubwa sana wa mambo ya fedha, na mara nyingi alikuwa anatushauri kuhusu haya mambo lakini tulikuwa tunamuona kama kachanganyikiwa: Mimi na wenzangu wengine wa tano tulikwenda mahali tukanunua viwanja na kuanza kujenga kwa kasi sana na badae tukachuku na mikopo kuongeza kasi hiyo. Kwa haraka haraka kwa wastani tuliweza kutenga kama milioni moja kwa mwezi kila mmoja wetu kwa ajiri ya miradi ya ujenzi. Mungu si athumani baada ya miaka mitatu paka minne wote watano tukawa tumehamia kwenye site zetu huku tukiendelea na finishing.

Jamaa alikuwa kila mwezi anaweka milioni moja kwenye mfuko mmoja wa uwekezaji wa pamoja na alikuwa anapata average interest kama ya 11.85% kwa mwaka. Badae akawa ananunua na bond za serikali pamoja na mambo ya kununua mashamba mbali kidogo na mji yakichangamka anakata na kuyauza. Kiufupi jamaa ana zaidi ya milioni 200 kwenye mfuko anaoweka pesa pamoja na kuwa na asset ya viwanja na mashamba na benki ana pesa chafu.

Turudi kwetu tuliojenga na sasa tuna mikoko yetu, umbali wa kwenda na kurudi nyumbani ni 50 Km kila siku. Na pia siwezi pata picha ile hofu ya kwamba nikiachishwa kazi bado ipo maana siwezi nikala nyumba.

Kwa ajili ya muda niishie hapa kwa leo, nipate mawazo ya watu wengine pia. Kiufupi mimi naona kuna mitaji mingi ya biashara na uwekezaji inapotea kwa huu mwamvuli wa kujenga na kununua hii mikoko.

Ahsanteni!!!
Sawaaa. Siye tutajenga na kununuwa magari. WEWE WEKEZA KWENYE HISA, SIJUWI KITU GANI HUKO, FAINALI UZEENI...
 
Tatizo ni pale mnadhani utajiri ni kwa kila mtu, wengine ni savaiva tukipumua tu inatosha.
 
Nimekuelewa mtoa maada, lakini acha ninunue hata ka IST kwanza , jana nimepigwa na jua hatari , leo wakati natoka home naenda town nimevaa raba kali sana. Nimekanyagwa kwenye daladala nimefika nimechafuka kinoma, acha ninunue ka usafiri kwanza mengine yatafuata, nimechoka kutembea kwa miguu kama ng'ombe
 
Huko kote ukiwekeza hizo Hela utakazopata utazipeleka wapi!? Kama sio kwenye kujenga.!?

Wako waliojenga kwanza Kisha wakawekeza na wanaofata hio theory Yako.

Binafsi Nina nyumba ya kupangisha ila Sina ya kuishi bado naishi magetoni.

Ni uamuzi tu.
 
Nimenunua Tressury Bonds, na nimewekeza mfuko wa uwekezaji (UTTAMIS) faida milioni 1 na laki nne kila mwezi bado nipo kazini mshahara unalipa kodi ya nyumba nilikopanga, mafuta ya gari, vocha na chakula na hii faida ninayopata kwenye uwekezaji ndio naipeleka kujenga sina presha yaani maisha murua kabisa.
mkuu samahani ili upate hiyo faida ni lazime uweke hela kuanzia sh ngapi
 
"Tafuta kiwanja, Jenga, Oa/Olewa, nunua mkoko",......hii huwa naiita AFRICAN MATRIX....na Watoto wetu nao wata ambiwa hivyo hivyo....😞
 
Inategemea sana na investment unayofanya, kama unafuga kuku, au unalima au duka la nguo, vipodozi nk, ninaweza kukuelewa kama utafanya biashara kabla ya ndinga. Kama wewe ni hustler mwanasheria, au Software Engineer sijui IT baada ya kuzunguka sana na project zako utakuja kugundua waTz perception yetu kwa mtu anayemiliki gari ni tofauti sana...Unaweza kutengeneza pesa nyingi sana, ukawa na network ya watu wengi wakubwa na ukakopesheka na kuaminika ukiwa na gari kuliko ukishuka kwenye daladala...

Mimi nilikua naenda ofisi kwa ofisi kwa miguu kumarket software solution zangu ila nilikua natumia nguvu kubwa sana kumwaminisha mtu, na bado walikua wanalipa ela ndogo sana na bado usumbufu ni kama wote yani...

Ninachosema, baadhi ya fields gari ni selemu ya investment...
Hata ukiwa unafanya interview, ukienda na gari una nguvu ya kunegotiate mshahara mkubwa zaidi
 
Back
Top Bottom