Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,280
Una familia ya watoto wanne, umefanikiwa kimaisha watoto wanasoma na unajenga nyumba ya ghorofa vyumba 12 vya kulala.
Kwanza gharama za ujenzi ni kubwa, baada ya ujenzi kutunza nyumba ya vyumba 12 ni gharama kubwa sana. Hata ukiwa na mawazo ya familia kukutana watoto wanne wenye mafanikio si mara nyingi watakuwa nyumbani.
Nyumba ya vyumba vinne mpaka sita inatosha, pembeni unaweza kuweka houseboy quarter na guest wing.
Ukiwa mzee wewe na mke wako au mume wako kuishi kwenye nyumba ya vyumba 12 wakati watoto wote wana miji yao nayo ni gharama,