Kuishi Mbezi Kimara ni laana?

Kuishi Mbezi Kimara ni laana?

kupinga ni kawaida,hata great thinkers wakwanza walipingwa na waliofuatia.
 
Umeona eh yaani roho kwatu! Ila ukiwa na gari yako katisha ya Goba au Kinyerezi/Segerea.

ni kweli Mama Joe ingawa hizo njia za mkato sasa hivi na mvua hii nazo zitakuwa kerooo.
 
Last edited by a moderator:
Aheee hii ilinikuta mwaka jana nilibaki hoi, halafu vile vilima wakati wa mvua sio salama kabisa. Nashangaa kwanini hawaiweki lami na ruti za daladala ndo wajenge hii ya Morogoro kama walivyofanya ya mbezi beach chini / Africana. Inarudisha nyuma watu biashara zinakufa cost inakuwa kubwa mno.
Huko nako uwe tayari kubadilisha shock ups na mabushi kabla ya muda.siyo suluhisho.
 
Pole sana mkuu, mie nlishaona hii barabara hata ikikamilika haitaleta suluhisho la muda mrefu. Huu ni ujinga wa wanasiasa kujifanya wataalam na kibaya wataalam wanaongozwa na wanasiasa.
Upo sawa kabisa, lakini mtakoma, si mnalala sana. Kidumu hoyee
 
Huko nako uwe tayari kubadilisha shock ups na mabushi kabla ya muda.siyo suluhisho.

Wote sio mafisadi kama yeye. Magari tutayapata wapi, mafuta tutelage wapi, maintanance, tunarudi nyuma tunarnda mbele. Huyo naye ni wale wale tu ndugu yangu
 
Mndengereko nakuunga mkono hawa jamaa wamepunguza sana spid ya kaz na ukiangalia unagundua hawa jamaa wanapuuza sana tabu mateso na kero tunazopata wakaz wa mbez kimara. Ifike mahal serrkal yetu ifumbue macho itizame na kutatua kero hii.
 
Kusema laana siyo sahihi.....

Ubinafsi wa wanasiasa ndo unatufikisha hapa.......

.ila pamoja na hiyo foleni siwezi hama mbezi.....hata niwe nafika saa tisa usiku nyumbani...
 
Jamani hamieni kigamboni hakuna shida ya foleni .
 
Tuwe wavumilivu hiyo taabu itakwisha na tutasahau! Mambo mazuri hayataki haraka! Tupo ktk mpito

We mzima kweli? Je unaishi maeneo haya ya Mbezi Kimara au unachangia mada tu?? Nikuulize swali la kizushi tu...mtu anayeishi upande wa TRA Baruti Au anayetoka Kibaha na gari anaweza vipi kufika upande wa Korogwe kwa Thomas Lyimo? Au mwenye gari anayetoka Kimara Mwisho anapata wapi huduma ya kuuziwa mafuta kwa maana ya Petrol station? !!? Samahani watu tunaumia na kuteseka halafu unaleta mizaha....sio poa hata kdgo.
 
Swali lingine la kujiuliza kulikuwa na haja gani ya kuweka zile kona kali km za kitonga pale kimara mwisho..hadi sasa scania mbili zimeshaanguka na kuua..strabag wanafunga barabara ovyo wanaongeza foleni ovyo

Ile kona aisee ni janga sana.....Mungu atusimamie tu pale mana sijajua madhumuni ya a wajenzi ya kuweka ile kona ni nini....
 
Jamani hamieni kigamboni hakuna shida ya foleni .

Ah tutahama na nyumba zetu...?

Pantoni lenyewe janga pia...kuna siku nilishuhudia linaelekea ule upande zinazopaki boti za zanzibar......kwa ujumla nchi yetu iko hovyo kwenye swala la usafiri...
 
Jana nlikuwa namrudisha mke wa mtu kwao mbezi, c unajua wachaga wako bize na hela cc twala. Nimetoka ubungo saa 10 nimefika temboni saa 1:30 jioni, kurudi ubungo nimefika saa 4:30 usiku, sirogwi tena kuja mbezi, khaaa
 
Ah tutahama na nyumba zetu...?

Pantoni lenyewe janga pia...kuna siku nilishuhudia linaelekea ule upande zinazopaki boti za zanzibar......kwa ujumla nchi yetu iko hovyo kwenye swala la usafiri...
Wanajenga daraja sasa hivi kwa hiyo baada ya daraja kuisha mambo yatakua mazuri. Tatizo kila kitu wamesiasisha ndio maana miundo mbinu itabaki kuwa janga la kitaifa .
 
kimara ni majanga umeme unakatika katika ovyo,maji hamna,usafiri tabu kwakweli.kimara ni balaaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom