UDART vipi mnasitisha huduma saa nne usiku stendi ya Mbezi?

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
5,472
2,000
Jana abiria tuliotoka mikoani tulioshuka mida ya saa nne usiku pale stendi kuu ya Magufuli tulipigwa na butwaa pale usafiri tulioutegemea kututoa huko kutusogeza mjini ukikosekana!

Tulitoka stendi ya Magufuli tukajikongoja na mizigo na wengine wakiwa na watoto wadogo kufika mbezi stendi tukakuta vibanda vya tiketi vya gari za mwendokasi vikiwa vimefungwa.

Bahati nzuri likaja basi moja bombardier la UDART likashusha, dereva baada ya kushusha akawa anafunga vioo vya gari zima, tukamuomba atuchukue kutusaidia usafiri akakataa katakata, akisema watu wa tiketi wameshafunga hivyo huduma pale hakuna kama tunaweza tuifuate huduma hiyo Kimara mwisho kwamba kule bado wanatoa huduma kwa muda huo.

Swali la kuwauliza UDART, hivi nyie si ni watoa huduma kama wale wa Pantoni Ferry Kigamboni?

Stendi kuu imehania mwisho wa mji, hapa nyie mlikua na jukumu la kuhakikisha mnasaidia wasafiri waliotoka ma elfu ya kilometa kufika makwao, matokeo yake saa tatu saa nne mshafunga dirisha za ticket, mnategemea watu wafike vipi makwao?

Udart nyie ni watoa huduma na si kama waalimu ambao saa 8 mchana wanarudi majumbani kwao kupumzika

Niiombe serikali kupitia Tamisemi waangalie mapungufu haya ikibidi kituo cha mbezi mwisho huduma za Udart ziwepo at least hadi saa saba usiku au saa nane kwa maana stendi ya Magufuli ni kituo kikubwa kinachopokea mabasi toka ndani na nje ya nchi, panalazimika pawe na link ya uhakika kati yake na kituo cha Mbezi mwisho. Mbona ferry huduma za kuvuka ni 24hrs?

Dubai kuna usafiri wa tax na mabasi ya Serikali ya kwenda Airport 24hrs .7 days a week!

Halafu tunashangaa vipi wenzetu walivyoendelea wakati sisi tunalala saa mbili usiku.
 

maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
9,394
2,000
Naamini mkurugenzi mpya aliyetoka TRA ni mchapakazi na atalifanyia kazi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom