Kuishi kwa Shemeji!

Kuna wanaume huwa wanaenda mbali wanatafuna wadogo wa mke wake kwa kigezo amawaoa pamoja na dada yao na anawalisha na kuwavalisha wao ni kunya tu.

...dahhh, incest, taboo au nini hii?...
 
Wakuu!

Kwa familia za kiAfrika tuna tabia za ndugu wa kutoka kwa mke na kwa mume kuishi na familia fulani, hasa wanapokuwa katika hali ya kutafuta misaada au kuugua.

Je inakuwaje pale mke na mume wanapokorofishana na kufikia hatua ya mke kufunga virago kurudi kwao...Je ndugu wa upande wa kike wanaondoka au hubaki?..chukulia kuwa hao ndugu si sehemu ya mgogoro wa familia husika, na hawajawahi kushabikia upande wowote!

Chanzo cha mgogoro lazima kiondoshwe!
 
Husninyo,
Ni jambo jema Mwanamke kujiandaa, na kama ana uwezo ni njema akijenga kwao...lakini shida moja ya maendeleo ya aina hii ni kwamba Mwanamke wa aina hii anakuwa na kiburi sana, naanatumia umiliki wa nyumba kama kichaka cha kumtishia mume na kutomheshimu!

pj mwanamke wa hivyo huwa na ujasiri na wanaume mnaogopa wanawake wajasiri maana mnashindwa kuwapelekesha mnavyotaka. Mwanamke wa hivyo akikosana na mumewe kidogo huonekana ana jeuri sababu ana nyumba wakati hata kama asingekuwa na nyumba migogoro pia ingeweza kutoke.
 
Huo nimtihani mkubwa sana, maana siku akishushiwa kipondo sijui unaingilia kuamulia au au unaugulia pembeni dada akipigwa....!

Mtambuzi Heshima kwako,

hili jambo linahitaji uangalifu wa hali ya juu, mie kila siku napinga SANA hii kitu, unakuta baba jitu zima na kazi linafanya linang'ang'ania kwa dada yake aliyeolewa, mimi nasema hivi kwa kuwa nimekutana nayo, mke anapokosea na ukamgombeza kwa sauti au kushusha kipondo(Mungu epusha) sijui kaka mtu anajisikiaje ukizingatia ni mwanaume kama wewe, nafikiri rohoni huwa wanatamani kuingilia lakini roho inawasuta kuwa itakuwa ndio passport ya kuondolewa
Nina mfano wa Dada na kaka wa tumbo moja, mvulana akiwa ndo mkubwa, na wote wamepata majiko.
Kaka mtu alishindwana na mkewe, na baada ya kuona maji yanazidi unga aliamua kuondoka na kwenda kuishi kwa mdogo wake wa kike ambaye ameolewa, so akawa anaishi kwa shemejie!
Hakika situation hiyo ilikuwa ngumu mno, ambapo watu wa nje waliona haiwezekani, wakaenda kumbeleza mwanamke yule ili arudishe moyo, akatoa masharti mazito na hatimaye akamruhusu mumewe kurudi kwake!...aisee!
 
Nawa ombeeni woote wana JF isiwakute situation cumbersome kama hiyo.

Ni fedheha kubwa sana kuishi kwa dada alipo olewa. Hasa kwenye manyumba yetu ya kibongo. Dada akishughulikiwa, wewe unasikiliza. Looooo!!!!!
HAIWEZEKANI!!!!!!!!!!!
Doctorz,
Sijui una maana gani hapa, sijakuelewa!
 
Kuna wanaume huwa wanaenda mbali wanatafuna wadogo wa mke wake kwa kigezo amawaoa pamoja na dada yao na anawalisha na kuwavalisha wao ni kunya tu.
Hii ni wazi kabisa, nina mfano Live!
Muulizeni Jamaa aliyepata kuwa kigogo wa cdm mkoa wa mbeya, lakini baadaye akahongwa na gambaz na kutangaza kukihama chama!...yeye anajua zaidi hii makitu inavyofanyika!
 
haiko clear sana hii mada yako Mkuu, kuna vitu vingi sana unatakiwa kuvifafanua unapozungumzia kufungasha virago
Mokoyo,
Umeelewa sana wharamsey!...na wewe tena kule kwenu wanaume ndio wanaofungasha virago kwa jeuri ya wanawake!
Najua unajua sana hizi situations, lakini sema huna point za kujibu!
 
Ndugu wote wa mke nao inabidi wafunge virago. Watabakije hapo, kwa misingi ipi? Nani atawahudumia?
Lakini kuna ugomvi serious wa familia ambao hata mtoto au mtu mzima aliyeko ndani humo hatosikia wala kustukia kitu, ila chumbani ni moto unawaka!
Wakitoka sebuleni wanasalimia vizuri, na kila mtu anawahi kunako mkoloni!
Na inafikia siku wanashindwana, mama anaamua kuondoka, anapack baadhi ya vitu vyake taratibu, na anaondoka, mashemeji wanashangaa tu, huku akiwaaga kuwa anaenda mahala kusalimia, kumbe yamemshinda!
Na unawezakuta baba naye ana aina fulani ya ustaarabu, ataendlea kushi vizuri tu na mashemeji zake, na kila kitu anawapa, pamoja na ada!
All in all ugomvi kwenye familia ni mbaya sana, kwa mtu mwadilifu dawa ni kuondoa tofauti haraka iwezekanavyo!
 
pj mwanamke wa hivyo huwa na ujasiri na wanaume mnaogopa wanawake wajasiri maana mnashindwa kuwapelekesha mnavyotaka. Mwanamke wa hivyo akikosana na mumewe kidogo huonekana ana jeuri sababu ana nyumba wakati hata kama asingekuwa na nyumba migogoro pia ingeweza kutoke.
Mwanamke akiwa jasiri sana hafai kwa matumizi ya kawaida ya nyumbani!...nadhani wanaume wengi wataniunga mkono.
 
pia maranyingi huwa tunasema kama unamapenzi ya dhati basi utapenda familia nzima na sio mmoja, so kuachana na mmoja sio maana kuichukia familia nzima. kumbuka UDUGU NI KUFAANA NA SIO KUFANANA.

Kuipenda familia nzima sio ndio maana yake waje wajazane kwako. Haya ndio yanaleta migogoro kwenye ndoa zetu. Uswahili huu ukiendekezwa mtaendelea kuwa na mizozo maisha yote.
 
Wakuu!

Kwa familia za kiAfrika tuna tabia za ndugu wa kutoka kwa mke na kwa mume kuishi na familia fulani, hasa wanapokuwa katika hali ya kutafuta misaada au kuugua.

Je inakuwaje pale mke na mume wanapokorofishana na kufikia hatua ya mke kufunga virago kurudi kwao...Je ndugu wa upande wa kike wanaondoka au hubaki?..chukulia kuwa hao ndugu si sehemu ya mgogoro wa familia husika, na hawajawahi kushabikia upande wowote!

Dah.! ni ngumu sana lakini kama huna jinsi itabidi uvumilie tu utimize malengo yako......ila kuna jamaa alikua anaishi na shemeji yake....siku moja shemeji kamto out kwenda kupata kinywaji kidogo......walifika baa jamaa akaagiza kili,...shemeji akamwambia....aaaah shem jaribu kunywa Gordon....ukinywa hiii unapiga mashine usiku kucha...ngoma hailali.
 
H a ha haaa!
Shemeji gani huyo wa kuongea naye maongezi ya jinsi hiyo?
Lakini inawezekana.
Kuna jamaa alipata kazi hapa A Town, akaacha familia yake Dar akaja akawa anaishi kibachela kwa mdogo wa mkewe wa kiume.
Ajabu dogo akawa anamwambia shemeji yake..."shem huyu demu wa chumba cha tatu we piga tu bana, mbona anakumaind hivyo?"
 
ndugu yangu mimi hapa kwangu wapo wadogo zake mke wangu watatu wakiume moja anasoma masters mwingine mwaka wa 3. afu huyo mwingine form 5 wanachumba chao washaweka kila kitu hadi tv yani hapa ni mawazo maana bila hata aibu wananiambia na matumizi yao kama laptop mimi ndo naghalamika hata chuo mimi ndo niwapeleke sijui hata nifanyeje
 
1. Wazazi wao wako hai?
2. Kama wapo hai wana uwezo wa kuwahudumia?
3. Wa masters hafanyi kazi? Kama anafanya kwa nini yupo hapo?
4. Kuwahudumia si lazima ni hiari, kumbuka hata msaada unaowapi sio wajibu wako, ni hiari...wasiigeuze hiari kuwa lazima
 
mkuu wazazi wao wako hai kabisa na hata kama hawana uwezo wa kuwahudumia hao jamaa wanamkopo wa serikali wote hawafanyi kazi na hapa kuwahudumia washafanya lazima maana usipowapa walichokuomba siku hiyo huko ndani hakulaliki yani hawana mpango wa kuhama washaweka tv na makochi yao kwenye vyumba nilivyowapa sasa watoto wangu wanalala kwa shida sasa hivi
 
Back
Top Bottom