Kuishi kwa Shemeji!

Mnakumbukaga extended family Tanzania ilianzaga kwenye sera ya ujamaa miaka hiyo.
 
Pole sana! Mueleze mkeo hili tatizo anaweza akalipatia ufumbuzi!
ndugu yangu mimi hapa kwangu wapo wadogo zake mke wangu watatu wakiume moja anasoma masters mwingine mwaka wa 3. afu huyo mwingine form 5 wanachumba chao washaweka kila kitu hadi tv yani hapa ni mawazo maana bila hata aibu wananiambia na matumizi yao kama laptop mimi ndo naghalamika hata chuo mimi ndo niwapeleke sijui hata nifanyeje
 
Wakuu!

Kwa familia za kiAfrika tuna tabia za ndugu wa kutoka kwa mke na kwa mume kuishi na familia fulani, hasa wanapokuwa katika hali ya kutafuta misaada au kuugua.

Je inakuwaje pale mke na mume wanapokorofishana na kufikia hatua ya mke kufunga virago kurudi kwao...Je ndugu wa upande wa kike wanaondoka au hubaki?..chukulia kuwa hao ndugu si sehemu ya mgogoro wa familia husika, na hawajawahi kushabikia upande wowote!
Vipi umemtimua mke wako nini mkuu? Ushauri wangu ni kwamba hao usiwatimue hao shemeji zako, watajipima wenyewe kama ni sawa sawa kwa wao kubaki au kuondoka baada ya ndugu yao kutimuliwa.
 
mkuu wazazi wao wako hai kabisa na hata kama hawana uwezo wa kuwahudumia hao jamaa wanamkopo wa serikali wote hawafanyi kazi na hapa kuwahudumia washafanya lazima maana usipowapa walichokuomba siku hiyo huko ndani hakulaliki yani hawana mpango wa kuhama washaweka tv na makochi yao kwenye vyumba nilivyowapa sasa watoto wangu wanalala kwa shida sasa hivi

dada yao anasemaje???????

Halafu inaonyesha unawaendekeza wewe.......

Ingekua mie kwanza ningeangalia ustawi wa wanangu....wanalala kwenye mazingira gani.........

Then ningewakumbusha kuwa msaada ni hiari....

Tatu ningetumia nguvu kazi yao kugenerate income.... Yaani hapo ndo pakufuga kuku bata na ng'ombe....asiyetaka kuhudumia na kufanya kazi akatafute pa kwenda...sera ni asiyefanya kazi na asile
 
Back
Top Bottom