Kuishi kwa Shemeji! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuishi kwa Shemeji!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by PakaJimmy, Mar 26, 2012.

 1. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Wakuu!

  Kwa familia za kiAfrika tuna tabia za ndugu wa kutoka kwa mke na kwa mume kuishi na familia fulani, hasa wanapokuwa katika hali ya kutafuta misaada au kuugua.

  Je inakuwaje pale mke na mume wanapokorofishana na kufikia hatua ya mke kufunga virago kurudi kwao...Je ndugu wa upande wa kike wanaondoka au hubaki?..chukulia kuwa hao ndugu si sehemu ya mgogoro wa familia husika, na hawajawahi kushabikia upande wowote!
   
 2. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,263
  Trophy Points: 280
  Hapo lazima wasepe kwani walikaa kwa c/o yanani mke kama mke hayupo wat next???
   
 3. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ndoa ipi sasa ya kidini, kimila, kiserikali...! au ya kukutana Tandale kwa mtogole? jioni mnaowana kesho mashemeji wanahamia, mtondogoo mnapeana talaka.....! fafanua tuanze kudadavua.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Broda,
  Ishu hapa nadhani si aina ya ndoa!
  Mimi sijui wewe ni wa dini gani, lakini jichukulie wewe una mke na mkashindwana, shemeji zako itakuwakuwaje?...Na kama wao hawakushiriki ugomvi wako na mkeo, waondoke?
  Obviously, familia ambayo ina watu wengine wanaokuja kuishi ni lazima itakuwa ni kongwe kidogo, lakini ishu ya dini sielewi inaingiaje, maana ugomvi katika familia si function ya aina ya ndoa!
   
 5. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,237
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  nafikiri kuishi na mtu ambaya anahitaji msaada haiitaji kuwa lazima awe ndugu yako, ni moyo wa upendo tuu ndo unaohitajika,

  ndio ni wachache sana ambao wana moyo wa upendo wa kuishi na mtu ambaye sio ndugu yake au hanauhusiano nae kabisa lakini mi nafikiri kama mtu unajiweza huna haja ya kumrudisha kwao kisa umeachana na mke wako au mmewako

  pia maranyingi huwa tunasema kama unamapenzi ya dhati basi utapenda familia nzima na sio mmoja, so kuachana na mmoja sio maana kuichukia familia nzima. kumbuka UDUGU NI KUFAANA NA SIO KUFANANA.
   
 6. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkiwa na mahusiano ya jinsia mbili tofauti, neno ushemeji lazima liingie, sio ndoa tu.
  Ndoa navyoelewa ni mkataba wa halali baina ya mwanamke na mwanaume.
  Sasa kabla sijaendelea kutokana na nukuu yako hii labda unamaanisha ushemeji kama ushemeji au vyovyote vile...?
   
 7. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Mbona umeongelea mke kuondoka? Kwani mume hawezi kuondoka?
   
 8. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,338
  Likes Received: 2,343
  Trophy Points: 280
  Teh teh teh hiyo ndo raha ya Afrika hapo inategemeana na extent ya ugomvi kama ule wa kutiana jamba jamba usifukuze mtu ila kama ugomvi wa kukatana shoka watafutie nauli waende kwa amani.
   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ligi ndefu ya nini broda?
  Utanukuu vifungu vyote vya sheria ya ndoa ya Mwaka 1971, lakini hili sio suala la sheria na mahakama, ni social matter! Otherwise ningeshaipeleka kule Jukwaa la Sheria!
   
 10. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ..Kama hao ndugu wa Mke wana aibu ni lazima wataondoka, basically kinachowaweka hapo kwako ni Ndg yao ambae ndie mkeo. Kama hawana aibu watabaki ingawa nafsi itawasuta na pia watakughasi kiasi fulani shemeji yao ambae ni wewe kwamba umsamehe dada yao arudi.
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  OK...OK...OK...!
  Tufanye basi mume ameondoka, je wadogo zake wataondoka nao?...kwanini?
  (Japo hapa najua unapigania ku-retain heshima ya eneo maarufu la huko China-Beijing)
   
 12. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hapa tunapanuana mawazo!
  ww umeongelea inshu ya ushemeji kuja kuishi nyumbani kwako, pindi mnapotifuana na mke akaamua kuondoka, je! vipi kuhusu mashemeji...?
  Nami nilitaka kujua kama hawa mashemeji ndio wale kama ni dada'ake mliowana kindoa au jamii inafahamu tu kuwa mnaishi pamoja basi...?
  Hakuna ligi hapo.
   
 13. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #13
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mkuu,
  Chukulia ugomvi ni serious kidogo, mfano kufumania. Je kama ulikuwa unaishi nao na kuwalipia karo mashemegi zako utasitisha zoezi hilo?
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kukaa kwa shemeji..........!
  Huo nimtihani mkubwa sana, maana siku akishushiwa kipondo sijui unaingilia kuamulia au au unaugulia pembeni dada akipigwa....!
   
 15. R

  Raia Safi Member

  #15
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Iwe ndoa yoyote inabidi wasepe tu!
   
 16. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #16
  Mar 26, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  hapo hakuna mjadala, wote mtafungasha mizigo muondoke...:A S 13:
   
 17. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #17
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Du!
  Inasikitisha sana hii na moyo umeniuma!
  Kwahiyo dada ku'behave vyema chumbani kule ni salama ya watu wengi sana huko nje!..du!
   
 18. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #18
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Masanja Wa ze komedi huwa anawachana live wanaoishi kwa mashemeji lakini hawasikii....Hapo ndugu inabidi wasepe tu
   
 19. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #19
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,148
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  Ata usipowafukuza wanajiondoa wenyewe..lakini kumbuka mkipeana talaka mnagawana hadi vyumba vya nyumba kwahiyo mke akipewa mgao wake wanahamia humo.
   
 20. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #20
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ile ya Masanja ni too much!..Huwa ikikaribia kuanza ile mimi naaga nyumbani naenda Bar!
   
Loading...