Kuishi kwa mazoea badala ya sheria

Kuishi kwa mazoea badala ya sheria

anayepinga matumizi ya hiyo stendi "mpya" kuna 2 aidha ni siasa au labda haelewi vizuri khs mipango miji, hiyo stendi imewekwa kitaalamu na kwa akili kubwa kwa maoni yangu.

mabasi yote yatumiayo br. ya morogoro hayapaswi kuingia mjini abiria watashukia hapo na kuingia mwendokasi ambayo itawainggiza mjini in theory atleast, sasa tulipaswa tujadili jinsi ya kuboresha hapo kwenye mwendokasi lkn mpango ni briliant na kwa maoni yangu walioubuni na kuupanga walistahili tuzo, kwanza ukiangalia plan ya mradi wa mwendokasi kuna mpaka sehemu ya maegeso ya magari binafsi ambapo watu wanaotokea mikoani wangepaki magari (kama wangependa) na kupanda mwendokasi kuingia mjini na kuepuka foleni kwa maana mwendokasi haina foleni hivyo inakwenda faster in theory atleast klk gari binafsi au ilipaswa kuwa hivyo.

shida inakuja kwa upande wa mabasi yanayotokea kusini mtwara na lindi hao hawakupaswa kwa maoni yangu kulamizishwa kutumia hiyo stendi ya mbezi kwani ni itakuwa counterproductive ilipaswa wajengewe stendi yao huko tena sasa hivi mwendo kasi imeshafika huko mbagala pia, hivyo hao wa kusini wanastahili kuwa exempted kutumia hiyo stendi ya mbezi ...
Mjini ni wapi.
 
Tuwaulize hivi Shekilango kulikuwa karibu na makazi ya watu wote? Shekilango.kuna vyoo vya abiria? hakuna mauza nguo?

Ni uongo kusema ati walikuwa wanawapeleka abiria mpaka majumbani, yaani abiria wa Tegeta na wengine Kigamboni na Chamazi unawapelekaje baada ya kufika Dar! Wanatufanya sisi wote wapumbavu sijui?
umeeleza ukweli mtupu kwa uchungu sana gentleman dah!

huenda sekta ya usafirishaji imevamiwa na wahuni 🐒
 
Kinachokera stendi ya magufuli huduma za vyoo ni chafu sana na kunamatapeli wengi sana wanasumbua wananchi.Matapeli yakikuona tu hata kama husafiri yataanza kujiongelesha unaenda wapi moshi aumwanza?lengo ili uyahurumie angalau yapate ya chai
 
UKIMSIKIA BINADAMU YOYOTE ANA TAMANI UTAWALA WA SHERIA TAMBUA HUYO NI MPUMBAVU NA ANITHI WA AKILI ...kwa sababu neno sheria na neno haki ni maneno mawili yenye maana tofauti kabisa ila wapumbavu na wanasheria na wasomi wengi wanashindwa kutambua kuwa utawala wa shetia haimaanishi haki ....WENYE AKILI TUNATAKA UTAWALA WA HAKI WAPUMBAVU WANATAKA UTAWALA WA SHERIA .
We uko dunia ya mazuzu
 
Shida ni uelwa tu, watu wengi wanadhani bus likitoka Kusini tuseme Mtwara na Mtwara haliruhusiwi kushusha abiria Mbagala mpaka lifike Ubungo kwanza. Siodhani kama ndivyo ilivyo.

Hata ukitokea Dodoma au Mwanza unaweza shusha abiria Ruvu, njiani kuna vituo vidogo kama reli ilivyo. Reli ya SGR kutoka Dar hadi Kigoma ina vituo njiani haina maana SGR ikitoka Dar haisimaminl popote mpaka Kigoma lakini inajulikana kuna kituo Kikuu Dar na Kigoma.

Isitoshe mkuu wangu hata hilo bus la kutoka Mtwara linaweza kuwa na abiria safari yao inaishia Tegeta, Ubungo au Kimara! Ukimshushia Mbagala watawezaje kufika makwao? Swali linarudi palepale, tunacheza mchiriku.

Kinachotakiwa hapa Stendi ya Magufuli ndio mwisho wa safari za mikoani kuja Dar on main roads. Haina maana bus likifika Chalinze lisisimame pale kushusha abiria wa hapo mpaka wafike Magufuli stand , sio kweli ni upotoshaji tu kutaka sababu ambazo hazijengi.
Tena mabasi ya kusini ndiyo yalitunyanyasa sana wanakushusha Mbagala utajiju na mizigo yako! Hao wamiliki waache kutaka kuiweka serikali mifukoni mwao kwa kuwatesa wananchi. Matajiri hufanyaga vituko km hv wakiona serikali ni dhaifu. Wizara ya Uchukuzi haina waziri wala naibu waziri, ht yule mmbulu Habibu Suluo wa LATRA wameshamtisha. Huyu Rais hii nchi hayaiacha salama. Kweli Samia ni mswahili hakustahili kuwa ht waziri, mtu km Makame Mbarawa ni waziri? Hata David Kihenzile hafai, watu wazuri km kina Reuben Kwagilwa ht PM wameshatishwa. Eti mzanzibari Masauni anamtisha Kwagilwa? Alitumwa na dadake, nchi hii sahv haina uongozi wa juu
 
1. Tuanze na kuongelea uwezo na hali ya kituo cha Magufuli. Hauwezi kusema kuwa kitaboreshwa wakati kinaendelea kutumika maana ni hatari kwa usalama na afya za watumiaji. Watu wanapenda kupandia kwenye terminal za watu binafsi kwa sababu tuu ya huduma ( vyoo visafi vinavyo tosheleza), usalama wao na mizigo yao na kukwepa bughudha.
2. Biashara ya usafiri Tanzania na nchi nyingi zinazoendelea ni tofauti na ilivyo katika nchi zilizoendelea. Katika nchi zilizoendelea biashara hiyo inamilikiwa na operators wachache. Marekani kuna Greyhound, Ulaya kuna Flix n.k. Kwa sababu hiyo ni rahisi wao kuwa na sehemu zao ndani ya terminus kubwa. Pamoja na hayo miji mingi inakuwa na vituo vidogo vya kushusha na kupakia abiria.
Kwetu biashara hiyo inatawaliwa na operators wadogo wadogo wenye mabasi yasiyozidi matano. Utitiri huu wa operators unafanya management ya kituo kuwa changamoto.
3. Vituo vikuu vya mabasi havijengwi in isolation. Vituo hivyo vinaunganishwa na mifumo mingine ya usafiri. Mara nyingi vinakuwa karibu na vituo vikubwa vya treni za underground, treni za juu ya ardhi, mabasi ya mjini n.k. Viwanja vya ndege navyo vina vituo vya mabasi ya kwenda mikoani na mjini. Sisi hapa tunajenga vituo hivyo bila kuhakikisha kuwa kuna connections salama na za bei nafuu za kuwaleta na kuwatoa abiria. Kusema kuwa dala dala zitakuja ni upuuzi hasa ukizingatia aina ya wasafiri tuliokuwa nao.
4. Tofauti na tunavyo aminishwa, vituo vingi vya mabasi vikubwa katika nchi zilizoendea viko katikati ya mji, sio pembezoni. Port Authority New York iko katikati ya mji. Victoria Station London kiko katikati ya mji. Kinacho zingatiwa ni convenience kwa wasafiri. Na kukiweka katikati ya mji kinafanya biashara nyingine kama migahawa na maduka makubwa kuwa viable maana hazitegemei wasafiri peke yake.
Hilo la msongamano ni traffic engineering na management issue.
5. Tusiwabeze wafanya biashara. Wao wanafuata matakwa ya abiria wao. Badala ya kuwawekea Speed Gavana, Manispaa wangeweza kujenga terminal building pale pale Magufuli ambayo itatumiwa na operators wakubwa peke yao. Kila operator angekodishwa sehemu ya kutosha ya kuwa na nafasi ya huduma kwa ajili ya abiria wake. Hii ingewapa uwezo wa kupunguza bugudha kwa wateja wake. Operators wadogo wadogo waendelee kubanana walipo sasa.
6. Manispaa itafute namna ya kuhakikisha kuna usafiri wa hakika na salama wa kutawanya na kuleta abiria. Watu wapewe special license za kuunganisha kituo mama na vituo vidogo vya mjini.

Amandla...
 
Nimefuatilia sana mijadala mingi inaoendelea kuhusiana na tamko la Serikali juu ya mabus ya Usafiri Mikoani na matumizi ya Stendi ya Magufuli.

Ni hivi, miji yote mikubwa duniani ina Kituo kikuu cha Usafiri wa mabus au treni (Central Station) ambapo mabus yote hufikia pale kisha kuna usafiri wa ndani ambao kwa mji wetu wa Dar kuna usafiri wa Dart, taxi, Uber, Daladala na kadhalika ambao kazi yao huunganisha safari za abiria kule waondako.

Hii ni mipango miji inayolenga uboreshaji wa huduma, kupunguza msongamano wa magari mijini na usalama wa wananchi barabarani. Msafiri wa bus hawezi kuwa na haki zote barabarani pasipo kuzingatia watu wengine katika biashara zao.

Sii kila mfanya biashara ya Usafiri ana mabus ya kwenda Mikoani wengine shughuli zao huishia mjini na ndio riziki zao zinavyopatikana na mzunguko wa fedha unavyotakiwa. Hatuwezi kuondoa Umaskini nchini kwa huruma na sadaka za uongo wakati hawa ni wafanya biashara sio NGOs.

Ikiwa Stendi ya Magufuli ina mapungufu basi ni vema yakajadiliwa hayo mapungufu yakaboreshwa kuliko kuweka madai mengine ya uongo kama kwamba wananchi ni wajinga sana.

Isitoshe tunajua, hakuna bus linalotoza nauli moja kwa wasafiri wote, tiketi hutolewa kulingana na msafiri anaposhukia. Ukisema Pugu utatozwa gharama yake tofauti na yule anayekwenda Kariakoo au Mbezi.

Kisha hawa hawa wenye mabus ndio wana wapiga debe! Bei ya tiketi huongezwa kwa faida zaidi halafu unaambiwa ati wanasaidia maskini wasioweza kupanda Dart au Daladala.

Inawezekanaje bus linatoka Kigoma na samaki wamefungiwa kwenye buti la bus halafu anapelekwa Mpaka Kariakoo sokoni, waseme ati msafiri anasaidiwa! Samaki kwenye buti la mizigo na masanduku ya nguo za watu unasema unamsaidia nani?

Kisha Hakuna mzigo unaosafirishwa bure hata ukituma kikasha cha ubuyu utatozwa gharama ya usafiri.

Ifike pahala Watanzania tuache mazoea, tujifunze kuishi kwa Sheria na taratibu zilowekwa ndio Ustaarabu. Kutetea wenye mabus ambao wanadai hupeleka wateja wao Kariakoo, Chanika au Mbagala BURE wakati tunajua ndiko wao hulaza magari yao ni kutufanya wananchi wote wapumbavu kutetea Upumbavu - Haikubaliki.
Naomba nikuulize swali dogo Tu, je Mabasi hayo huko kwingine yana lala kwenye Kituo kikuu cha mabasi??
Ni wazi haya lali pale, hivyo Mabasi yanapewa nafasi Kituo kikuu sema masaa 2 kabla ya basi kuondoka, kama ilivyo Kwa ndege kwenye airport. Hivyo ni wazi wenye mabus watakuwa na maeneo Yao, ambapo basi litaa Kwa masaa Mengi bila kulipia hizo gharama za maegesho., hivyo MTU anaweza kuwa na yard yake Chanika , Kigamboni n.k
Hivyo akiambatana na abiria huko kigamboni, Chanika sio tatizo. Au akianza kupakia Mizigo huko sio tatizo kuna Mizigo unahitaji muda ili kuipangilia lakini pale stand ulipopewa nafasi ya masaa 2 huwezi kuifanya KAZI hiyo Kwa ufanisi.

Mimi ninaona wenye mabasi na Malory wange hamasishwa kuwa na maeneo Yao ya maegesho, hiyo kupita magufuli nk pia inategemeana na njia ntu anayo pitia. Magari ya lindi Ntwara yakianzia mbagala itakuwa ngumu kupita Kwa magufuli.basi linaenda Tanga , Moshi na Arusha na Lina pita Barabara ya Bagamoyo , na abiria wanalolipanda wamepewa vituo elekezi vya kupandio njiani , sio lazima yapite Magufuli
 
Nimefuatilia sana mijadala mingi inaoendelea kuhusiana na tamko la Serikali juu ya mabus ya Usafiri Mikoani na matumizi ya Stendi ya Magufuli.

Ni hivi, miji yote mikubwa duniani ina Kituo kikuu cha Usafiri wa mabus au treni (Central Station) ambapo mabus yote hufikia pale kisha kuna usafiri wa ndani ambao kwa mji wetu wa Dar kuna usafiri wa Dart, taxi, Uber, Daladala na kadhalika ambao kazi yao huunganisha safari za abiria kule waondako.

Hii ni mipango miji inayolenga uboreshaji wa huduma, kupunguza msongamano wa magari mijini na usalama wa wananchi barabarani. Msafiri wa bus hawezi kuwa na haki zote barabarani pasipo kuzingatia watu wengine katika biashara zao.

Sii kila mfanya biashara ya Usafiri ana mabus ya kwenda Mikoani wengine shughuli zao huishia mjini na ndio riziki zao zinavyopatikana na mzunguko wa fedha unavyotakiwa. Hatuwezi kuondoa Umaskini nchini kwa huruma na sadaka za uongo wakati hawa ni wafanya biashara sio NGOs.

Ikiwa Stendi ya Magufuli ina mapungufu basi ni vema yakajadiliwa hayo mapungufu yakaboreshwa kuliko kuweka madai mengine ya uongo kama kwamba wananchi ni wajinga sana.

Isitoshe tunajua, hakuna bus linalotoza nauli moja kwa wasafiri wote, tiketi hutolewa kulingana na msafiri anaposhukia. Ukisema Pugu utatozwa gharama yake tofauti na yule anayekwenda Kariakoo au Mbezi.

Kisha hawa hawa wenye mabus ndio wana wapiga debe! Bei ya tiketi huongezwa kwa faida zaidi halafu unaambiwa ati wanasaidia maskini wasioweza kupanda Dart au Daladala.

Inawezekanaje bus linatoka Kigoma na samaki wamefungiwa kwenye buti la bus halafu anapelekwa Mpaka Kariakoo sokoni, waseme ati msafiri anasaidiwa! Samaki kwenye buti la mizigo na masanduku ya nguo za watu unasema unamsaidia nani?

Kisha Hakuna mzigo unaosafirishwa bure hata ukituma kikasha cha ubuyu utatozwa gharama ya usafiri.

Ifike pahala Watanzania tuache mazoea, tujifunze kuishi kwa Sheria na taratibu zilowekwa ndio Ustaarabu. Kutetea wenye mabus ambao wanadai hupeleka wateja wao Kariakoo, Chanika au Mbagala BURE wakati tunajua ndiko wao hulaza magari yao ni kutufanya wananchi wote wapumbavu kutetea Upumbavu - Haikubaliki.
Gereji zao ziko wapi? Au mabasi hayahitaji matengenezo. Kutoka Magufuli mpaka Kisemvule ni kilomita ngapi? Wewe unaweza kukodi teksi toka Mbezi mpaka Kisemvule au Mbagala? Teksi toka Magufuli mpaka Kinondoni si chini ya shilingi 30,000/= ambayo ni zaidi ya nauli ya Dar kwenda Morogoro.
Unapojadili jambo usijifikirie wewe unayeishi Mbezi ya Magufuli ukamuudhi anayeishi Mbezi ya Bagamoyo.
 
Back
Top Bottom