Kuiper Belt: Behind the certain

Pale uliposema "Hao Aliens wanaweza kuwa ni product ya huyo shetani.....".Hapa ilimaanisha nini ? Sasa unaponiambia wapi sijaelewa unanishangaza sana.Hoja yako hiyo niliijibu kwa kukuonyesha ni jinsi gani huwezi kuonyesha uhusiano kati ya Shetani na hao Aliens.Kama hukuelewa tamko shetani lilisimama kumaanisha Shetani wa kijini,hapa kunaonyesha dhahiri ni jinsi gani usivyokuwa na elimu juu ya tamko hilo la Shetani na jini.Sasa kutokana na kauli yako ya kuniambia kauli zangu zinakinzana,ukweli uko dhidi yako ni kuwa elimu yako haikuwa na uwezo wa kukufikisha kutambua suala la shetani na jini.

Kwahiyo mzee kauli zangu hazipingani aisee.Rudi kusoma hoja vizuri,kisha ujenge hoja.Uchache wa elimu za watu na kutaka kuingilia mambo makubwa na kuyaelezea ndio kumetufikisha hapa.Si kila mtu anapaswa aandike kuhusu jambo fulani,wala si lazima wewe uandike kuhusu jambo fulani na kamwe hautoulizwa kwanini hujaandika kuhusu jambo fulani.Kila mtu anatakiwa kuvaa viatu vyake,viatu vinavyomtosha yeye,si fulani kuvaa viatu vya fulani bila kuwa na sifa anuai za kuvaa viatu hivyo.Ndio maana mimi kwa uchache wangu wa elimu ni kaamua kuwa mwanafunzi,na kuhoji jambo kielimu.

Ukiandika makala nyingine usisahau kuni tag mzee.
 
Kiongozi kamwe huwezi kuukataa ukweli huo kama kweli wewe ni mtu wa elimu.Hoja yako msingi wake ni wa sayansi ndio maana pale ulipo anza kuleta stori za Kuiper belt na nadharia zake.Ndio maana kuna jamaa mmoja alikuuliza swali moja la msingi sana juu ya maelezo,akionyesha ya kuwa maelezo yako hayajaonyesha uwepo wa Mola aliyeumba,yaani kuhusu hizi ngano mbona Mola haonekani nafasi yake.Sasa unapotaka kukanusha hoja yako na kukataa ya kuwa haija mili kisayansi,basi twambie hoja yako msingi wake ni upi.Ila kaa ukijua hoja yako msingi wake ni sayansi.

Nimezisoma sana hoja mzee,ndio maana nikaamua kukujibu,bali nimezielewa sana.
 
Umeuliza swali zuri sana mzee,ukweli unabaki pale pale.Umejaribu kugusia nukta moja ya utoto na ghafla ukafikia hitimisho lisilo la kielimu kwa kuegemeza kwenye mahakama.Sisi hatuangalii mahakama sisi tunaangalia utoto na suala la ushahidi na tunaangalia vipi tutaupata ukweli kama ulivyo si kama unavyojitokeza kwa watu.

Ukimuangalia mtoto kwa umbile bila kaungalia silika yake ni vigumu sana kunielewa,ila tunaelekea kuzuri sasa.Niliposema mtoto sikuacha kuzungumzia jambo la msingi sana liitwalo kupambanua mambo.

Turudi katika ukweli muhimili,hii umeshawi kusikia kuna mtume alipewa utume akiwa mtoto au nabii aliyekuwa nabii akiwa mtoto,ukitaka kuukataa ukweli utaruhusu madudu mengi sana katika kupata habari ya uhakika.Mfano wa hili ni sawa sawa na kuchukua ushahidi wa mtu mlevi au mtu muovu.

Sijasema watoto hawasemi kweli mzee,mfano mtoto ukimuuliza huyu ni baba yako,kama kweli ni baba yake atakwambia ni baba yake lakini mtoto hawezi kung'amua mambo na kuyapembua na kutofautisha kweli kutokana na uongo.Embu hapa jaribu kufikiri kidogo kisha nitakuja na mifano juu ya hilo.
 
Tamko kutawala lina maana ya kilugha na maana ya kisheria.Ndio maana nahisi naongea mambo mepesi sana kiasi ambacho akili yako haikuweza kuyafikia.Kutawala si mpaka uwe katika mfumo fulani,yaani kutawala kidemokrasia au mfano wake katika kutawala kwa kifedhuli.Kutawala hapa nazungumzia kutawala kwa ujumla kwa kiludha na kimatendo.Binadamu ana akili kuliko viumbe wengine na amepewa akili kwa ajili ya kutahiniwa na kuwatawala viumbe wengine,kwa kuwajua tabia zao na kuweza kuwahudumia.Huu ni mfano mwepesi sana juu ya utawala wa binadamu dhidi ya viumbe wengine.

Leo tembo hawezi kumfuga binadamu na kumzidi maarifa lakini,leo binadamu anamfuga tembo na kumfundisha.Hivi hata hili linataka tuminyane mzee ? Embu jitahidi kuelewa isee.
 
Nimekumbuka ile series ya falling skies jinsi wale alien walivyokuwa wanawasiliana na binadam
 
Unaposema binadamu ana akili kuliko viumbe wengine una maana gani?

Hao viumbe wengine ni wapi/wako wapi?
 
Kuna mambo mtoto hawezi kuhusishwa hasa mambo yanayohusu tafakuri ambapo mtoto anakuwa hana.Ili binadamu aweze kujitambua anahitaji kufikia umri fulani ambao utamfanya awe na uwezo wa kutafakari kwasababu ubongo wake unakuwa umekomaa vya kutosha.Huu ndiyo muktadha wa hoja yako kuhusu utoto.Tatizo huo siyo muktadha wa hiki tunachokijadili hapa....

Suala la utume na mengine ya kufanana na hayo hawezi kupewa mtoto kwasababu yanahitaji fikra zilizokomaa na tafakuri hivyo mfano wako huu una matege....

Hapa tunazungumzia kitendo cha kuona kitu na kukielezea namna kilivyo bila kupindisha.Katika muktadha huu mtoto anaweza kuwa kwenye nafasi kubwa na nzuri zaidi kuaminika kwasababu mtoto hana namna ya kupindisha kwa maslahi yoyote labda tu atishwe.....

Katika kushuhudia jambo,wakiwa wameona watu wa wili mmoja ni mtoto na mwingine ni mtu mzima kisha wakapaswa watoe ushahidi wa jambo lile ushahidi wa mtoto utachukuliwa kwa uzito zaidi kutokana na utoto wake.Jambo lililo hapa linafanana na hilo,ni suala la kuona na kusema ulichokiona na siyo zaidi ya hapo na hapa mtoto anakuwa na uzito zaidi....
 
1;Unaposoma maandiko zingatia sana kila mwandishi anachokuwa anaandika na kujua muktadha wa jumla na muktadha wa kila sentensi ili uelewe mkuu.Kwenye sentensi yamngu nimetumia neno "inawezekana",hapa nilikuwa sijamaanisha iko hivyo isipokuwa nilimaanisha kuwa "kuna uwezekano" nilichokisema kikawa hivyo lakini siyo kama unavyodhani wewe...

2;Niliposema product nadhani nilikuchanganya.Nilitumia neno hilo nikimaanisha kuwa "hao niliowataja wanaweza kuwa ni matokeo ya 'akili' ya Shetani",nitakupa mfano maana naona una shida ya kuelewa haraka....

Mtu akisema kwamba tarakilishi [Computer] ni matokeo ya binadamu hana maana ya kwamba hiyo tarakilishi ni binadamu pia bali matokeo ya kufikiri au akili ya binadamu.Sasa maana hii ndiyo niliyoimaanisha nilipoandika kuwa inawezekana Aliens ni product ya huyo huyo Shetani...

Ukiandika makala nyingine usisahau kuni tag mzee
Haina tatizo kiongozi.....
 
Nilikuuliza kwamba,kwako wewe sayansi ni uongo yote au kuna mambo inasema kweli?

Sijaona mahali umejibu hili swali....
1;Siyo kweli kuwa napaswa kuituhumu akili yangu kwasababu tu ya kutoyaelewa maelezo yako nitakueleza hili nikiwa najibu maelezo yako hapa chini....

2;Mfano wako pia siyo sahihi na hili linaendelea kuonesha shida kwenye tafakari yako..

Kujifunza jambo ili ulielewe siyo sawa na kujifunza ili ulifanye.Kinachotofautisha hayo mawili ni dhumuni la kujifunza na sentensi yako ya pili inakataza dhumuni la kujifunza jambo ili ulifanye na siyo kwamba unakatazwa kujifunza jambo kwa ujumla wakeHii ndiyo tofauti iliyoko kwenye mfano wako...

Wewe ulichokisema ni tofauti na hiki.Nakubali kwamba ukikagua msingi wa kitu unaweza kujia tatizo la kitu hicho lakini hili linategemea na muundo wa hoja na muktadha mzima wa jambo lenyewe...

Kama jambo ni uongo kwa ujumla wake itakuiwa sahihi kurejea misingi yake lakini kama siyo uongo lote misingi haiwezi kukusaidia chochote,hapa rejea swali langu kwako kama unaamini [sijatumia neno amini kwa bahati mbaya] sayansi yote ni uongo au inadanganya kwenye baadhi ya maeneo tu....
2.Pili kuona kwako kauli zangu kama zinakinzana,lazima uituhumu elimu yako kuwa haina uwezo kung'amua mawazo yangu au hoja nilizo zihudhurisha hapo juu.
Hapana,jambo kutokueleweka linakuwa na mambo mawili...

1;Mtoa maelezo kuhusu jambo haeleweki
2;Anayesikiliza maelezo hana uwezo wa kuelewa

Hapa ninachokiona mimi ni tatizo la kwanza na linaongezewa nguvu na kauli yako ya kudhani moja kwa moja kuwa mimi ndiye mqwenye tatizo na siyo wewe.Nasema hivi kwasababu mtu yoyote mwenye tafakari hawezi kujihesabia haki kwanza isipokuwa anaweka nafasi ya kukosolewa [room of doubt] kwasababu anajua uwezekano wa yeye kutokuwa sahihi upo....

Wewe hujafanya hivi,unanirushia tu tuhuma japokuwa nakuonesha mara nyingi tu namna unavyokosea kwenye maelezo yako bila wewe kuonesha ni namna ipi hukosei....

Jaribu kuangalia upya kiongozi...
 
Ndiyo maana nakuambia kuwa hujaelewa....

Base ya hoja yangu siyo sayansi pekee na ndiyo maana nimemtaja huyo mama wa ki-Japan anayetoka familia ya kifalme,sijui ni kwa vipi unashindwa kuelewa mambo rahisi kama haya....

Unapotaka kuleta ishu ya Mola ndiyo unazidi kuingia machakani kabisa.Unataka nimtaje hapo kwasababu ipi haswa? Yaani unaweza kujadili kuhusu uwepo wa vyura wenye macho 20 kwenye mapango ya Amboni na wapo watu waliowaona vyura hao halafu unamtaja Mola kwa misingi ipi?

Kama nilikuwa nazungumzia chanzo cha uwepo wa Aliens hapo sawa ningetakiwa kuonesha kwamba base ya hoja zangu ni uwepo wa Mungu au kinyume chake,lakini nazungumzia uwepo wa viumbe ambavyo kuna watu wamewaona,sasa hapo unataka nitaje/nimtaje Mungu kwa misingi ipi?

Hii ni shida sana....
 
 
Sasa kiongozi kama umeshindwa kuona usawa wa hizo kauli mbili.Unazidi kunipa mashaka na kunifanya nitoke kifua mbele kwa wewe kushindwa kung'amua kauli hizo mbili.

Niliposema "Nilijifunza shari ili niijue nisifanyeshari" na kauli "Haifai kujifunza shari".Hapa ulitakiwa kwanza ujue nini maana ya shari,pili kwanini sitakiwi kujifunza shari na kwanini nilijifunza shari ili nisiifanye shari.Kauli zote mbili zime mili katika kuelewa jambo.Kitu ambacho wewe umekitoa katika kauli moja.

Kiongozi naposema akili haina uwezo wa kung'amua haya ninayo yasema nimemaanisha hivyo.
 
Hilo ndio tatizo kubwa uliokuwa nalo.Mzee mambo ya kiulimwengu na yasiyokuwa hayo huwezi kuyajadili bila kuzungumzia uwepo wa yule alieviweka kutafakari kwa mtindo huo ni kutafakari kwa kitoto na ndio huko kulikowafanya watu wawe wazito wakufikiri kuliko tukuka.
 
hivi ulielewa utofauti niliouzungumzia kwenye hayo maelezo ni upi?

Mkuu inaonekana kama tunazungushana kwenye jambo ambalo hatuwezi kuelewana na shida kubwa ni namna ya kufikiri iliyopo hapa....

Na hilo ndilo tatizo kubwa....
 
Unafahamu maana ya neno muktadha?

Maana hili ndilo tatizo lako kubwa mkuu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…