Kuiomba Tanganyika ni kuenzi ukoloni

Kuiomba Tanganyika ni kuenzi ukoloni

Mkuu kwani huo muungano una faida gani,nikikuomba unipe au utaje faida za muungano,unipe facts sio hisia na mambo ya kufikirika utanitajia?

Faida kubwa ya muungano Ni Amani tuliyonayo pili ni ulinzi tuliyonao tukiiacha Zanzibari Tanzania haipo salama kabisa kutokana na matatizo ya itikadi ya kiislamu na ugaidi Usalama Zanzibar umeimalishwa kutoka na muungano

Sent from my iPhone
 
Tanganyika ni ya mjerumani bali Tanzania ni zao la watanzania sasa unadai nchi ambayo sii yako akili matope

Sent from my iPhone

Kama unaishi mjini kwa kazi kuandika propaganda zaifu namna hii nakuonea uruma. Ila kama umefikiria kwelikweli ukaona unapointi ya kusema nakushauri ukajiunge na elimu ya watu wazima.
 
Kama unaishi mjini kwa kazi kuandika propaganda zaifu namna hii nakuonea uruma. Ila kama umefikiria kwelikweli ukaona unapointi ya kusema nakushauri ukajiunge na elimu ya watu wazima.

nimeandika Tanganyika imetoka wapi watu hawakuelewi sasa nimehisi naongea na watanzania wenzangu ambao hawakupata fursa ya Elimu kama unahusika apply kwenye topic

Sent from my iPhone
 
Ujinga uko wapi? Wewe ni Nape? Siamini kwamba jambo kubwa kama hilo, unalikataa kwa sababu ndogo kiasi hicho. Nani alikufundisha kwamba Tanganyika ilikuwepo kwa miaka miwili tu! Kabla ya hapo Mwingereza alitawala nchi gani?

Achaneni na vijimaelezo vya wajumbe uchwala wa CCM. ETI TUNAENZI UKOLONI! What is your name? Mbona wengi munafurahia kuitwa majina ya wakoloni? Mbona Rais wako anafurahia nchi kuwa mwanachama wa common wealth. Unajua maana yake?

Kwa wa TZ wenzangu, sasa nayaona madhala ya kuwa chini ya CCM kwa kipindi kirefu. Kiwango chetu cha uelewa na hata kufikiri kinaendelea kuwa chini kabisa! CCM wao hata baada ya miaka yote hii bado viongozi wao ni class 7.

Mkuu wasamee hawajui wasemalo wanahisi watanganyika wa leo ni miaka ya 70...........

"wakishindwa kuunda serekali moja,serekali tatu haiepukiki"
 
Umoja wa mataifa unasimamia wanyongwe wasio na kitu kwa namna watakayo matajiri wanaouchangia. Hata uongozi bila wakubwa kupenda hupati. Atashtakiwa na kunyongwa sadam na Gaddafi sio Bushi. Huu mfano sio kabisa.
 
nimeandika Tanganyika imetoka wapi watu hawakuelewi sasa nimehisi naongea na watanzania wenzangu ambao hawakupata fursa ya Elimu kama unahusika apply kwenye topic

Sent from my iPhone

Embu soma ulichoandika. Yaani Uandike wewe alafu watu wasinielewe mimi
 
Faida kubwa ya muungano Ni Amani tuliyonayo pili ni ulinzi tuliyonao tukiiacha Zanzibari Tanzania haipo salama kabisa kutokana na matatizo ya itikadi ya kiislamu na ugaidi Usalama Zanzibar umeimalishwa kutoka na muungano

Sent from my iPhone

Kwani mkuu kabla ya muungano hatukua na amani?kwa hiyo wazanzibari ndio chanzo cha amani yetu?sitaki kuamini hilo. Pili kwa hiyo hatutaki kuwaachia wazanzibar kwa kuhofia makundi ya wahuni wa kiislam?

Mkuu bado hizo ni hoja dhaifu sana kujustfy kwa nini tuudumishe muungano,muungano hauna faida yoyote zaidi ya faida za kufikirika.
 
Kuna uchunguzi umefanyika kuwa mtoto hamzidi baba yake akili piga ua galagaza "street smart-Bloomberg TV!"

Sent from my iPhone
 
HISTORIA INANYESHA TUMEPIGA HATUA KWA KUANZISHA TANZANIA NA NI TENDO LAKUONYESHA TUPO HURU KIMAWAZO NA KIFIKRA!
Kurudisha Tanganyika yenye historia hii ni kuonyesha kizazi cha vilaza
Maeneo yaliyoitwa baadaye "Tanganyika" yaliunganishwa mara ya kwanza tangu mwaka 1886 kama koloni ya Ujerumani iliyoitwa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Kabla ya kufika kwa ukoloni kulikuwa na madola madogo mbalimbali na maeneo madogo ya kikabila. Kanda la pwani pamoja na njia za misafara kuelekea Ziwa Tanganyika vilikuwa chini ya athira ya Usultani wa Zanzibar.

Tangu 1885 Karl Peters kwa niaba ya Shirika la Ukoloni wa Kijerumani (Gesellschaft für Deutsche Kolonisation) alianza kufanya mikataba na watawala wa kienyeji katika maeneo ya Usagara, Nguru, Useguha und Ukami iliyoweka msingi kwa madai yake ya kuchukua utawala mkuu wa maeneo haya. Uenezeaji wa Wajerumani uliendelea hasa baada ya kushinda upinzani katika vita ya Abushiri na vita dhidi ya Wahehe.

Koloni ile ya kijerumani ilikuwa kubwa zaidi kuliko Tanganyika ya baadaye maana ilijumlisha pia maeneo ya Rwanda na Burundi pamoja na sehemu ndogo ya Msumbiji.

Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia (1914 - 1918) koloni hii ya Kijerumani ilitekwa na jeshi za Uingereza na Ubelgiji. Mkataba wa Versailles wa 1919 ulikuwa na kanuni za kuchukua koloni zote za Ujerumani na kuzikabidhi kwa mataifa washindi wa vita. Sehemu kubwa ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani iliwekwa chini ya utawala wa Uingereza, kasoro maeneo ya Rwanda na Burundi yaliyokabidhiwa mkononi mwa Ubelgiji.

1919 sehemu kubwa ya koloni ya Kijerumani ilikabidhiwa rasmi mkononi mwa Uingereza kama eneo lindwa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa kulingana na kifungo 22 cha mkataba wa Versailles. Mwaka 1922 Shirikisho la Mataifa lilithebitisha hatua hii na kuamua masharti ya kukabidhi.

Waingereza walihitaji jina jipya kwa ajili ya koloni mpya na tangu Januari 1920 wakaamua kuiita "Tanganyika Territory" kwa kutumia jina la ziwa kubwa upande wa mashariki ya eneo.

Sent from my iPhone

Ni nchi ngapi zilibadili majina baada ya uhuru? Unakusudia Zanzibar bado wanaenzi ukoloni? Hoja nyingine ni mfu sana. Kwa wasomi wa aina yako wasioenzi historia, bado tuna safari ndefu kufika uhuru kamili. Unapigania usichokijua
 
Sijawahi kuona wala kusoma mawazo ya kipuuzi kama ya huyu mleta maada
MUNGU IBARIKI TANGANYIKA
 
Faida kubwa ya muungano Ni Amani tuliyonayo pili ni ulinzi tuliyonao tukiiacha Zanzibari Tanzania haipo salama kabisa kutokana na matatizo ya itikadi ya kiislamu na ugaidi Usalama Zanzibar umeimalishwa kutoka na muungano

Sent from my iPhone

1. Faida ya muungano ni amani - fafanua ni kwa jinsi gani muungano umeleta amani katika zama hizi, nami nitakuonyesha kuyumba kwa amani yetu watanganyika kunavyo sababishwa na muungano.

2. Ulinzi - fafanua muungano wetu unawazuiaje magaidi mf. Alqaeda kutekeleza mashambulizi yao Tanganyika wakiamua, nami nitakuonyesha ni kwa jinsi gani muungano umechangia kuwepo vitendo vya ugaidi Tanganyika
 
Kwani mkuu kabla ya muungano hatukua na amani?kwa hiyo wazanzibari ndio chanzo cha amani yetu?sitaki kuamini hilo. Pili kwa hiyo hatutaki kuwaachia wazanzibar kwa kuhofia makundi ya wahuni wa kiislam?

Mkuu bado hizo ni hoja dhaifu sana kujustfy kwa nini tuudumishe muungano,muungano hauna faida yoyote zaidi ya faida za kufikirika.

"MAASI YA TANGANYIKA RIFLES
Jeshi la Tanganyika Rifles liliasi tarehe 20 Januari 1964 na maasi hayo kuzimwa 25 Januari 1964. Maasi yalihusisha vikosi vya DSM na Tabora 1st Bn na 2nd Bn." - http://tpdf.mil.tz/index.php?id=4
 
Wakulalamika ni Zanzibar sisi si watanzania maana Mungano ulivyo kwasasa ni kama tumeiteka Zanzibar sasa kuuomba madara ya Tanganyika nikuomba jina tu ambalo ni kuomba ukoloni maana katika muuungano Zanzibar tuliwateka hawana chochote tuwape madaraka zaidi wawatumikie wananchi wao

Sent from my iPhone

Mimi siombi Tanganyika, ninataka Tanganyika iwe-reactivated.
 
"MAASI YA TANGANYIKA RIFLES
Jeshi la Tanganyika Rifles liliasi tarehe 20 Januari 1964 na maasi hayo kuzimwa 25 Januari 1964. Maasi yalihusisha vikosi vya DSM na Tabora 1st Bn na 2nd Bn." - http://tpdf.mil.tz/index.php?id=4

Muungano ulitatuaje tatizo hili?
 
Muungano ulitatuaje tatizo hili?

Nimeweka hilo kujibu swali la mtu aliyesema tulikuwa na amani kabla ya Muungano, kuhusu swali lako rejea:

MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

Kuungana kwa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Apr 1964 pia vijana waliobaki baada ya maasi toka Tanganyika Rifles waliungana na vijana jeshi la Ukombozi wa Wananchi wa Zanzibar (PLA) Peoples Liberation Army).

CHANZO:​
[url]http://tpdf.mil.tz/index.php?id=4[/URL]​

Faida kubwa ya muungano Ni Amani tuliyonayo pili ni ulinzi tuliyonao tukiiacha Zanzibari Tanzania haipo salama kabisa kutokana na matatizo ya itikadi ya kiislamu na ugaidi Usalama Zanzibar umeimalishwa kutoka na muungano

Wewe lazima unaumwa si bure, kwanza nimesoma historia yako ndefu ya Tanganyika bila kutumia muda kuangalia uhalisia wake umeshindwa kuonyesha ubaya wa Tanganyika kama nchi au kama jina la kurithi kutoka kwa Mkoloni. Pili, unaposema Tanganyika ikipatikana hatuko salama kwasababu ya Zanzibar ndugu yangu hoja hii haina mantiki yoyote. Vita za kisasa zinapiganishwa kidijitali zaidi watu wana ndege ambazo hazihitaji Rubani sasa hiyo Zanzibar yako itakusaidia nini. Hali kadhaliwa wanaweza kuweka Manowari Bahari ya Hindi na kutoa kichapo mwanzo mwisho?
 
Nimeweka hilo kujibu swali la mtu aliyesema tulikuwa na amani kabla ya Muungano, kuhusu swali lako rejea:

MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

Kuungana kwa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Apr 1964 pia vijana waliobaki baada ya maasi toka Tanganyika Rifles waliungana na vijana jeshi la Ukombozi wa Wananchi wa Zanzibar (PLA) Peoples Liberation Army).

CHANZO:​
[url]http://tpdf.mil.tz/index.php?id=4[/URL]​

Ni heri ungeanza kwanza na sababu za kuasi, ndipo uelezee ni kwa jinsi gani muungano umezuia uasi. Na kama hujui nitakusaidia;

Sababu kubwa ya uasi ilikuwa ni maslahi. Maafisa wa kizungu walilipwa mishahara minono wakati weusi walilipwa kiduchu.

Pia vyeo vya juu vilihodhiwa na wazungu huku weusi wakikabana koo chini.

Haya bingwa wa muungano tufafanulie ni kwa vipi muungano ulitatua matatizo hayo.
 
Back
Top Bottom