Kuiomba Tanganyika ni kuenzi ukoloni

Kuiomba Tanganyika ni kuenzi ukoloni

Pascal Ndege

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2012
Posts
2,977
Reaction score
1,900
HISTORIA INANYESHA TUMEPIGA HATUA KWA KUANZISHA TANZANIA NA NI TENDO LAKUONYESHA TUPO HURU KIMAWAZO NA KIFIKRA!
Kurudisha Tanganyika yenye historia hii ni kuonyesha kizazi cha vilaza
Maeneo yaliyoitwa baadaye "Tanganyika" yaliunganishwa mara ya kwanza tangu mwaka 1886 kama koloni ya Ujerumani iliyoitwa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Kabla ya kufika kwa ukoloni kulikuwa na madola madogo mbalimbali na maeneo madogo ya kikabila. Kanda la pwani pamoja na njia za misafara kuelekea Ziwa Tanganyika vilikuwa chini ya athira ya Usultani wa Zanzibar.

Tangu 1885 Karl Peters kwa niaba ya Shirika la Ukoloni wa Kijerumani (Gesellschaft für Deutsche Kolonisation) alianza kufanya mikataba na watawala wa kienyeji katika maeneo ya Usagara, Nguru, Useguha und Ukami iliyoweka msingi kwa madai yake ya kuchukua utawala mkuu wa maeneo haya. Uenezeaji wa Wajerumani uliendelea hasa baada ya kushinda upinzani katika vita ya Abushiri na vita dhidi ya Wahehe.

Koloni ile ya kijerumani ilikuwa kubwa zaidi kuliko Tanganyika ya baadaye maana ilijumlisha pia maeneo ya Rwanda na Burundi pamoja na sehemu ndogo ya Msumbiji.

Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia (1914 - 1918) koloni hii ya Kijerumani ilitekwa na jeshi za Uingereza na Ubelgiji. Mkataba wa Versailles wa 1919 ulikuwa na kanuni za kuchukua koloni zote za Ujerumani na kuzikabidhi kwa mataifa washindi wa vita. Sehemu kubwa ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani iliwekwa chini ya utawala wa Uingereza, kasoro maeneo ya Rwanda na Burundi yaliyokabidhiwa mkononi mwa Ubelgiji.

1919 sehemu kubwa ya koloni ya Kijerumani ilikabidhiwa rasmi mkononi mwa Uingereza kama eneo lindwa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa kulingana na kifungo 22 cha mkataba wa Versailles. Mwaka 1922 Shirikisho la Mataifa lilithebitisha hatua hii na kuamua masharti ya kukabidhi.

Waingereza walihitaji jina jipya kwa ajili ya koloni mpya na tangu Januari 1920 wakaamua kuiita "Tanganyika Territory" kwa kutumia jina la ziwa kubwa upande wa mashariki ya eneo.

Sent from my iPhone
 
ImageUploadedByJamiiForums1396528263.640598.jpg

Baada ya kuomba bendera ya tanganyika nitahakikisha tunapewa bendera halisi ya Tanganyika! Kwasababu tutakuwa tumeamua kuishi kwa historia

Sent from my iPhone
 
Ni ujinga ukiomba nchi ya Tanganyika iliyodumu kwa muda wa miaka 2 na miezi 4 tukaikataa Tanzania iliyodumu miaka 50.
 
Mkuu Pascal Ndege,umepotoka.Kuidai Tangayika ni kuhakiki uhuru na kuutukuza uhuru tulioupata mwaka 1961. Iliyopata uhuru toka kwa wakoloni ni Tanganyika.Inayodaiwa ni Tanganyika. Kuna kosa gani kuidai? Halafu usichanganye uhuru wa nchi na ushirikiano.Uhuru kila nchi ina wake;ushirikiano ni wa hiari na hauonyeshi kuwa huru toka kwenye ukoloni.Kwa taarifa yako,wakoloni wanatawala tena nchi zetu kupitia ushirikiano uliopo.
 
Last edited by a moderator:
Sijakiona kifute cha "LIKE" hapo kwenye bendera halisi ya Tanganyika hapa huwenda UKAWA wamejipenyeza ache nikupe "big like" hukuhuku!
 
Propaganda mufilisi za CCM !!!!!!!! Mnaishia kuleta hati za kughushi za Muungano! Mmeshikwa pabaya mwaka huu! Hamchomoki!!!!
 
Mkuu Pascal Ndege,umepotoka.Kuidai Tangayika ni kuhakiki uhuru na kuutukuza uhuru tulioupata mwaka 1961. Iliyopata uhuru toka kwa wakoloni ni Tanganyika.Inayodaiwa ni Tanganyika. Kuna kosa gani kuidai? Halafu usichanganye uhuru wa nchi na ushirikiano.Uhuru kila nchi ina wake;ushirikiano ni wa hiari na hauonyeshi kuwa huru toka kwenye ukoloni.Kwa taarifa yako,wakoloni wanatawala tena nchi zetu kupitia ushirikiano uliopo.

division mbowe hawajui tanganyika
 
Last edited by a moderator:
mkuu samahani unataka kutuambia wanaotumia majina ya nchi walizokomboa kutoka uhuru wamepotoka?
kuweka historiia vizuri. Tanganyika ilipata uhuru 9 december 1961 ikawa jamhuri mwaka 1962 then Tanganyika na zanzibar zikaungana na kuwa Tanzania .
HISTORIA INANYESHA TUMEPIGA HATUA KWA KUANZISHA TANZANIA NA NI TENDO LAKUONYESHA TUPO HURU KIMAWAZO NA KIFIKRA!
Kurudisha Tanganyika yenye historia hii ni kuonyesha kizazi cha vilaza
Maeneo yaliyoitwa baadaye "Tanganyika" yaliunganishwa mara ya kwanza tangu mwaka 1886 kama koloni ya Ujerumani iliyoitwa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Kabla ya kufika kwa ukoloni kulikuwa na madola madogo mbalimbali na maeneo madogo ya kikabila. Kanda la pwani pamoja na njia za misafara kuelekea Ziwa Tanganyika vilikuwa chini ya athira ya Usultani wa Zanzibar.

Tangu 1885 Karl Peters kwa niaba ya Shirika la Ukoloni wa Kijerumani (Gesellschaft für Deutsche Kolonisation) alianza kufanya mikataba na watawala wa kienyeji katika maeneo ya Usagara, Nguru, Useguha und Ukami iliyoweka msingi kwa madai yake ya kuchukua utawala mkuu wa maeneo haya. Uenezeaji wa Wajerumani uliendelea hasa baada ya kushinda upinzani katika vita ya Abushiri na vita dhidi ya Wahehe.

Koloni ile ya kijerumani ilikuwa kubwa zaidi kuliko Tanganyika ya baadaye maana ilijumlisha pia maeneo ya Rwanda na Burundi pamoja na sehemu ndogo ya Msumbiji.

Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia (1914 - 1918) koloni hii ya Kijerumani ilitekwa na jeshi za Uingereza na Ubelgiji. Mkataba wa Versailles wa 1919 ulikuwa na kanuni za kuchukua koloni zote za Ujerumani na kuzikabidhi kwa mataifa washindi wa vita. Sehemu kubwa ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani iliwekwa chini ya utawala wa Uingereza, kasoro maeneo ya Rwanda na Burundi yaliyokabidhiwa mkononi mwa Ubelgiji.

1919 sehemu kubwa ya koloni ya Kijerumani ilikabidhiwa rasmi mkononi mwa Uingereza kama eneo lindwa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa kulingana na kifungo 22 cha mkataba wa Versailles. Mwaka 1922 Shirikisho la Mataifa lilithebitisha hatua hii na kuamua masharti ya kukabidhi.

Waingereza walihitaji jina jipya kwa ajili ya koloni mpya na tangu Januari 1920 wakaamua kuiita "Tanganyika Territory" kwa kutumia jina la ziwa kubwa upande wa mashariki ya eneo.

Sent from my iPhone
 
Hoja ya kipuuzi kabisa, kwa hiyo unataka tukwepe Wajerumani na Waingereza tujikabidhi kwa Sultani? hujui kwamba nchi yako ililazimishwa kuolewa na Zanzibar? Zanzbar wanaamua na kufanya kila kitu wakati Tanganyika haiwezi na inapotaka kujaribu lazima ikae na Zanzibar?
Mitanganyika mingine!
 
Hiyo Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961 na ikawa Jamhuri mwaka1962. Tena tukiwa na bendera yetu, kwa nini tusitumie hiyo wewe unatuwekea ya Mkoloni.... Anyway mipaka ya Africa iliwekwa na Wakoloni.
Endelea kuelezea Historia ikawaje hadi 1964
 
Mkuu Pascal Ndege,umepotoka.Kuidai Tangayika ni kuhakiki uhuru na kuutukuza uhuru tulioupata mwaka 1961. Iliyopata uhuru toka kwa wakoloni ni Tanganyika.Inayodaiwa ni Tanganyika. Kuna kosa gani kuidai? Halafu usichanganye uhuru wa nchi na ushirikiano.Uhuru kila nchi ina wake;ushirikiano ni wa hiari na hauonyeshi kuwa huru toka kwenye ukoloni.Kwa taarifa yako,wakoloni wanatawala tena nchi zetu kupitia ushirikiano uliopo.

Tanganyika ni ya mjerumani bali Tanzania ni zao la watanzania sasa unadai nchi ambayo sii yako akili matope

Sent from my iPhone
 
Last edited by a moderator:
Hiyo Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961 na ikawa Jamhuri mwaka1962. Tena tukiwa na bendera yetu, kwa nini tusitumie hiyo wewe unatuwekea ya Mkoloni.... Anyway mipaka ya Africa iliwekwa na Wakoloni.
Endelea kuelezea Historia ikawaje hadi 1964

Nimekueleza Tanganyika jinsi ilivyo siii yako wewe ni ya mjerumani sisi kama sisi ni watanzania na

Sent from my iPhone
 
Tunataka TANGANYIKA YETU, lugha zenu za ngonjera haziwez kutuziba midomo

watahangaika sana mwaka huu, na wakithubutu kuizuia italipuka kama bomu la nyuklia.
 
Tanganyika ni ya mjerumani bali Tanzania ni zao la watanzania sasa unadai nchi ambayo sii yako akili matope

Sent from my iPhone

Vipi tukidai tanzania bara, hiyo si ya kikoloni, nafikiri hapo utaunga mkono.
Msidanganyike na jina angalieni namna ya kuimarisha Muungano
 
Uko sahihi mkuu., Nilipendekeza serikali 1, na ikishindikana basi 3 lkn litangazwe shindano la kutafuta jina jipya la Tanganyika
 
Hoja ya kipuuzi kabisa, kwa hiyo unataka tukwepe Wajerumani na Waingereza tujikabidhi kwa Sultani? hujui kwamba nchi yako ililazimishwa kuolewa na Zanzibar? Zanzbar wanaamua na kufanya kila kitu wakati Tanganyika haiwezi na inapotaka kujaribu lazima ikae na Zanzibar?
Mitanganyika mingine!

Hata Tanganyika machifu walilazimishwa na wakauwawa yani muungano aliyoutengeneza mkoloni ndio sahihi ule wakijasili wa muafrika siyo sahihi lol ImageUploadedByJamiiForums1396529600.332411.jpg

Sent from my iPhone
 
Hivi Wakuu kwani kuna reshuffle ya Wakuu wa Wilaya hivi karibuni inakuja? Manake mada zingine bana zinashindikana hata kutetewa.
 
Back
Top Bottom