Danny Jully
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 4,416
- 3,867
Hapana mimi ni kilaza tu ila kwahili naona Giza tu kila Mtanzania haoni manufaa ya muungano wetu serikali ya Zanzibar ipewe madaraka zaidi Tanzania ibakie kama ilivyo Matatizo yanaisha Mbona south hatujaungana lakini tuenda bila viza? Ni udugu uliyokomaaa zaidi kuwa na TanzaniaView attachment 148930
Sent from my iPhone
Ni kweli kabisa utaendelea kuona giza kwa sababu hakuna aliye tayari kukubali kuwa hakuna nchi moja inayoitwa Tanzania, Tanzania ni muungano wa nchi mbili Tanganyika na Zanzibar na hilo hakuna asiyejua hivyo. Maswali magumu yanayopewa majibu rahisi ni vp Tanganyika isiwepo lakini Zanzibar iwepo. TANGANYIKA IKO WAPI?? Jibu rahisi imejificha kwenye koti la muungano! Hilo koti kwa nini halikushonwa kubwa ili litoshe kuificha Tanganyika na Zanzibar? Jibu jingine rahisi,eti Zanzibar ingemezwa kwa kuwa ni ndogo na kupoteza utaifa wao. Hapa ndipo kitendawili kingine kilipo...kwamba Tanganyika ipoteze utaifa wao lakini Zanzibar hapana! Ile saa ya ukombozi ya yule mchungaji asiye na kondoo sasa itimie...Hiyo Tanganyika ichomolewe huko ilikojificha kwenye koti la muungano nayo ionekane na hilo koti libaki lenyewe lisiwe na Zanzibar wala Tanganyika. Nchi zote mbili ziwe huru. Na tume ya Warioba imeeleza vizuri sana jinsi ya kuichomoa Tanganyika kwenye koti la muungano. Wewe unaposema Zanzibar ipewe madaraka kamili na Tanzania ibaki ilivyo...maana yake unakubali Tanganyika iwepo kwa sababu hakuna mamna nyingine ya Zanzibar kuwa na uhuru kamili bila kubadili mfumo uliopo wa muungano.